You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Changulla, Josephine Tabitha[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 9 21 June 2011 Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2011 na Mwelekeo wa Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka 2011/2012 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012
Mheshimiwa Spika, ninapenda kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kwa Hotuba yake nzuri sana. Ninaipongeza Kamati husika. Pia ninatoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine, kufanikisha matayarisho ya Bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ninaomba nichangie katika Bajeti hii. Bajeti hii ni nzuri sana na imetulia, kwani imegusa makundi yote; vijana, akina mama, watoto na akina baba.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Mwaka 20118/2012, ina vipaumbele vifuatavyo:-

kwanza ni umeme, mishati ya umeme ni muhimu sana katika maisha ya Mtanzania wa kawaida. Umeme unarahisisha maisha yetu. Niiombe Serikali ijitahidi sana kutimiza ahadi zake inazozitoa kwa Wananchi wake. Umeme siyo starehe au anasa, bali ni maendeleo.

pili, ni maji, maji ni muhimu sana katika maisha ya Mtanzania; hivyo, ninaiomba Serikali iliangalie tatizo hili kwa macho mawili; kwa mfano, tatizo la ukosefu wa maji Mkoani Geita limekuwa likichangia kwa kiasi Fulani, kukua kwa umaskini, kwani akina mama wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi sana na nguvu nyingi katika kutafuta maji badala ya kufanya kazi zao za kila siku za ujenzi wa Taifa.

Tatu, miundombinu, miundombinu kwa Taifa letu ni tatizo; ninaishukuru sana Serikali kwa kuliona hilo. Mkoa wa Geita ni Mkoa mpya, kwa maana hiyo unakabiliwa na changamoto nyingi; barabara mbovu, kwa mfano, barabara inayotoka Geita – Msalala kupitia Nyang’wale ni mbaya sana, ninaiomba Serikali iifikirie.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimalizie kwa kuipongeza sana Serikali inayoongozwa na chama chetu cha Mapinduzi, Chama Dume, kwa umakini wake katika kujali na kusikia vilio vya wanyonge na Wananchi wake kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja.