You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Telele, Kaika Saning'o[CCM]

Ngorongoro Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 2 6 April 2011 Hoja za Kamati
Mheshimiwa Naibu Spika, lipo tatizo la Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya kukaimu kwa muda mrefu hivyo kushindwa kufanya maamuzi makubwa na magumu. Wakati mwingine watumishi wa Halmashauri za Wilaya kushindwa kuelewa ni kwa nini Kaimu huyo hathibitishwi wakati ni mchapakazi na mwadilifu. Mfano mzuri ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Engineer Maziku. Naomba athibitishwe kwani Ngorongoro ni Wilaya ya pembezoni na yenye mazingira magumu.

Pili, fedha nyingi za Halmshauri zinaliwa na Wakandarasi kupitia tender mbalimbali zenye mgao kwa wakuu wa Halmashauri wa Wilaya waliotoa kandarasi hiyo kama DED na kadhalika.