You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Abama, Mwanamrisho Taratibu Maalim[CHADEMA]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 29 20 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mheshimiwa Spika, katika
kuchangia kwa maandishi hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba
kuchangia mambo matatu. Mambo hayo ni Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi na Walimu.

Mheshimiwa Spika, nikianza na Elimu ya Awali, kwanza kabisa kama tunataka
elimu yetu iwe bora, ni lazima mtoto aandaliwe kwa Elimu ya Awali na hivyo basi, mtoto
asomeshwe kwa vitendo ili atakapoingia katika Elimu ya Msingi asiwe mgeni na masomo
atakayoyakuta huko. Maana katika Elimu ya Awali, mtoto anakuwa au shule nyingi za
awali, watoto huwa wanasomeshwa masomo kwa Kiingereza hasa zile za kulipia. Kwa
hiyo, ni ushauri wangu kwamba hata hizo za Serikali ambazo ziko kwenye Halmashauri,
basi nazo ziboreshwe angalau mwanafunzi akitoka hapo akiingia Shule ya Msingi,
anaendelea na siyo kuanza Alifu.

Mheshimiwa Spika, kwanini tusiboreshe mitaala yetu ya Elimu ya Msingi ili
mtoto anapotoka katika Elimu ya Awali asiyaone masomo mageni? Kwani Elimu ya
Awali huwa wanasoma Kiingereza zaidi. Baadhi ya shule cha kusikitisha anapoingia
elimu ya msingi ni Kiswahili kitupu, kwa hiyo, hapo unamrudisha nyumba na ndiyo
maana elimu yetu inakuwa bora elimu tu na siyo elimu bora.

Mheshimiwa Spika, nikija katika elimu ya msingi, wakati sasa umefika kurejesha
elimu hii ya msingi ya kusoma kwa vitendo. Nakumbuka niliposoma mimi kipindi cha
Sayansi huwa tunapelekwa laboratory kusoma kwa vitendo, tunafundishwa jinsi ya
kuchuguza kitu kwa Microscope, tunajifunza kwa makundi. Hali kadhalika katika siku za
project tunapelekwa shamba kulima, kupanda na kuvuna. Pia wakati wa mavuno au kazi
za mikono hapo inakuwa tunafundishwa ubunifu wa kutengeneza vitu kwa mikono.

Mheshimiwa Spika, naomba haya yote yarejeshwe, kwani mtoto akitoka hapo
siyo lazima apate ajira Serikalini, yeye atakuwa na uwezo wa kujiajiri mwenyewe kwa
sababu hiyo VETA siyo wananchi wengi wanaoweza kulipia watoto wao kwenda pale
kusoma, jamani lazima tuwafikirie walio wengi siyo matajiri, ni masikini hasa.

Mheshimiwa Spika, nikiwa kwa walimu ni watu waliosahaulika kabisa hata
mishahara yao basi haikidhi haja. Kwa wanavyolitumikia Taifa hili karibia toka Rais hadi
Mwenyekiti wa Kata anatokana na Mwalimu. Imefika wakati sasa tuwape motisha
walimu wetu ili bado waendelee kusomesha kwa bidii ili Taifa lipate wataalam.
Tunakoendea, tuwatunze walimu wetu. Katika bajeti hii shilingi bilioni 525.941 ni kwa
ajili ya matumizi ya kawaida. Kwanini pesa hizi zisitiwe kwenye kwenye mishahara ya
walimu ili basi wapate kufanya kazi kwa ufanisi zaidi?

Mheshimiwa Spika, katika pesa za maendeleo, shilingi bilioni 139.632 ni pesa
kidogo sana. Kwa kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, maendeleo gani utayafanya?
Naomba hapa nifahamishwe.

Mheshimiwa Spika, kwanini hatubuni njia mbadala ya haya yote ili tuwe na elimu
bora ili nayo iweze kutoa walimu bora pia tupate wanafunzi bora tuondokane na bora
elimu?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.