| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 9 | 18 November 2011 | Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011) | ||
Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue nafasi hii nimshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuweza kutufikisha hapa Bungeni tukiwa katika hali ya uzima. Mheshimiwa Spika, Muswada huu umekuja kwa wakati mwafaka kwa Watanzania ambao wanahamu na maendeleo ya nchi yao. Mheshimiwa Spika, ukiisoma Hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni ya upotoshaji sana. Hotuba ambayo haiwatakii mema Watanzania kwa ujumla. Mheshimiwa Spika, katika kuliona hili, ninaiomba Serikali iwe macho kuwaelimisha Watanzania waweze kuelewa madhumuni ya Muswada huu; kwa kuwa Watanzania wengi hawafahamu Katiba ni nini na hasa Wananchi ambao wanaishi Vijijini. Ninaomba nijikite kwenye Muswada, kifungu cha madaraka ya Rais, kama wanavyodai Wapinzani kuwa apunguziwe madaraka. Madaraka ya Rais, ninaomba yasiingiliwe na yaachwe kama yalivyo. Rais ndiye Mkuu wa Nchi na Rais huyo huyo ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, kumtaka apunguziwe madaraka, huko ndiko kumdhihaki Kiongozi wa Nchi. Mheshimiwa Spika, kwa maoni yangu na kwa kuwa Wabunge wengi wameshachangia mengi, ninaomba niseme Muswada huu umekuja wakati mwafaka na ujadiliwe ili hatua zinazofuata ziendelee. |
|||||