You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Jecha, Asha Mshimba[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 4 14 June 2011 Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2011/2012 – 2015/2016
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. Dhana ya Mpango ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kufungua fursa za ukuaji wa uchumi wa Taifa ili Mpango uweze kufanikiwa haraka, lazima uwazi na uwajibikaji kuanzia ngazi ya chini mpaka juu tuwe tunazungumza na kutetea jambo moja. Mfano, katika kilimo, kila mwenye uwezo wa kulima lazima alime, ashibe na ndio asafirishe au auze na sekta nyingine vivyo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nchi hii ni ya kidemokrasia, hivyo kila mtu ni lazima aheshimu na kutii sheria mbalimbali zilizopo. Uhuru usio na mpaka ni fujo na hauendi sanjali na dhana ya mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni kuhusu fursa katika kutumia masoko mbalimbali. Juhudi za makusudi zichukuliwe kuelimisha wananchi kuweza kuyatumia masoko ndani na nje ya nchi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa elimu uliopo uweze kumwandaa kijana kukabiliana na mazingira magumu ya kuweza kujitegemea.


Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukuaji wa uchumi, ni kweli uchumi wetu unakua na kipato cha Mtanzania mmoja mmoja kinaongezeka, kuna kundi kubwa la vijana ambao ndio nguvu kazi hawataki kujituma na kuzalisha, badala yake wanakimbilia mijini na kuzurura, sheria ya kuwashughulikia wazembe na wazururaji ifanye kazi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iwe na dhamira ya dhati ya kuwawezesha wananchi wake kumiliki rasilimali ili iwawezeshe wananchi nao kushiriki katika ubia wa miradi mbalimbali. Naunga mkono hoja.