| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To |
|---|---|---|---|
| 6 | 8 | 9 February 2012 | Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review (Amendment) Bill, 2011) |
Mheshimiwa Spika, awali nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutia saini sheria hii ambayo ni muhimu sana kwa mustakabali mwema wa nchi yetu. Mheshimiwa Spika, kipengele cha kuwaondoa Ma-DC, sioni muafaka kwa kuwa Mkuu wa Wilaya ndiye mhusika mkuu wa usimamizi wa mwenendo wa siasa, amani na utulivu katika sehemu husika. Kwa hiyo, nahisi badala ya kumwondoa DC, ni vyema wakaongezwa Wakurugenzi/Makatibu ndani ya sheria. Siyo kweli kabisa kuwa Wakurugenzi/Makatibu kuwa hawana itikadi yoyote. Pili hawana amri ya kuwa na mamlaka ya kusimamia amani/siasa na utaalam wa mwenendo wa utawala kiujumla. Mheshimiwa Spika, ni vyema tukaainisha ni nani mwenye mamlaka ya kutoa elimu na sifa gani. Ambaye anastahiki sifa hizi lazima ziainishwe, la si hivyo, kutakuwa na hatari ya badala ya kuelimisha ukweli kutakuwa na upotovu wa elimu hiyo lakini pia ukusanyaji wa maoni lazima uratibiwe na Tume au wakala wake waliopewa kwa mujibu wa “Defined Criteria”. Ni imani yangu jambo hili litaleta utulivu katika ukusanyaji wa maoni. Siyo vyema kabisa kila mtu, kila kikundi, kila asasi au taasisi kuingia mtaani na kukusanya maoni. Huo ni unyimaji wa haki za mwananchi mmoja mmoja. Mheshimiwa Spika, kutokana na unyeti wa jambo hili, siyo vyema kupunguza kiwango cha adhabu kwa yeyote atakayesimamisha hatua za kupinga hatua za mchakato wa kusimamia utoaji wa elimu au ukusanyaji wa maoni. Maoni yangu, adhabu kali itumike kwani ni kosa la jinai. Mheshimiwa Spika, Katiba ili ipitishwe ni lazima iwe kwa simple majority ya asilimia zaidi ya 50. Siyo vyema kutokana na hali ya kisiasa hasa ZNZ ikiwekwa zaidi ya asilimia 60. Basi kutakuwa na mvutano wa kudumu ambao hata unaweza kuondoa amani na kuletea kurejewa kwa kupiga kura mara kwa mara utakaohusisha mirengo ya siasa zaidi badala ya uhalisia wa kitaifa. |
|||