| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 29 | 20 July 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi | ||
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko mengi sana ya walimu wapya wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza kukosa mishahara yao kwa wakati, hivyo husababisha usumbufu mkubwa sana. Je, Serikali itawasaidia vipi au itaweka mikakati gani ili kusaidia walimu hao kupata haki yao haraka wanapoajiriwa? Ninaiomba Wizara ilifikirie sana suala hili ili kuepusha migogoro na pia kuwarahisishia na kuwapunguzia ukali wa maisha walimu wapya. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wanafunzi muda mrefu wanakuwa shuleni kuliko muda wanaokuwa nyumbani, ninaiomba Wizara ipange Mpango Maalum wa kuwafundisha watoto wetu elimu ya nadharia kama hatari za madawa ya kulevya, mimba za utotoni na madhara yake. Pia wapwewe elimu ya afya ya jamii. Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja. |
|||||