| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 2 | 6 | 15 February 2011 | Kujadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete | ||
Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hatuba nzuri yenye matumaini makubwa kwa Watanzania. Mheshimiwa Spika, nalipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri inayofanya hapa nchini hasa kupamaba na majambazi. Pongezi za kipekee ziwandee maaskari Polisi wa Wilaya ya Karagwe wakiongozwa na OCD Kiruwaga. Kazi waifanyayo ni ngumu sana hasa kwa kuzingatia kuwa Wilaya ya Karagwe na Mkoa wa Kagera na Kigoma iko mpakani mwa nchi za Rwanda, Burundi na Uganda. Mara nyingi majambazi kutoka nchi hizi wamekuwa wakizishambulia sehemu za Karagwe na Mkoa mzima wa Kagera na Kigoma na kwa kuwa jeshi letu la Polisi halina vitendea kazi vya kutosha ikiwemo magari, pikipiki, fedha, mafuta na hata askari wa kutosha. Ningependa kuiomba iutangaze Mkoa wa Kagera na Kigoma kama Mkoa Maalum wa Kiulinzi kama ilivyo kwa Wilaya ya Tarime, Kinondoni, Temeke na Ilala. Mheshimiwa Spika, kuhusu mifugo na kilimo, naomba Serikali ianzishe haraka iwezekanavyo utaratibu wa kununua mazao ya nafaka kwa vipimo vya kilogramu na siyo kwa debe, gunia au kwa kukadiria. Sambamba na hilo, nashauri Serikali ilete utaratibu wa kununua mifugo minadani kwa kuwapima kwenye mzani badala ya kumkadiria mnyama. Benki ya Kilimo itakayoanzishwa iwe na matawi yake katika kila Wilaya hapa nchini ili kuwarahisishia wananchi wa vijijini kupata mikopo hiyo bila kusafiri kwenda Dar es Salaam kupata mikopo hiyo. Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa madawa ya mifugo hasa madawa ya kuua kupe na inzi. Lakini kwa masikitiko makubwa dawa hizi za ruzuku haziwafikii wafugaji wa vijijini ambapo ndio walengwa, badala yake dawa hizi zimeishia mikononi mwa wajanja wachache. Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha dawa hizi zinawafikia wafugaji wa vijijini na mijini pia. Mheshimiwa Spika, kuhusu huduma ya maji Wilaya Karagwe, ni tatizo kubwa sana. Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe ikiwemo miji ya Kayanga na Omurushaka haina maji na kama yapo ni kidogo sana labda asilimia thelathini tu. Ni kwanini Serikali haipeleki huduma ya maji kwa wananchi hawa? Serikali imekuwa ikilitangazia Bunge hili kuwa mradi wa maji wa Benki ya Dunia katika vijiji mbalimbali Wilayani Karagwe ungeanza. Hadi sasa huduma hiyo haijaanza na wananchi wamechoka kusubiri. Ni vizuri tujue mradi huu umekwama wapi na je ni juhudi zipi zinafanywa na Serikali kuleta maji katika vijiji hivi? Mkoa wa Kagera unapakana na Ziwa Victoria, pia una mto Kagera na maziwa madogo madogo yakiwemo ya songambele na kadhalika. Kwa masikitiko makubwa, Wilaya ya Karagwe haina maji ya kutosha kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya binadamu, pamoja na mifugo. Mheshimiwa Spika, Hifadhi ya Wanyamapori ya Kimisi na Burigi imekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Kata za Nyakasimbi, Ihembe, Kihanga, Nyakakika, Rugu na Rugera kwa wanyama wakali tembo na simba kushambulia wananchi na mali zao. Idara ya Hifadhi ya Wanyamapori imeshindwa kabisa kuwadhibiti wanyama hao. Naomba na kushauri Serikali kuwa National Parks kwa kuzifanya National Parks ulinzi utakuwepo kwa kuwadhibiti wanyama wakali. Naunga mkono hoja. |
|||||