You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Umbulla, Martha Jachi Sulle[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 2 6 April 2011 Hoja za Kamati
Mheshimiwa Naibu Spika, ninawapongeza Wenyeviti wa Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupanga matumizi kulingana na vipaumbele ni jambo moja, lakini kutumia vizuri kile kilichoidhinishwa na Bunge ni jambo la pili.

Tatizo kubwa ni nidhamu na uadilifu wa matumizi, juhudi kubwa ielekezwe kwenye kujenga nidhamu na uadiilfu wa matumizi ya fedha za Serikali.

Wadau na wamiliki wakubwa wa taarifa hizi zote tatu ni Watanzania. Taarifa au Ripoti zetu ziwe na tija kwa Watanzania ndipo tutaonekana tumewajibika ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tupate mafanikio makubwa ni lazima tuondokane na dhana ya itikadi katika masuala yanayogusa maslahi ya Taifa letu.

Katika ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu ya 2009, idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kuwa maskini ni milioni 14, kati ya milioni 40+. Kati ya hao; 14 milioni, 12.5, sawa na asilimia around 84 wanaishi vijijini.

Sasa naomba kuuliza; hivi tunapopanga matumizi ya fedha za Serikali katika Halmashauri ni kwa asilimia ngapi zinawalenga hawa 84%?

Mheshimiwa Naibu Spika, tunao Wenyeviti wa Vijiji na wa Vitongoji, Watendaji wa Vijiji na Waheshimiwa Madiwani; hawa ndiyo wanaosimamia utekelezaji wa Miradi yote ya Maendeleo na Programu zote zinazobuniwa na Serikali na kadhalika; lakini Viongozi hawa hawafikiriwi hata kidogo kujengewa uwezo ili wafanye kazi vizuri. Viongozi hawa wapewe motisha walau mishahara ya kima cha chini ya Serikali.

Naishauri Serikali iwe sambamba na udhibiti wa fedha na uratibu wa Miradi ya Maendeleo. Tubuni mpango mahususi wa kuwajengea uwezo Viongozi hawa ili waweze kusimamia vizuri rasilimali nyingi zinazoelekezwa ngazi ya Halmashauri kutoka Serikali Kuu. Mara chache sana wanakwenda kwenye semina, warsha na mafunzo mbalimbali, tofauti na Viongozi wa Juu wanaoenda kila mara.

Mheshimiwa Naibu Spika, haifai watu wanaosimamia fedha nyingi na miradi mingi, maisha yao yakaendelea kuwa duni. Uratibu au udhibiti hauna tija kama wazalishaji hawana tija.