| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To |
|---|---|---|---|
| 4 | 36 | 29 July 2011 | Makadiriio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi |
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hilo hilo ambalo nilitaka mwongozo wako. Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na utamaduni wa siku kadhaa, hotuba nyingi sana zimepitishwa kwa guillotine na ni kwa sababu wakati wote Meza imekuwa ikiongeza nusu saa tu ile inayoruhusiwa na Meza bila kutengua Kanuni na kadhalika. Sasa, naomba mwongozo wako kuhusu jambo hili ambalo tunataka kulifanya hivi sasa. Kwa mujibu wa maelezo uliyoyatoa, ni kwamba tunakwenda kwenye fungu 51 na Wizara hii ilipaswa tuanze na fungu la 14. Tafsiri yake ni kwamba watu wakishashika mshahara wa Waziri kwenye fungu la 51 kwa wingi, tutafikia hatua muda utakwisha halafu moja kwa moja tutakwenda kwenye guillotine na vifungu ambavyo kiutaratibu tungeanza navyo, tunaanza na 51 badala ya kuanza na 14. Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba mwongozo wako ili tuweze kwenda kwa kadri ya utaratibu, tuweze kuanza na fungu la 14 ili tukifika wakati ule wa fungu la 51, tupate fursa ya kutumia Kanuni kuongeza muda tuitendee haki hii Wizara ambayo ni Wizara muhimu sana kwa Taifa letu. |
|||