You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Amer, Abdulsalaam Selemani[CCM]

Mikumi Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 17 1 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 - Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Nampongeza Waziri Mkuu kwa Hotuba na hali halisi ya nchi yetu. Nakwenda moja kwa moja kwenye uwezeshwaji wa wananchi kiuchumi na kuongeza ajira. Katika kutekeleza Ilani ya Chama Tawala, CCM tumeweza kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi kwa
ajili ya kuwezeshwa kwa mikopo na kujiletea maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iwezeshe Wizara ya Ushirika na Masoko kwa kuongeza Bajeti ili kutimiza azma ya Serikali ya Chama Tawala yaani Chama cha Mapinduzi kuondoa umaskini nchini. Maofisa Ushirika katika ngazi ya Wilaya ni kama wamekufa kwani Idara hii katika Halmashauri inadharauliwa sana kama haipo. Naiomba Serikali kupitia Wizara hiyo ya Ushirika na Masoko itoe fungu moja kwa moja kwenda katika Halmashauri za Wilaya, kwa kweli itasaidia sana katika kuelimisha wananchi na pia Semina kwa kuweza kuanzisha SACCOS katika kila Kata.

Mheshimiwa Spika, pamoja na nia nzuri ya Serikali kuwawezesha wananchi kupitia SACCOS na vikundi vilivyoundwa, itungwe Sheria au kuunda moja ya Mashirika ya kufungua Benki nchini kuwakopesha SACCOS kwa riba nafuu ili iweze kuwakopesha wananchi kwa riba nafuu. Naamini kwa riba ya sasa hata kama atafanya biashara lakini hawezi kumudu kulipa deni.

Mheshimiwa Spika, naamini kwa kampeni tuliyofanya na tuendelee kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi ili tuweze kuondokana na umaskini na kuongeza ajira. Naomba Serikali iziombe Taasisi zote zinazotoa mikopo au zinazowezesha kufungua Ofisi zao kila Mkoa ili ziwe karibu na walengwa kuepuka gharama za ufuatiliaji. Mheshimiwa Spika, nashukru na naunga mkono hoja.