| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 9 | 18 November 2011 | Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011) | ||
Mheshimiwa Spika, Serikali ihakikishe inaimarisha Sheria zaidi kwani uharibifu umekuwa mkubwa wa kufuja mali za umma, bila hatua zozote kuchukuliwa na uonevu uliokithiri na hasa Mahakamani na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Mheshimiwa Spika, Serikali iweke Sheria itakayowazuia (wabana) wezi wa mali za umma kuliko wanavyofikiria sasa kwani Sheria zilizopo sasa zinawapa uhuru uliopitiliza. Mheshimiwa Spika, Sheria iwekwe ya mtumishi wa Serikali ngazi za juu kutokukaa au kushika nafasi ya utendaji kwa miaka mingi hasa Makatibu wa Wizara na Wahasibu wao. Uwepo utaratibu wa watumishi kuzoea kupanda na kushushwa katika utumishi wao. Mheshimiwa Spika, nchi haiwezi kwenda mbele kwa Sheria zilizozorota hata Mtendaji wa Kijiji au Kata akichangisha na kula hakuna Sheria inayombana na matokeo yake huhamishwa kwenda eneo lingine ikiwa wananchi watalalamika. Mheshimiwa Spika, kila mwenye Mamlaka ya kushika hela tulipofikia sasa ni yake siyo tena ya Serikali hata taarifa zao utafikiri zimeandikwa Mbinguni zikionyesha maendeleo ya hali ya juu wakati hela zote zikiwa zimeliwa. Hii hupelekea wananchi kushikwa na ghadhabu na kukichukia Chama kilichopo madarakani. Mheshimiwa Spika, kumweka mtu madarakani hasa nafasi moja mwenye cheo kikubwa chenye maslahi ni kujichimbia kaburi na unapomwondoa katika madaraka unatafuta kifo wewe. Mheshimiwa Spika, nashauri, kwanza, Makatibu Wakuu wa Wizara wawekewe utaratibu maalum si wa muda mrefu. Pili, Sheria ya Fedha za maendeleo ya vijiji ziwe hadharani, wananchi waambiwe kuepuka uchakachuzi. Tatu, kuweka Sheria kwenye miradi yote kuwa wazi kuepuka uchakachuzi wa fedha na uwepo usimamizi wa Serikali na kijiji wakati Mkandarasi anapofanya kazi husika kama vile Wakandarasi na Wataalam wanavyoshirikiana kujenga barabara za lami, kila mtu kwa nafasi yake huwa makini wanapoangalia uchanganyaji wa ratio. |
|||||