You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Ahmed, Rukia Kassim[CUF]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 4 14 June 2011 Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2011/2012 – 2015/2016
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuchangia Mpango huu wa Maendeleo wa Miaka Mitano kwa njia ya maandishi. Mpango huu iwapo utatekelezwa kwa vitendo na kwa ufanisi na uwajibikaji na sio kwa maneno tu kubakia vitabuni, utaleta mafanikio makubwa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanikiwa kuiwezesha reli ya kati kufanya kazi, itakuwa ni hatua moja ya muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu. Reli ni kiungo muhimu katika sekta ya usafirishaji wa hitaji linalotegemewa na Mikoa mingi na hata nchi jirani ambazo hazina bandari, kwa kusafirisha shehena kubwa za mizigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango umepangika lakini wasiwasi wangu ni juu ya ufanisi katika utekelezaji kwani uzoefu unaonesha kuna uzembe, ubadhirifu na matamanio binafsi kwa Watendaji wetu hasa wale wa ngazi za Wizara na Taasisi za Kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.