You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Maige, Ezekiel Magolyo[CCM]

Msalala Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 2 6 April 2011 Hoja za Kamati
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII:

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na mimi nianze kuwashukuru na kuwapongeza sana Kamati zote tatu kwa kazi nzuri ambayo wameifanya na kipekee sana nipongeze Kamati ya POAC kwa kutusaidia sana kuimarisha usimamizi katika Mashirika ya Umma. Kwa hiyo, kwa msingi huo naomba niseme kwamba pendekezo la Kamati namba 4.1.7 nakubaliana nalo kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama kusema mawili, kwanza pamoja na kukubaliana na pendekezo hilo lakini ninapenda Bunge lako tukufu lielewe mazingira ya maamuzi yaliyofanyika wakati ule hasa kujaribu ku-clear hisia ambazo zimekwishaanza kujengeka kwenye umma kwamba maamuzi yale yalikuwa hayazingatii maslahi ya umma.

Mwaka 2007 tulikuwa tumeanza kuingiza kwenye mtikisiko wa uchumi duniani, utalii wetu wa Tanzania zaidi ya 90% ni wildlife based yaani unategemea wanyamapori na hao wanyamapori wako kwenye hifadhi na zaidi ya 95% ya huduma zote zinatolewa na sekta binafsi katika mazingira ya ushindani.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mazingira hayo tulikuwa tumefanya utafiti na kulikuwa na indications kwamba chochote ambacho kingefanyika cha kuweza kuongeza bei kingeweza kuathiri sekta nzima ya utalii kwa maana tunaendesha utalii ambao tunaita low volume high yield tourism, na kwa kufanya hivyo maana yake ni kwamba kuna hatari ya kitu kinachoitwa price increase ukiongeza gharama kwa wawekezaji. Lengo lililokuwepo lilikuwa ni kuokoa sekta ya utalii na niseme kwamba zoezi hilo lilifanyika kwa mafanikio makubwa sana. low volume height yield tourism

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005 wakati tunakwenda kwenye uchaguzi tulitegemea tungepata watalii milioni moja na tungepata fedha dola za Kimarekani bilioni 1.4, tusingefanya chochote kwenye financial crisis iliyokuwepo tulitegemea watalii wangepungua kwa 30% lakini kwa jitihada zilizofanyika ikiwemo kupunguza cost increases kwenye maeneo mbalimbali watalii walipungua kwa asilimia chache na tukapata watalii 896,000 na fedha tulizopata tulipata jumla ya dola bilioni 1.2.

Mheshimiwa Naibu Spika, tusingefanya hivyo revenue ambayo ingepatikana kwenye utalii ilikuwa inakisiwa kupunguza kutoka dola bilioni 1.4 ingefikia dola za Kimarekani milioni 980. Kwa hiyo, kwa kuzuia kuongeza gharama kwa kipindi hicho ya shilingi bilioni 21 za Kitanzania, utalii wetu uliweza kunufaika kwa kuwa resilient kwenye pressure ya mtikisiko wa uchumi na kuweza kuongeza revenue dola za Kimarekani milioni 420 na wakati huo wageni badala ya kupungua hadi kufikia 700,000 kutoka projection ya milioni moja, wageni mpaka tunafika mwaka 2010 tulikuwa na wageni 896,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niliombe Bunge lako tukufu lielewe kwamba mazingira yaliyokuwepo yalilenga zaidi kuokoa sekta ya utalii na Waziri mwenye dhamana ya sekta ya utalii alitumia Mamlaka yake kuhakikisha kwamba athari hizo ambazo zingeweza kujitokeza hazijitokezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hali hiyo kuwa imepita na ndiyo maana nakubaliana kimsingi na mapendekezo ya Kamati, mwaka 2010 tarehe 20 Desemba nilipokutana na Bodi ya TANAPA kwa mara ya kwanza moja ya vitu vya kwanza kabisa binafsi nilivyoanza kuzungumza nao ni kuwaambia kwamba sasa mtikisiko wa uchumi haupo tena kwa hiyo naomba muanze kufanya revision na kutekeleza mapendekezo yenu ambayo mliyaleta Wizarani mwaka 2007.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadaye Kamati ya Bunge na yenyewe ikawa imependekeza kitu kile kile. Naomba tu kwamba katika kuyafanya haya Waheshimiwa Wabunge muwe na imani na sisi na muelewe kwamba tunafanya kwa nia njema na kwa kutumia utafiti mahususi. Naomba nishukuru sana.