| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 43 | 10 August 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2011/2012 | ||
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongeza Waziri kwa hotuba yake. Naiomba Serikali iwashawishi wawekezaji kwa kuweka viwanda vya maziwa katika Jiji la Dar es Salaam kwa sababu maziwa ni muhimu sana kwa matumizi ya kila siku, hii pia itawapa wafugaji wetu kupata soko lenye uhakika pia ajira kwa vijana wetu zitaongezeka. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba viwanda vya ngozi kama SIDO viboreshwe kwa mikoa yote ambayo ina wafugaji wengi pia wapate soko lenye uhakika, pia wajasiriamali wataongezeka, na ajira zitapatikana. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara iwashawishi wawekezaji kwa kuweka kiwanda cha kusindika samaki kwa sababu samaki ni chakula muhimu sana pia ukizingatia upatikanaji wake ni wa msimu na uvuvi ni moja ya rasilimali katika nchi yetu hii itawapa moyo wavuvi wetu kwa kuwa na uhakika wa kipato chao pia vijana wetu wataelekea huko na kuweza kujiajiri wenyewe pia itasaidia kutoagiza samaki wa makopo toka nje. Kwa kuwa kule Zanzibar hasa Kisiwa cha Tumbatu kuna samaki wengi sana hii itapunguza umaskini kwa kuwa kutakuwa na soko lenye uhakika. Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. |
|||||