You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 24 13 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili ni zito sana kwa Wanajeshi wetu hasa wenye vyeo vya chini, wameshastaafu wengi wao huwa hawana hata pahala pa kulala na kazi maalum za kujivunia kupata
kipato kwa siku za baadae. Kwa kuzingatia wengi wao wana nguvu na taaluma na ili wasijihusishe na mambo ya kihalifu napendekeza kwanza wapewe mkopo huku wakikatwa mara tu wanapoajiriwa ili waanze kujenga nyumba na makazi yao ya kudumu wakati wao wanakaa kambini.

Pili, kuwadhibiti na kutangatanga kwa kufunguliwa Cooperative (Ushirika) na kutumia nguvu zao kwa kuzalisha mali badala ya kuwa watchman au waganga na hata wahalifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi maalum natoa kwa mstaafu shujaa Bwana Juma Ali Khamis wa Zanzibar ambaye hana miguu kuanzia kwenye mapaja aliumia na bomu vita vya Kagera. Kwa wenye ulemavu, kama ni wachache basi wasaidiwe kwani bado wanategemewa na familia zao. Busara yeye angepatiwa bajaji ya kutembeza wageni ili ajikimu na maisha. Anakaa Saateni, Kambi ya JKU Zanzibar, Mheshimiwa Waziri anamfahamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uajiri kuna minong’ono mingi juu ya uajiri kwa wanajeshi JWTZ kuwa namba ya waajiriwa toka Zanzibar ni ndogo. Hili limekuwa kero miongoni mwa Wazanzibar. Ni busara uajiri ukafikiriwa kutokana na minimum requrements (vigezo vya chini) ili malalamiko haya yasiendelee. Vivyo hivyo juu ya upandishwaji wa vyeo. Wengi wanafika hata kuwahesabu watendaji jambo ambalo nadhani linaweza (makamanda) kuleta vuguvugu baya katika jamii ya Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mipaka na beacons kama hotuba ya Mheshimiwa Waziri ilivyojieleza, matatizo ya beacons yamejitokeza hata katika mazungumzo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa mwelekeo ulivyo na msimamo wa kuungana kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jambo hili linaweza kuleta kutofahamiana baina ya nchi zetu. Wazo langu, kipaumbele kitolewe katika kulimaliza tatizo hili la sivyo kero zitazidi kuendelea na mtangamano wa Jumuiya unaweza kuwa na matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza Jeshi letu jinsi lianvyojitokeza wakati wa maafa na kusitiri waathirika, ila napendekeza Jeshi pamoja na Kitengo cha Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu washirikiane kutoa taaluma za msingi (basic emergency preparedness and management) kwa watumishi wa sekta nyingine za Serikali kama inavyofanywa kwenye UKIMWI, ikiwezekana hata katika vyuo na (simulation events au cases) zifanywe kuleta umahiri na utayari kwa wananchi ili maafa yasiwe makubwa pindipo janga likitokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, nguvu na mazoezi ya pamoja ni muhimu kikanda. Ni imani yangu kuwa ulinzi wa pamoja ki-EAC ni imara zaidi kuliko nchi moja moja. Itakuwa vigumu adui kututeka kama ilivyotokea Afrika Kaskazini.

Mheshimiwa Naibu Spika, angalizo, kutokana na ukuaji wa sayansi ya kompyuta na mapigano yake kiutandawazi (cyber technological war) ni vema Jeshi likaongeza utaalamu wa ugunduzi wa hatari zinazoweza kutukabili. Ulinzi uwe imara hata katika matumizi ya twitters na facebook katika kuleta propaganda za chini kwa chini zisizo bayana. Hatari hiyo hivi sasa iko bayana kwenye blogs.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hivi sasa uchimbaji wa Uranium utaanza, inafaa Jeshi pia litayarishe wataalamu wa kugundua na hata kuzima matumizi mabaya kiulinzi katika nyanja zote (uchimbaji, usafirishaji, storing na processing) itambulike kuwa sio watu wote wema wako watakaotumia haya kwa njia haramu ya kuangamiza Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.