| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 46 | 13 August 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 - Wizara ya Nishati na Madini | ||
Mheshimiwa Spika, napenda kushukuru Serikali kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Najua Wizara hii inasimamia sekta nyeti yenye migogoro mingi kwa sababu Watanzania wengi wanaihitaji. Hata hivyo, napenda kupongeza mipango inayoendelea hususani ya umeme katika Mkoa wa Simiyu, katika kitabu cha bajeti nimeona jinsi utaratibu wa usambazaji umeme vijijini ulivyopangwa kutekelezwa lakini pia katika utendaji halisi nimeshuhudia jinsi nguzo zinavyosambazwa na nyaya kutandazwa katika maeneo mengi ya Mkoa wa Simiyu mfano Kata ya Bariadi - Nkolola, Bariadi - Kilala na Bariadi Sapiwi - Mkula - Lamadi. Hii ni hatua njema hasa ukizingatia maeneo mengi ya Mkoa wa Simiyu yanakaribia kuwa jangwa kutokana na kuisha kwa misitu. Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Simiyu kuna Viwanda vingi vya Pamba hivyo kupatikana kwa umeme wa gridi kutapunguza gharama ya uendeshaji wa viwanda hivyo. Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa linaloikabili nchi hii sasa ni kukatika kwa umeme na migao. Hii ni matokeo ya kutegemea zaidi umeme wa maji, naomba tutoke huko kwa haraka sana tuweke nguvu kuzalisha umeme usiotegemea maji. Iwapo tukifanikiwa hili, nchi yetu itaweza kujikomboa na kuimarisha uchumi wetu. Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. |
|||||