You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Minza, Esther Lukago Midimu[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
2 6 15 February 2011 Kujadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hotuba yake nzuri aliyolihutubia Bunge. Pia napenda kukupongeza wewe Spika, kwa nafasi hiyo uliyoipata.

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Mheshimiwa Rais imezingatia vipaumbele vyake alivyoainisha katika hotuba yake. Naomba nami nichukue nafasi hii kuchangia hotuba hiyo na hasa kuhusu kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, naishukuru sana Serikali kwa kuhamisha uanzishwaji wa SACCOS na VICOBA. Kwa kweli SACCOS ni mkombozi wa wananchi katika kuondoa umasikini. Ushauri wangu ni kwamba, SACCOS hizi ungetafutwa utaratibu wa kuziwezesha ili lengo la kuondoa umasikini kwa wananchi wetu liweze kwenda kwa kasi zaidi.

Vile vile, majengo yanayojengwa kwa ajili ya kuasaidia vijana wetu maarufu kama wamachanga yajengwe katika Mikoa yote kusaidia vijana kutokuwa wazururaji na kujiajiri.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hotuba hii.