You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Arfi, Said Amour[CHADEMA]

Mpanda Mjini Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 19 5 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora), na Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) kwa mwaka wa Fedha 2011/2012
Mheshimiwa Spika, kumekuwepo malalamiko toka kwa
wananchi juu ya ajira na hususan taratibu iliyoanzishwa ya kuwa na Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma, kwa matarajio ingeweza kuleta ufanisi na kupunguza kero,
matokeo yake yamekuwa tofauti na kuwa kero badala ya ufanisi na faraja.

Mheshimiwa Spika, hofu yangu hayakufanyika maandalizi ya kutosha na
kuiwezesha Sekretarieti hiyo kwa rasilimali fedha na watu kwa kuzingatia ukubwa wa
nchi hii na mahitaji yake ya ajira pia uamuzi huo unakinzana na mpango wa kugatua
madaraka na kuipunguzia mzigo Serikali Kuu ya maamuzi na kuwepo kwa Sekretarieti
ya Ajira ni kinyume chake.

Mheshimiwa Spika, ili kupunguza kero na malalamiko ipo haja Wizara kuangalia
upya uwepo wa Sekretarieti hii na kama ni lazima basi wawezeshwe vya kutosha kukabili
changamoto zilizopo na kupunguza malalamiko mengi.