| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 2 | 4 | 11 February 2011 | Hoja ya Kujadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais | ||
Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Mwenyenzi Mungu, kwa kunipa nafasi hii ya kuchaguliwa kuwa Mbunge ili niweze kuwawakilisha wananchi wa Jimbo langu. Pili, nachukua nafasi hii, kuwashukuru sana wale wananchi wa Jimbo la Kalenga, kwa kuniamini na kunipa nafasi hii niwawakilishe na naahidi kabisa siwezi kuwaangusha. Tatu, namshukuru mke wangu Jane, kwa uvumilivu wake wakati wa kampeni na katika shughuli hizi za kisiasa nikiwa mbali naye. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakishukuru sana Chama hasa Rais kwa namna ya pekee alivyofanya kazi na anavyoendelea kufanya kazi kwa ajili ya nchi hii. Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, naomba kuchangia na nitachangia upande wa elimu na uchumi na nitagusa matatizo ya Jimbo langu yanayoendana na kipengele namba tisa ambacho Mheshimiwa Rais amegusia masuala haya. Mheshimiwa Spika, upande wa elimu kama walivyozungumza wenzangu, kuna maeneo ambayo napenda kuyasisitiza. Ni kweli tumefika mahali ambapo sasa si vizuri kulaumu tunakotoka, tunatakiwa tuzungumzie tufanye nini. Tumepata matatizo na tunaambiwa sasa hivi World Bank imetoa msaada wa Dola milioni 1050 ikielekeza kwanza kutupa nafasi ya kufundisha Walimu zaidi, kujenga nyumba 1200 za Walimu, kukarabati nyumba 500 za Walimu, kujenga maabara na vilevile kusaidia capitation grant ya shilingi 25,000/- kwa kila mwanafunzi. Huu ni msaada mkubwa na nichangamoto kubwa lakini niseme bado hilo halitoshi. Mheshimiwa Spika, bado tuna matatizo makubwa ya madawati katika shule zote za msingi na sekondari. Mimi mwenyewe nimefanya tathmini katika Jimbo langu, katika shule zote za msingi nimepata upungufu wa madawati 5,289 na katika shule za sekondari 15 katika Jimbo langu nimepata upungufu wa madawati 689. Hii yote ina maana kwamba bado tuna kazi kubwa ukiachilia mbali suala la kuongeza zaidi nyumba za Walimu. Ili performance ya shule iboreke, tunahitaji ku-combine msaada huo na kuelekeza nguvu za Serikali na wananchi. Mheshimiwa Spika, sasa nini kifanyike? Pendekezo langu ni kwamba Serikali katika Bajeti inayokuja itenge kiwango kikubwa kuliko kiwango kilichokuwa katika Bajeti iliyopita ili kuelekeza katika upungufu huu. Mpaka sasa hivi, Serikali ilikuwa inatenga asilimia 18 katika Bajeti lakini napendekeza iwe zaidi katika kiwango cha pesa zitakazopatikana ili tuboreshe elimu maana hakuna mbadala wa elimu na kitu chochote. Mheshimiwa Spika, baada ya kuwa nimesema hilo la upande wa elimu, naomba sasa kuzungumzia upande wa uchumi. Ni sahihi kabisa kama Mheshimiwa Rais alivyozungumzia, akaweka kipaumbele namba mbili na namba tatu. Namba mbili akizungumza namna tunavyohitajika sasa kuboresha uchumi katika nchi hii. Sina sababu ya kurudia kutoa takwimu za hali halisi ya kudorora kwa uchumi lakini katika hali tuliyonayo, napendekeza yafuatayo katika kipengele namba mbili. Mheshimiwa Spika, cha kwanza, kwa mtizamo wangu wa dhati kabisa, tunahitaji sasa kuboresha zile sera ambazo zina-promote performance ya uchumi. Sera zile lazima ziwe zinalenga majority kwa maana ya percentage kubwa ya watu walio vijijini. Sasa contribution hiyo italeta mkusanyiko, combination kubwa ya kuboresha uchumi katika nchi, Sera ambazo zinalenga kuhamasisha watu walio wengi waingie katika msukumo wa kuzalisha. Mheshimiwa Spika, la pili, tunahitaji kuboresha Sera za Uchumi ambazo zinalenga percentage ya performance at around seven percent rate of economic growth. Hii single digit katika umaskini tulionao Tanzania, haitoshelezi. Nchi tajiri ni sawasawa hata uki-perform one or two percent kwa sababu ni developed country is okay lakini kwetu haitoshelezi tunatakiwa tu-perform at a level of two digits. Mheshimiwa Spika, mkakati wa tatu katika huo uchumi, tunatakiwa tuangalie zile Sera ambazo zinafanya uchumi ziwe sustainable kwa maana kwamba tukishakuwa na sera zenye msukumo, kwanza watu wengi waingie katika performance ya uchumi na pili zile zinazolenga ku-target ku-perform katika rate ipi, tatu ni sera ambazo ziko sustainable, tusiwe na sera ambazo zinabadilika kila wakati, tutakosa consistence ya investment. Mheshimiwa Spika, la mwisho, naomba nizungumzie kipengele namba tisa kama Mheshimiwa Rais alivyosema, ni suala la ku-invest. Sasa katika critical resources zitakazosaidia hii performance iwepo, tuwe na umeme, tuwe na full exploitation za energy. Katika Jimbo langu la Kalenga, kuna vijiji vikubwa ambavyo vinastahili kuwa na umeme. Tuna kijiji cha Magulilwa, Mugama, Kiponzero na kijiji cha Wasa. Vijiji vikubwa na vina shule kubwa, vina taasisi kubwa na vina watu wengi. Katika mwelekeo wa vipaumbele vya Rais, ni vizuri sana kutazama namna hii ili tuweze kueneza umeme katika vijiji hivyo. Mheshimiwa Spika, vilevile tunahitaji kuboresha barabara inayounganisha Kalenga na Hospitali Teule ya Ipamba. Barabara hiyo naomba ichukuliwe na Serikali Kuu kusudi kurahisisha usafiri wa wagonjwa wanaokwenda kupata huduma katika Hospitali ya Ipamba. Naomba sana suala hilo lizingatiwe. Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kumshukuru Rais katika vipaumbele hivyo alivyoviweka mbele yetu na mwisho kabisa naunga mkono hoja ya hotuba ya Rais. |
|||||