You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 31 22 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kupitia kifungu hiki cha Mshahara wa Waziri, ningeomba kupata ufafanuzi kuhusu jambo moja la Kisera. Ninaelewa kwamba, jukumu mojawapo la Kisera la Wizara hii ni kujenga taswira pana ya nchi yetu Kimataifa. Sasa kuna suala mahususi ambalo nililiuliza kuhusiana na tuhuma juu ya Watanzania kushiriki kwenye masuala ya uuzaji wa silaha haramu ambazo zinachafua taswira ya nchi yetu.

Ninaelewa kwamba, Mheshimiwa Membe, analifahamu jambo hili, kwa sababu mwaka 2000 lilijadiliwa kwenye Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa na mwaka wa
2006 lilijadiliwa vilevile Umoja wa Mataifa. Sasa ningependa kupata kauli ili tusichafuke kama Watanzania, kwa sababu ya matendo ya watu binafsi kuhusiana na tuhuma hizi hususan tuhuma zinazoihusu Kampuni ya Meremeta, kwa sababu wengi wamezoea kufikiria kwamba, ilikuwa ni kashfa sijui ya utoroshaji wa madini peke yake na ufisadi wa pesa za Watanzania shilingi bilioni 100, lakini kuna tuhuma nzito vilevile za kuhusiana na utoroshaji wa silaha. Kwa hiyo, ninaomba ufafanuzi kuhusu hilo.