| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 9 | 18 November 2011 | Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011) | ||
Mheshimiwa Spika, napenda kwanza kutoa sifa nyingi kwa Ris wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya M. Kikwete, kwa kukubali Muswada wa Katiba kujadiliwa na wananchi wote. Mheshimiwa Spika, kitu cha kwanza kabisa nachopenda kuongelea ni elimu ndogo waliyonayo wananchi ya uelewa wa mambo ya Katiba, hayo yote yanafuatia na Chama pinzani kuelezea kinyume na inavyokusudiwa. Kwa kifupi wananchi wengi hawajui kama Muswada huu umeshapitishwa au ndiyo umekuja Bungeni kupitishwa. Ndiyo maana umeleta matatizo. Mheshimiwa Spika, tunaomba Serikali ifanye kila njia na iwe wazi zaidi kwa kuwaelimisha wananchi kuwa sasa ni wakati wao wa kutoa maoni yao yaliyo moyoni mwao bila woga ili wananchi wa Tanzania wapate Katiba yao na tunawahamasisha kwamba nafasi hii hutokea mara chache katika maisha na kila mwananchi ajivunie kutoa mchango wake. Sijui hao wenzetu wanaitakia nini nchi hii, kama Uhuru tumeshaupata mwaka 1961, je, hao wenzetu wanataka uhuru gani? Naomba Serikali ilikazie macho jambo hili, tusiache amani tuliyonayo ikapotea na watu wenye uchoyo wa madaraka. Kama ningekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, naona hayo yangeisha, kwa nini watuchezee hivi? Wanafanya wanavyotaka, wao ni nani? Kwa nini tunawaonea haya? Hao wanataka tuwaonyeshe mfano kidogo washike adabu siyo kulitia Bunge letu Tukufu hasara kila siku mara wamo ndani mara nje. Naona tutunge Sheria waondokao au wasusao Bungeni bila sababu ya maana wasije vikao vitatu posho na mshahara wasipate. Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ubariki Muungano. |
|||||