You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Khamis, Kheir Ali[CCM]

Kwamtipura Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 21 8 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mheshimiwa Naibu Spika, Muungano wa Tanzania ni kitu ambacho kinatakiwa kujadiliwa kwa makini zaidi. Muungano wa Tanzania ni silaha ya Watanzania dhidi ya maadui wa ndani na wa nje ya nchi hii.

Muungano wa Tanzania umetokana na ridhaa ya Watanzania wenyewe na siyo viongozi wawili yaani Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Mzee Karume waliwaita Wazanzibari katika Uwanja wa Karume House mwaka 1964 na kuwauliza wananchi kama wanautaka Muungano au hawautaki na wote wakakiri kuwa Muungano wanautaka. Mzee Karume alifanya hivyo kwa vile Baraza la Mapinduzi la wakati huo lilikuwa linachaguliwa na Rais badala ya kuchaguliwa kwa kura za wananchi na kwa hivyo uwakilishi wa wananchi usingepatikana. Mwalimu Nyerere aliwasilisha Bungeni pendekezo la Muungano ili kupata ridhaa yao kwa vile wao walichaguliwa na wananchi na kwa hiyo wanawakilisha mawazo ya wananchi wao. Kwa maana hiyo wananchi wa Tanganyika waliridhia Muungano huo kupitia kwa Wabunge wao. Kwa hiyo Muungano wa Tanzania uliridhiwa na Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muungano wa Tanzania wa Serikali mbili ni Muungano wa kisiasa na Muungano wa Serikali tatu ni mwelekeo wa Shirikisho ambao ni Muungano dhaifu. Ni kuzigawa nchi na mwelekeo wake ni kama ule wa Urusi alioufanya Goberchev kuigwa USSR. Mwalimu Nyerere alisema ukianza kuigawa nchi
mwisho wake utaigawa hata familia yako, kwa hiyo, Watanzania kuna haja ya kuwa makini na watu wa aina hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna haja ya kuimarisha Muungano kwa kushughulikia kero zilizojitokeza ndani ya Muungano ili uwe imara zaidi chini ya muundo wa sasa wa Serikali mbili, naunga mkono hoja.