| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 17 | 1 July 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 - Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa | ||
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuchangia kwa maandishi hotuba hii. Mheshimiwa Spika, ni miaka 47 sasa toka Muungano wetu ulipoasisiwa na viongozi wetu ambao ni Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Abeid Amani Karume, na kumbukumbu yangu, kuna mambo walikubaliana yawe ya Muungano na mengine yasiwe ya Muungano. Mheshimiwa Spika, kama sitakosea, ofisi yako ndiyo inashughulikia mambo hayo na hadi leo hii bado Wazanzibar wanalalamikia utekelezaji wake ambao unakwenda kwa kusuasua sana na vikao hivyo utekelezaji wake hautoi matunda kwa Zanzibar. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni nchi ambayo imeasisi ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Tanzania, Muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar na bado kuna kasoro za Muungano hazijamaliza kutatuliwa. heshimiwa Spika, naomba kwanza kabisa zimalize kutatuliwa kero zote ili Tanzania itapojiunga na jumuiya hiyo, basi Zanzibar iingie nayo kama nchi. Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia eneo la huduma za jamii. Tatizo kubwa la miradi ya maendeleo vijijini na mijini ni kuwa miradi hiyo huwa haiendelei hasa mradi wa maji wa TASAF, mradi huu ni wa kuchimba visima, lakini hauna ushughulikiwaji wa mgao wa maji kwa wananchi ambao wanapata taabu sana ya maji na visima vipo, lakini vimefungwa na hutolewa kwa nadra tu. Mheshimiwa Spika, nashauri kwamba miradi yote ya maendeleo inayopelekwa mijini na vijijini ni lazima kuwepo na mwangalizi ambaye atatoa taarifa endapo tu kutatokea hujuma maana kumfungia mwananchi maji ni hujuma. Mheshimiwa Spika, kuhusu kudhibiti Ukimwi, kama ulivyosema, hivi sasa umeanza kuona dalili za kutia moyo na wananchi wamepata mwamko, na pia wananchi kiasi wanajitolea sasa bila uwoga kwenda kupima afya zao na kama mtu ameathirika huenda kujiunga na kuanza dozi. Mheshimiwa Spika, nilisikia kuna dawa ambayo ni chanjo ambayo ukichanjwa hupati HIV. Je, kuna watu wangapi walipata chanjo hiyo na mpaka leo hii hatukuisikia kuletwa ila kuna dawa za ARV ambazo humzidishia mgonjwa matumaini ya kuishi. Mheshimiwa Spika, mara nyingi huona vituo vya huduma ya kutoa ushauri nasaha huwa vinashughulikiwa na watumishi ambao wao hawajaathirika na huwa wanafanya ubadhilifu wa kutoa vyakula kwa waathirika ambao vyakula vile ni kwa ajili yao. Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwamba vituo vya huduma nasaha vishughulikiwe na wanaoishi na HIV wenyewe kwani wapo wenye elimu na wasomi kwani wanakuwa hawawanyanyapai wenzao maana na wao pia ni waathirika. Mara nyingi Sekta hii bajeti yake ni kubwa lakini haiwafikii walengwa ila wanafaidika wazima ambapo sio lengo la kufikia “Tanzania bila ya Ukimwi inawezekana.” Mheshimiwa Spika, tukitimiza wajibu wetu, yote haya yanawezekana. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. Ahsante. |
|||||