You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Zitto, Kabwe Zuberi[CHADEMA]

Kigoma Kaskazini Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 4 11 April 2011 Muswada wa Sheria ya Famasi wa Mwaka 2010 (The Pharmacy Bill, 2010)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Muswada huu. Kwanza nafahamu wewe na Spika aliyepita ni miongoni mwa Wajumbe kutoka Chama cha Mapinduzi ambao mmepitishwa kugombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama chenu. Nilikuwa naomba watu wote wa CCM ambao tunaheshimiana wawape kura ili muweze kuingia kwenye kikao muhimu hicho cha chama chenu.

Lakini pili, nimpongeze sana Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa kusoma maoni ya Kambi kwa ufasaha kabisa. Naamini kabisa kwamba tunao Mawaziri Vivuli ambao wataweza kuisimamia Serikali ya CCM vizuri kabisa na kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

Tatu, niwapongeze Serikali kwa kuja na huu Muswada, nafahamu kwamba ni Muswada ambao umechelewa muda mrefu sana, ilikuwa tuupitishe toka Bunge la Tisa, haikuwezekana na sasa umefanikiwa kupita kwenye hatua za Kamati na kuja kwenye Bunge hili la Kumi.

Lakini vile vile katika kazi yetu kama Bunge, kazi ya kutunga Sheria, Muswada huu umeingia kwenye rekodi kuwa ndio Muswada wa kwanza wa Bunge la Kumi kuweza kujadiliwa kwenye Bunge. Kwa hiyo, nilikuwa naomba hiyo rekodi iweze kuonekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina tatizo moja kubwa sana katika huu Muswada. Kwanza unapopata Muswada unaangalia madhumuni na sababu, Waziri Kivuli ameeleza hili vizuri sana. Ukisoma ukurasa wa 34 wa Muswada Objects and Reasons, the proposed law is intended to regulate the pharmacy profession in different levels. Ukienda kusoma kwa Kiswahili pamoja na kuongezeka kwa maneno na kuwa mapana zaidi, lakini pia bado ni kusimamia taaluma na maadili ya wafamasia katika utoaji wa huduma zinazohusu taaluma hiyo.

Sasa tunafahamu kwamba kuna market entry regulations, ni usimamizi unaohusiana na kuingia kwenye soko, ndio usimamizi wa profession. Lakini kuna market conduct regulation ambao ni usimamizi wa biashara. Sasa market conduct regulation imekuwa ikifanya TFDA siku zote za nyuma. Muswada huu unataka kuunganisha kwa pamoja kwamba Baraza la Wafamasia lishughulikie market entry regulation iwe regulator kwa wafamasia wanaoingia kwenye ufamasia wakishatoka kwenye vyuo kuwasimamia taaluma yao.

Wakati huo huo, wasimamie Market Conduct Regulation. Baraza hilo hilo sidhani kama principle inakwenda vizuri hapa. Nadhani ni vizuri, na tuna mifano. Nyuma huko na Waziri Kivuli amezungumza contractor Legislation Board, Engineers Legislation Boards, Nurses and Midwives Regulation Act ya mwaka 1997 zote zimetofautisha. Nadhani ni vizuri Mamlaka ya Council ya Wafamasia ikabakia kwenye kusimamia taaluma ya ufamasia. Isiingie kwenye kusimamia biashara ya ufamasia. Hii itasaidia sana nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa taarifa ni kwamba sasa hivi Tanzania tuna Wafamasia 700 tu kila mfamasia mmoja anahudumia wananchi 50,000 wenzetu kwa nchi za kiafrika kama Ghana mfamasia mmoja anahudumia watu 10,000, wenzetu Kenya wako juu kidogo wao wana wafamasia wengi kidogo, lakini hatupishani sana ndani ya eneo la Afrika ya Mashariki.

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo kubwa la wale ma-technician wa ufamasia tunao 300 tu. Bahati mbaya sana katikati ya miaka ya 1990 Taifa letu haliwafundishi tena pharmacist technicians hatuna. Hizi ni taarifa za Serikali, Taarifa ya Wizara ya Fedha. Wizara ya Fedha ilifanya tathmini ambao ilikuwa funded na WHO na European Union mwaka jana Septemba, walitoa hiyo taarifa na kuonyesha tatizo kubwa tulilonalo katika taaluma hii ya ufamasia. Kwa maana hiyo, ni kwamba tuna haja zaidi ya kuimarisha taaluma kuliko kwenda kusimamia biashara. Kwa hiyo, Muswada huu ungebakia kusimamia taaluma ya ufamasia na kuimarisha na kuweza kutatua tatizo kubwa sana la human resources katika taaluma hii ya ufamasia. Kwa hiyo, hili ndilo ambalo nilikuwa naomba liweze kuangaliwa. Muswada ubakie na madhumuni ya ku-regulate taaluma usiende kwenye ku-regulate biashara.

Lakini hata kama Bunge likikubali kwamba tukapisha Muswada kama jinsi ambavyo Serikali imeuleta kwa ajili ku-regulate pamoja na biashara ya ufamasia, bado tutakuwa tuna tatizo kwa sababu ukiangalia Muswada ule, Sheria ya Madawa ya Kenya ambayo inaanzisha Bodi ya Madawa na Sumu ya Kenya ambapo kwa kiasi kikubwa sheria yetu imeiga kutoka huko, wao hiyo regulation pamoja na kwamba wamechanganya kila kitu wameanzia kwenye utengenezaji kwa maana ya manufacturing wakaenda kwenye ufamasia na wakaenda kwenye trading ya madawa.

Kwa hiyo, wamechukua yote kwa comprehensive. Sisi tume - shell- pick kwamba utengenezaji, basi tuwaachie TFDA lakini biashara wachukue Baraza. Nadhani hapa kuna tatizo. Ni ama unachukua sekta nzima kuanzia utengenezaji licensing mpaka biashara au unafanya kazi ya taaluma tu ya ufamasia na kuiachia biashara ifanywe na TFDA. Tayari tumeshajenga uwezo wa TFDA imeshapata uwezo wa muda mrefu na uzoefu kutoka mwaka 2003 hakuna sababu sasa hivi kuanzia kuichukua na kuipunguza na kuipeleka kwenye kitu kipya ambacho kinaanza na itakuwa ni risk, yaani actually tunafanya kitu opportunistic venture sasa hivi. Kwa hiyo, maelezo ya Waziri amesema kwamba tutafanya marekebisho baadaye.

Waheshimiwa Wabunge, hakuna sababu ya kwenda kufanya marekebisho baadaye. Kifungu chote cha nne cha Muswada kiondolewe ambacho kinahusiana na biashara ya ufamasia, Muswada ubakie na kusimamia taaluma ya ufamasia. Hivyo ndivyo ambavyo tutaweza kulitendea wema Taifa letu. Vinginevyo tutaingia kwenye matatizo makubwa sana. Tutakwenda kuanzisha kitu kipya bila sababu yoyote ya msingi.

Unapotunga sheria, kuna jambo ambalo unataka kulijibu ambalo labda Serikali haijatueleza, labda itufahamishe ili Bunge liweze kufahamu. Kwa sababu unaitunga sheria ili kurekebisha kasoro ambazo zipo hivi sasa. Sasa Serikali ituambie, Wizara ya Afya kuna kasoro zipi ambazo mmeziona kwa TFDA kusimamia biashara ya madawa, tukielezwa hili na likawa kwa ufafanuzi mzuri na Wabunge wakaelewa, basi ndio hapo tunaweza tukaruhusu Muswada huu uweze kwenda. Lakini vinginevyo, kwa namna ambavyo Muswada huu ulivyo sidhani kama tutakuwa tunatendea haki Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna matatizo makubwa sana kwenye taaluma hii yarekebishwe, tunaambiwa na Taarifa za Serikali, taarifa ya Wizara ya Fedha kwamba asilimia 51 ya vijana wanaohitimu kwenye ufamasia wanaacha taaluma ya ufamasia wanakwenda benki, wanakwenda wapi asilimia 51.

Sasa ni vyema Baraza likahakikisha kwamba wana-retain kwanza tuongeze watu, lijenge uwezo hapo baadaye kama itakuja kuonekana kuna haja ya baadhi ya shughuli ama ni retail au wholesale au hata manufacturing kama zitahitajika ziingie kwenye Baraza tuwe tumeshafanya tathimini ya kutosha, lakini tumepata wafamasia wa kutosha. Yaani kwa mazingira ya sasa, naungana kabisa na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwamba ama kipengele Na. 4 yaani kifungu cha Nne cha Muswada chote kiondolewa au Muswada urudi kwenye Kamati ukafanyiwe kazi upya, kusema kwamba haiwezekani tutakuja kufanya marekebisho baadaye hapa kwa Muswada huu unaondoa kazi yote ya TFDA katika kusimamia biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 31 wa Muswada, ukurasa wa 32 wa Muswada kifungu 24, 26, 27, 47, 48 na 74 vifungu hivi vyote ndio ambavyo vilikuwa vinaipa TFDA ile mamlaka ya kufanya kazi ya kuweza kusimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa nadhani Serikali iangalie upya suala hili, ama ilete schedule of amendment, section (4) yote ya Muswada iondolewe kabisa katika Muswada na wafanye consequential amendment zote za maeneo ya Muswada tubakie na taaluma au Muswada urudi kwenye Kamati ukafanyiwe kazi upya uletwe hapa kwa ajili ya kushughulikia taaluma kama jinsi ambavyo madhumuni na sababu za Muswada zilivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ahsante.