You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Chatanda, Mary Pius[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 17 1 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 - Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Hotuba
aliyoiwasilisha Waziri Mkuu na kuiunga mkono. Hata hivyo, yapo baadhi ya mambo
ambayo yanahitjika kusimamiwa kwa karibu ili utekelezaji uweze kuwa wa ufanisi
mkubwa. Mambo hayo ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa ndiyo Viongozi Wakuu katika
ngazi ya mwanzo ya Uongozi wa Serikali, lakini walio wengi hawayaelewi vizuri
majukumu yao, kutokana na kuchaguliwa na kutopatiwa mafunzo. Hivyo; ni muhimu
sana kada hii ya uongozi ipewe umuhimu mkubwa wa mafunzo kwa sababu kero nyingi
zinatokana na Wananchi wanaowaongoza katika maeneo yao; na hivyo hushindwa
kuyakabili kutokana na kutozijua taratibu au baadhi ya sheria ndogondogo wanazotakiwa
kuzitumia. Sambamba na hilo, baadhi ya Wenyeviti wa Mitaa/Vijiji wamekuwa vyanzo
vya kero kwa kutumia nafasi zao vibaya kama vile utoaji wa vibali na uuzaji wa maeneo
ya vijiji bila ushirikishi, kinyume na sheria na taratibu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo, ninashauri
Wenyeviti/Serikali za Vijiji; ili tuweze kufaulu suala zima la Kilimo Kwanza, uwepo
utaratibu wa kila Kiongozi wa Kijiji kuwa na shamba la mfano wa Kilimo Bora. Hii
itasaidia Viongozi hawa wanapohimiza suala la Kilimo Bora, waweze kuelezea mifano
waliyoifanya wao kwanza na Wananchi wengine watafuata. Aidha, lipo tatizo la Maafisa
Ugani kutowajibika ipasavyo katika maeneo waliyopangiwa kutokana na kutokuwa na
vitendea kazi kama vile usafiri wa kumwezesha kuyazungukia maeneo aliyopangiwa,
hivyo kumfanya akate tamaa na yeye kuungana kuwa mwanakijiji. Ninaishauri Serikali
iangalie namna ya kuwawezesha Watendaji hawa ili waweze kusimamia shughuli za
kilimo katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo la Watendaji wa Halimashauri kukaa eneo moja
kwa muda mrefu (miaka 10 - 20), bila uhamisho, jambo ambalo linasababisha kuzoeleka
na Wananchi na kuwa chanzo cha kutumika vibaya na wale wasioitakia mema nchi yetu.
Ninaishauri Serikali, Watumishi wawe wanahamishwa ili kuzinusuru Halmashauri. Kada
zinazotakiwa kuhamishwa ni Wakurugenzi, Waweka Hazina, Maafisa Utumishi, Maafisa
Mipango na Madaktari.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja.