| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 34 | 27 July 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi | ||
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie upande wa uvuvi haramu. Hii itasaidia sana pindi Wizara ikitenga fedha na kuwaelimisha wavuvi wasinunue pia kutumia zana zisizokubalika na baadaye kufanya uvuvi haramu. Naiomba Serikali ikemee pia hatua kali ziwekwe na zifanyiwe kazi ili wanaoagiza nyavu ndogo wasiweze kuziingiza hapa nchini na baadaye kuvua uvuvi haramu. Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Wizara isimamie sana mradi wa MACEMP utakapomaliza mkataba wake iombe uendelee tena kwani umetusaidia sana hata kule Visiwani Zanzibar, nawapongeza sana kwa kutusaidia pia utaporudi utupe mafunzo na elimu ya uvuvi halali. Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. |
|||||