You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Badwel, Omary Ahmad[CCM]

Bahi Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 23 12 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu mkubwa wa watumihsi katika Halmashauri zetu hususan Bahi ni jambo la hatari sana. Wilaya ya Bahi ina upungufu wa zaidi ya 51% ya watumishi katika sekta ya afya. Waziri atuambie mkakati wa Taifa wa kuhakikisha suala hili la upungufu wa watumishi linatatuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna watumishi wa zamani waliostaafishwa kwa kubana matumzi ya Serikali miaka ya 1990 kwa nini sasa wasirudishwe kazini ili kupunguza idadi ndogo ya watumishi waliopo?

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri nyingi zimejipanga kutekeleza mpango wa Serikali wa kila kijiji kuwa na zahanati ikiwemo wilaya yangu ya Bahi, lakini tatizo kubwa ni watumishi ambao hawaletwi na Serikali ili zahanati zilizojengwa ziweze kufunguliwa mfano wilaya ya Bahi ina zahanati sita katika vijiji vya Ibugule, Zejele, Chali Makulu, Nghulugano na Mindola ambazo wananchi na Serikali wamefanya kazi kubwa kuzikamilisha lakini hadi sasa hospitali hizo hazijafunguliwa. Jambo hili
linafifisha sana mioyo wa wananchi kuchangia ujenzi wa zahanati hizo na kwetu wanasiasa hasa Madiwani na Wabunge kuwa mtihani mkubwa sana. Sasa napenda kujua ni lini Serikali italeta watumishi wilayani kwangu Bahi ili zahanati hizo zifunguliwe?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini MSD inapokea fedha za dawa toka katika zahanati zetu na wakati mwingine hawaleti dawa kwa mujibu ya idadi ya fedha na dawa zilizoombwa licha ya kutoleta dawa hizo lakini pesa zilizobaki hazirudishwi kwa zahanati hizo. Je, Wizara inasema nini juu ya hili?