You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Mansoor, Shanif Hiran[CCM]

Kwimba Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 2 6 April 2011 Hoja za Kamati
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naomba nichangie sehemu ya pili, 2.2, inayohusu TRA. Mimi nashauri Serikali ingefuta misamaha ya kodi ya mafuta na misamaha mingine yote ambayo inatolewa na Custom and Excise Department ya Tanzania Revenue Authority na ipelekwe kwenye Income Tax Department, maana wawekezaji watatulipa pesa nyingi customs tutamia. Serikali itakuwa imepata pesa nyingi bila riba na ile misamaha ihame income tax, maana wao wanafanya biashara kwa faida yao, wana-deduct ile benefit ambayo wangeipata kwenye customs. Hii itawafanya waoneshe faida ndani ya biashara zao ili waweze kurudisha pesa zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, mauzo ya dhahabu na almasi yananyonywa na wawekezaji. Ninashauri madini haya yauzwe kupitia Benki ya Tanzania ili pesa za malipo zilipwe kwenye akaunti itakayokuwa BoT. Hii itaipa Serikali fursa ya kupata pesa za kigeni kwa gharama za juu na pia tutaweza ku-monitor mali yote wanayo-export.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa pia kuchangia mapato ya Serikali kwenye makampuni makubwa; kwa mfano, BP Tanzania, Mbeya Cement, TIPER na Airtel. Tunaomba yafuatiliwe mapato kwenye mauzo ya Zain, Celtel na Airtel; capital gain tax tumepata shilingi ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ningependa kuchangia matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na Wizara ya Miundombinu, kwa kubomoabomoa nyumba bila sababu na kufanya Serikali ilipe pesa nyingi sana ambazo zingefanya kazi nyingine za maendeleo. Nashauri Wizara ya Ujenzi ijipange kulipa Wakandarasi ili wajenge barabara na waache kufuata watu. Ahsante.