You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Kigola, Mendrad Lutengano[CCM]

Mufindi Kusini Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
8 13 29 June 2012 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2012/2013 – Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mheshimiwa Spika, kwa
kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni ofisi muhimu sana katika
kuratibu utaratibu wote katika Halmashauri zetu ili
kusimamia maendeleo ya Mikoa na Halmashauri zote
nchini Tanzania, naomba kutoa ushauri kwa Serikali
kama ifuatavyo:-

(i) Katika Halmashauri kuna mali nyingi sana za
Serikali lakini usimamizi wake bado duni kwa mfano
Kitengo cha Manunuzi bado hakijaimarishwa. Fedha
nyingi sana zinapotea kupitia kitengo hiki. Kwa hiyo,
Serikali iimarishe usimamizi madhubuti katika kitengo
hiki kwa kufuata Sheria ya Manunuzi.

(ii) Naomba Halmashauri zetu kuwa na miradi ili
kupata mapato ya ndani siyo kutegemea ruzuku
kutoka Serikali kuu.

(iii) Halmashauri zina wawekezaji ambao wana
miradi mikubwa kwa mfano viwanda vya chai,
viwanda vya mbao na viwanda vya karatasi ambavyo
vipo katika Jimbo la Mufindi Kusini, Wilaya ya Mufindi.
Kwa hiyo, Halmashauri inaweza kufaidikia kupitia
viwanda hivi kwa kupewa mrahaba kutoka katika
viwanda hivi.

Mheshimiwa Spika, suala la maji, katika vijiji vingi
hapa Tanzania wana tatizo la maji, ndiyo maana
Wabunge wengi sana wanauliza maswali ya maji hasa
miradi wa World Bank bado haitekelezeki. Naomba
Serikali itafute njia nyingine ili kutatua tatizo hili la maji.
Katika Jimbo la Mufindi Kusini, kuna Vijiji vya Sawala,
Kibao, Rufuna na Kipande. Wananchi wanapata shida
ya maji, wananchi wameshachangia fedha mpaka
sasa fedha zao zipo benki lakini Serikali bado
haijapeleka maji kwa mradi huu wa World Bank.

Mheshimiwa Spika, maji ni tatizo kubwa sana
katika Jimbo la Mufindi. Serikali kwa kushirikiana na
wananchi wa Jimbo la Mufindi Kusini walijenga matanki
ya maji katika vijiji vya Sawala, Kibao, Igowole, Nyololo,
Maduma na Nyigo lakini miundombinu yake
imechakaa sana mpaka sasa hivi matanki hayo
hayatumiki sababu miundombinu yake imechakaa.
Naiomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili
kukarabati miundombinu ya maji katika Jimbo la
Mufindi Kusini.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kujenga
barabara kwa kiwango cha lami, barabara ya Nyololo
– Igowole – Kibao – Mtwango – Mgololo. Ni barabara
muhimu sana katika uchumi wa Taifa kwa ujumla
sababu imepita katika viwanda vikubwa vya chai,
mbao, karatasi na viwanda vidogovidogo vya
wajasiriamali. Pia kuna idadi ya watu wengi wanaoishi
katika barabara hiyo. Naiomba sana Serikali
kulichukulia hili kuwa ni tatizo kubwa katia Jimbo la
Mufindi Kusini.