You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Maghembe, Prof. Jumanne Abdallah[CCM]

Mwanga Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
20 28 12 July 2010 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 - Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu; baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2010/11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napenda kumpongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi sana kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia nimpongeze sana Mheshimiwa Dr. Mohamed Ghalib Bilal kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi. Naomba pia nimpongeze kwa dhati Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Ali Mohamed Shein, kwa kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uchaguzi wa Oktoba, 2010 CCM imewaletea Watanzania viongozi hodari na wachapakazi wa hali ya juu watakaoivusha Tanzania kutoka nchi inayoendelea kuelekea Taifa la uchumi wa kati. Naungana na Wabunge na Watanzania wote kuwatakia viongozi wetu ushindi wa kishindo mwezi Oktoba, 2010.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo, napenda kuungana na wenzangu kuzipa pole familia za marehemu Mheshimiwa Rashidi Mfaume Kawawa, Waziri Mkuu wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Muasisi wa CCM na Mheshimiwa Sigifrid Seleman Ng’itu, Mbunge wa Ruangwa waliotangulia mbele ya haki katika mwaka wa fedha wa 2009/10. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani zangu za dhati kwa Naibu Mawaziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Gaudentia Mugosi Kabaka na Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza, Wabunge wa Viti Maalum kwa ushirikiano, uaminifu na uchapakazi walionionesha katika Wizara hii. Aidha, napenda kumshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamisi Omari Dihenga, Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Muhochi Gesimba, pamoja na Kamishna wa Elimu Mwalimu Aminiel Stephano Mrutu, Wakurugenzi wa Idara, Viongozi wa Vyuo Vikuu, Mashirika na Mabaraza Chini ya Wizara, Viongozi katika ngazi mbalimbali, Maprofesa, Walimu, Wahadhiri na Wafanyakazi wote kwa ushirikiano walionipa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara na katika maandalizi ya bajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kutoa shukrani na pongezi kwa Mwenyekiti Profesa Mayunga Nkunya na Wajumbe wa Baraza la Ushauri la Elimu la Taifa kwa ushauri wao mzuri. Aidha, napenda kuwashukuru Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Wanataaluma kwa ushirikiano wao.


Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia niwashukuru sana wananchi wa Jimbo langu la Mwanga kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2005. Ripoti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya yetu inaonyesha utekelezaji wa hali ya juu uliofikia takriban asilimia 95. Hivyo, nawaomba wana-CCM na wananchi wa Mwanga waendelee kuniunga mkono katika kura za maoni zilizo mbele yetu ili tuendelee kuiletea Wilaya yetu maendeleo ya Kimbunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu mpenzi Kudra Maghembe na watoto wangu Ngwalu Maghembe, Dr. Mwanamkuu Maghembe na Mcheja na Namvuma Maghembe kwa upendo, misaada ya kila aina na uvumilivu wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha na Uchumi kwa hotuba zao nzuri ambazo kwa pamoja zilitoa tathmini na mwelekeo wa Bajeti ya Serikali na hali ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Aidha, hotuba hizo zimeeleza utendaji wa kazi za Serikali na mwelekeo kwa mwaka 2010/2011. Kwa hali hiyo, hotuba yangu itatoa ufafanuzi wa Makadirio na Matumizi yanayohusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Omar S. Kwaangw’ kwa kufanya kazi ya uchambuzi wa kina na kwa ushauri wao katika kuimarisha utekelezaji wa bajeti hii na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza katika hotuba yangu ya Bajeti ya mwaka uliopita, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekabidhiwa majukumu yanayohusu, Elimu ya Awali na Msingi; Elimu ya Sekondari; Mafunzo ya Ualimu; Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Elimu ya Juu, Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Taasisi na Mabaraza yaliyo chini ya Wizara yanayosimamia ubora wa elimu na mafunzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2009/2010 na matarajio ya Mwaka 2010/2011. Naomba nianze kwa kutoa tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2009/10 na baadaye nitatoa mwelekeo wa Mapato na Matumizi kwa mwaka 2010/2011.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipanga kukusanya maduhuli ya Serikali Shilingi 4,510,784,000. Hadi tarehe 30 Juni, 2010; Shilingi 6,325,283,914 zilikuwa zimekusanywa. Lengo lilivukwa kutokana na baadhi ya shule za sekondari ambazo zimegatuliwa kuendelea kuwasilisha maduhuli yao katika hesabu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hadi mwezi Oktoba 2009. Kuanzia mwezi Novemba, 2009 maduhuli hayo yanawasilishwa kwenye Halmashauri husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2009/2010 bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilikuwa Shilingi 428,436,913,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya hizo, Shilingi 41,039,652,700 zilikuwa za Mishahara na Shilingi 387,397,260,300 zilikuwa za Matumizi Mengineyo. Hadi tarehe 30 Juni, 2010, matumizi ya kawaida yalikuwa Shilingi 421,204,126,333, ambapo Shilingi 40,536,159,244 zilikuwa za mishahara na Shilingi 380,667,967,089 zilikuwa za matumizi mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bajeti ya Maendeleo kwa mwaka 2009/10 ilikuwa Shilingi 129,283,697,000. Kati ya hizo, fedha za ndani zilikuwa Shilingi 65,366,471,999 na za nje zilikuwa Shilingi 63,917,225,001. Hadi kufikia Juni, 2010 ni asilimia 62 ya fedha hizo zilipokelewa, yaani shilingi bilioni 79.6. Hadi tarehe 30 Juni, 2010, matumizi yalikuwa Shilingi 80,453,399,723.05 ambapo Shilingi 50,207,557,2344 zilikuwa fedha za ndani na Shilingi 30,245,842,489 zilikuwa fedha za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya ya jumla ya mapato na matumizi niliyoyatoa, ifuatayo ni taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara na malengo kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Kamishna wa Elimu ina majukumu ya kuratibu utoaji wa elimu katika ngazi za Awali; Msingi; Sekondari; Mafunzo ya Ualimu; Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi; pamoja na Udhibiti wa ubora wa Elimu, Ukuzaji Mitaala, Uendeshaji Mitihani, Huduma za Maktaba na Mafunzo ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu. Ofisi ya Kamishna wa Elimu inajumuisha vitengo vya Elimu Maalum, Elimu kwa Mawasiliano, Usajili wa Shule, Ithibati ya Vifaa vya Elimu na Masuala Mtambuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Ofisi ya Kamishna wa Elimu:-

(a) Ilitoa Mafunzo ya Elimu Jumuishi, Stadi za Braille na lugha ya alama (Sign Language) kwa wakufunzi 57 wa vyuo vya Ualimu Kasulu na Kabanga;

(b) Ilichambua maombi 354 ya hatua mbalimbali za usajili, ambapo 112 yalikubaliwa na kupewa vibali vya kuendelea na ujenzi na 198 yalithibitishiwa wamiliki na mameneja wa shule. Aidha, maombi 44 yalirudishwa kwa wadau kwa ajili ya marekebisho;
(c) Iliandaa na kutangaza vipindi 580 vya Redio, ambapo vipindi 52 vilikuwa vya ufundishaji kwa kutumia mbinu shirikishi na 528 vilikuwa vya masomo ya redio kwa Shule za Msingi.

(d) Ilipokea maombi 229 ya kusajili shule ambapo shule 112 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi na shule 117 (Awali tatu, Awali na Msingi 46, Sekondari 57 na Vyuo vya Ualimu 11) zisizo za Serikali ziliidhinishwa na kusajiliwa;

(e) Ilitoa leseni za kufundisha kwa walimu 293;

(f) Ilikamilisha uandaaji wa ‘Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Masuala ya Kielimu kwa Kuzingatia Usawa wa Kijinsia;

(g) Ilifuatilia utoaji wa Elimu Maalum na Elimu Jumuishi na uanzishwaji wa shule au vitengo vya Elimu Maalum na Elimu Jumuishi katika Halmashauri 16;

(h) Ilisambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule 272 za msingi, 29 za Sekondari na Vyuo vya Ualimu sita;

(i) Iliteua vitabu viwili vya kiada kwa kila somo la Elimu ya Awali na msingi kwa ajili ya darasa la 1 – 5;

(j) Ilitoa Waraka Na. 2 wa Mwaka 2010 kuhusu vitabu vya kiada shuleni na kutoa mwongozo wa usambazaji wa vitabu teule;

(k) Ilitoa ithibati kwa vitabu 34 vya kiada kwa shule za Msingi. Aidha, ilitoa ithibati kwa vitabu vya sekondari vya masomo ya Hisabati, Fizikia, Kemia na Biolojia kwa kidato cha I na cha II , kupitia Programu ya msaada wa watu wa Marekani (USAID);

(l) Ilipitia Miswada ya vitabu 105 vya elimu ambapo Miswada 34 ilipewa ithibati na 41 ilikataliwa;

(m) Ilipitia upya nyaraka 128 zilizoandaliwa kati ya mwaka 1997 na 2009 na kuzihuisha; na


(n) Iliandika Sura 2 kati ya 8 za rasimu ya taarifa ya matokeo ya utafiti ngazi ya taifa kuhusu ubora wa elimu katika nchi 15 za Kusini na Mashariki ya Afrika (SACMEQ Project III).
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Wizara yangu iliendelea kutekeleza awamu ya pili ya MMEM (2007-2011) ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la kutoa Elimu ya Awali na Msingi kwa wote linafikiwa. Idara ya Elimu ya Msingi:-

(a) Ilitoa huduma jumuishi za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto, Wizara yangu ilishiriki katika kuandaa Sera Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Mtoto;

(b) Iliimarisha utoaji wa Elimu ya Awali Wizara, kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mtandao wa Malezi, makuzi na Maendeleo ya Mtoto na UNICEF iliratibu uandaaji wa: Mwongozo na Viwango vya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto; Mwongozo wa Wawezeshaji wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto; Mwongozo wa Vifaa vya Kufundishia na vifaa vya michezo kwa watoto wadogo;

(c) Ilitimiza azma ya Serikali ya kuwa na darasa la awali katika kila shule, Wizara iliratibu uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali wa shule za Serikali na zisizo za Serikali ambapo idadi ya wanafunzi wa Awali iliongezeka kutoka 638,591 mwaka 2005 (wasichana 319,974) na kufikia 925,465 (wasichana 463,837) mwaka 2010. Kati ya hao, 1,771 ni wanafunzi wenye mahitaji maalum. Aidha, idadi ya mikondo ya Elimu ya Awali iliongezeka kutoka 21,607 mwaka 2005 hadi 34,861 mwaka 2010. Walimu wa Elimu ya Awali waliongezeka kutoka 11,148 (wanawake 6,510) mwaka 2005 hadi 16,534 (wanawake 8,884) mwaka 2010;

(d) Idadi ya wanafunzi wa elimu ya msingi iliongezeka kutoka 7,541,208 (wasichana 3,685,496, wavulana 3,855,712) mwaka 2005 hadi 8,419,305 (wasichana 4,216,036) mwaka 2010 wakiwemo wanafunzi 36,585 wenye mahitaji maalumu. Walimu wa Elimu ya Msingi waliongezeka kutoka 135,013 (wanawake 64,707) mwaka 2005 hadi 165,856 (wanawake 83,686) mwaka 2010. Aidha, Shule za Msingi ziliongezeka kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010. Uwiano wa Mwanafunzi kwa mwalimu uliimarika kutoka 1:56 (mwalimu mmoja kwa wanafunzi 56 ) na kufikia 1:51 (mwalimu mmoja kwa wanafunzi 51);

(e) Ilishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kuanza ujenzi wa shule ya Msingi Monduli Jeshini (Sokoine Cantonment) na kukarabati shule za mfano ikiwemo Shule ya Arusha (Arusha School).
(f) Iliandaa na kutoa machapisho ya miongozo ya ununuzi wa vifaa, ujenzi wa shule, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza, uimarishaji wa taratibu za kitaasisi, hesabu na usimamizi wa fedha, ununuzi wa vitabu vya kiada na vifaa vingine vya elimu na ufuatiliaji na tathmini kwa ajili ya utekelezaji wa MMEM II. Nakala 2,625 za miongozo hiyo zilisambazwa katika Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara;

(g) Ilifanya ufuatiliaji, tathmini, utafiti na ukaguzi wa matumizi ya fedha za MMEM kwa kushirikiana na TAMISEMI;

(h) Iliratibu utoaji wa mafunzo kazini kwa walimu 270, ili kuwajengea uwezo wa ufundishaji wa masomo ya Hisabati na Sayansi;

(i) Iligharimia utoaji wa mafunzo katika usimamizi wa elimu kwa viongozi 11, wasimamizi wa elimu 494 wakiwemo Walimu Wakuu, Waratibu Elimu Kata na Maafisa Elimu ngazi ya Halmashauri;

(j) Ilifuatilia matumizi ya ruzuku ya uendeshaji ya shilingi bilioni 80 (shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka) kwa ajili ya kuinua ubora wa elimu katika Mikoa ya Mara, Shinyanga, Mbeya, Singida, Rukwa, Dodoma, Lindi Mtwara, Kigoma, Tabora, Manyara na Pwani;

(k) Ilishirikiana na WFP katika kuongeza wigo wa ufadhili wa Mradi wa Lishe Shuleni kutoka Halmashauri 13 (Bahi, Longido, Iramba, Manyoni, Kondoa, Chamwino, Karatu, Simanjiro, Kiteto, Ngorongoro, Mpwapwa, Singida (V) na Monduli) hadi kwenda 16, ikijumuisha Halmashauri za Kishapu, Shinyanga Vijijini na Meatu). Tathmini ya Mradi huu katika shule za Wilaya 16 inaonesha kuongezeka kwa mahudhurio na kupungua kwa mdondoko;


(l) Iliandaa rasimu ya mwongozo wa ufundishaji wa somo la sayansi kwa njia ya majaribio; na


(m) Iliwajengea uwezo wa uendeshaji wa mradi wa Bridge – IT walimu 1,000 na Wakaguzi wa shule 17, wawezeshaji 17, kanda za video 417 za kufundishia masomo ya sayansi na Hisabati kwa wanafunzi wa darasa la V na VI ambapo wanafunzi 60,000 wananufaika na mradi huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Idara ya Elimu ya Sekondari. Elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu kati ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu. Idara ya Elimu ya Sekondari inasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu katika ngazi hii, kutoa elimu bora kwa usawa kuanzia kidato 1–6 na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya ubora wa elimu itolewayo. Utekelezaji wa Sera ya elimu katika ngazi hii unalenga katika kuongeza nafasi za elimu ya sekondari na kuhakikisha kuwepo idadi kubwa ya wahitimu wa Kidato cha 6 kwa ajili ya Elimu ya Juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005. Idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka 1,745 mwaka 2005 na kufikia 4,266 mwaka 2010, kwa kujenga shule 3,397 za serikali katika ngazi ya Kata na shule 869 mpya zisizokuwa za Serikali. Aidha, wanafunzi wa elimu ya sekondari kidato 1-6 wa shule za serikali na zisizo za Serikali waliongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 (wasichana 244,571) hadi 1,638,699 mwaka 2010 (wasichana 728,528). Wanafunzi waliojiunga na kidato 1 waliongezeka kutoka 180,239 mwaka 2005 (wasichana 88,559,) na kufikia 438,827 mwaka 2010 (wasichana 198,810). Wanafunzi waliojiunga na Kidato cha tano waliongezeka kutoka 18,893 mwaka 2005 (wasichana 7,147) na kufikia 38,334 mwaka 2010 (wasichana 15,278). Walimu wa shule za sekondari waliongezeka kutoka 23,905 mwaka 2005 kufikia 40,517 (wanawake 12,696) mwaka 2010.


Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji na tathmini ya elimu ya sekondari ulifanyika na mafanikio kadhaa yalijitokeza. Katika kipindi cha mwaka 2005 na 2009, matokeo ya upimaji huo yalijidhihirisha katika ongezeko la kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne na sita. Kati ya wanafunzi 85,292 wa Kidato cha nne waliofanya mitihani mwaka 2005, wanafunzi 27,298 walifaulu na kupata daraja la IIII. Kati ya hao, wanafunzi 6,322 (23.2%) walitoka shule kongwe za Serikali, 7,933 (29.2%) walitoka 11 shule za sekondari za wananchi za kutwa na 12,953 (47.6%) walitoka shule zisizo za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009, jumla ya wanafunzi 239,434 walifanya mitihani ya Kidato cha nne. Kati ya hao, wanafunzi 41,363 walifaulu kwa kiwango cha daraja la I-III, ambapo wanafunzi 20,742 (50.15%) walitoka shule za wananchi za kutwa, 4,121 (9.96%) walitoka shule kongwe za Serikali na 16,500 (39.89%) walitoka shule zisizo za Serikali. Haya ni mafanikio makubwa sana katika utekelezaji wa mfumo wetu wa Elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu hizi zinaonesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu katika kiwango cha daraja la I-III ambao ndiyo wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano ni kutoka shule za sekondari za kutwa zilizojengwa na wananchi. Hali hii ya ufaulu imetokana na ushirikiano mkubwa kati ya serikali na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009 wanafunzi wa shule zetu za Sekondari walishiriki katika shindano la uandishi wa insha kwa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Tanzania iliibuka na ushindi wa kwanza na wa pili. Mwanafunzi aliyekuwa mshindi wa kwanza ni Allen Kamnde kutoka Shule ya Sekondari ya Seminari ya Maua na wa pili ni Mary Hingira kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machame. Aidha, shule zetu ziliibuka na kuwa na mshindi wa tatu katika shindano la insha la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwanafunzi aliyepata ushindi huu ni Peter Emil kutoka katika Shule ya Sekondari ya Tosamaganga. Pamoja na ushindi huu, mwanafunzi Happiness Watimanywa, kutoka St. Constantine Secondary School iliyoko Arusha alishika nafasi ya kwanza duniani katika mtihani wa somo la Uhasibu unaoendeshwa na University of Cambridge, International Examination Syndicate mwezi Juni 2009. Ushindi huu ni mkubwa na wa kujivunia katika mafanikio katika ngazi hii ya Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya ongezeko la ufaulu wa wanafunzi yamechangiwa na jitihada za Serikali kuendelea kutoa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika shule; kutoa mafunzo kwa walimu 3,000 wa masomo ya sayansi na hisabati pamoja na kuendesha kambi za sayansi kwa wanafunzi wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuimarisha usimamizi wa uendeshaji wa shule za Sekondari, Serikali iligatua uendeshaji wa shule hizo na kuziweka chini ya mamlaka za Halmashauri za Wilaya. Ili kufanikisha utaratibu huu, Wizara iliratibu taratibu za kupeleka usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari katika mamlaka za serikali za mitaa na kutoa Miongozo na mafunzo ya awali kwa maafisaelimu wa Elimu ya Sekondari na maafisaelimu Taaluma kwa kushirikiana na OWM - TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Ualimu ina jukumu la kutoa Elimu ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada, kuandaa na kupitia Sera, Miongozo na Viwango vya Elimu ya Ualimu na kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Walimu MMEMWA (Teacher Development and Management Strategy -TDMS).
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafunzo ya elimu ya ualimu ya daraja A na Stashahada hutolewa katika vyuo vya ualimu 34 vya Serikali na 57 visivyo vya Serikali ambavyo vyote kwa pamoja vina uwezo wa kudahili wanachuo 43,098 kwa wakati mmoja. Aidha, baadhi ya vyuo vikuu hutoa Elimu ya ualimu ngazi ya Stashahada. Vyuo vikuu hivyo ni: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), State University of Zanzibar (SUZA), Muslim University of Morogoro (MUM), Mwenge University College of Education, St. Augustine University of Tanzania (SAUT), Teofilo Kisanji University (TEKU), Sebastian Kolowa University (SEKUCO), Tumaini University na Mount Meru University, Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.Mheshimiwa Mwenyekiti, idadi ya wahitimu katika vyuo vya Ualimu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2009/10 wahitimu Daraja A walikuwa 12,305. Mwaka 2010/11, walimu 14,501 wanatarajiwa kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti. Kati ya hao, 7,939 wanatoka Vyuo vya ualimu vya Serikali na 6, 562 wanatoka katika Vyuo vya Ualimu vya watu na Mashirika binafsi. Aidha, katika mwaka 2009/10, wahitimu wa Stashahada walikuwa 5,530. Mwaka 2010/11, Wizara inatarajia walimu 7,084 kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada. Walimu 6,815 wanatoka katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na walimu 269 wanatoka katika Vyuo vya Ualimu vya binafsi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, ongezeko la wahitimu katika vyuo vya ualimu limechangiwa na jitihada za serikali na washiriki wa elimu katika kutoa Elimu ya Ualimu ambapo vyuo vya ualimu vimeongezeka kutoka 52 (33 vya Serikali) mwaka 2005 mpaka 77 (34 vya Serikali) mwaka 2010. Katika mwaka 2007, Serikali iliibadilisha Shule ya sekondari Shinyanga (Shinyanga Commercial Secondary School - SHYCOM) kuwa Chuo cha Ualimu wa Stashahada kwa masomo ya biashara na mwaka 2008, Serikali ilianzisha Chuo cha Ualimu Dakawa ili kukabiliana na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi. Aidha, katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010, walimu 12,464 wa Daraja ‘B’ na ‘C’ walipewa mafunzo na kupandisha kiwango chao kuwa Daraja ‘A’.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Idara ya Elimu ya Ualimu:-
(a) Iliwapatia mafunzo ya ualimu walimu wanafunzi 15,572 wa ngazi ya Cheti A na 12,529 wa Stashahada katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na kuratibu mafunzo ya ualimu kwa walimu wanafunzi 12,529 wa ngazi ya cheti na 913 wa ngazi ya stashahada katika vyuo binafsi;

(b) Iliwapatia mafunzo ya TEHAMA walimu wanafunzi wa stashahada 5,855 na ambao wamefanya mtihani wa Baraza mwezi Mei 2010;

(c) Iliwapatia wakufunzi 596 Mafunzo Kazini kuhusu ufundishaji kwa vitendo masomo ya Sayansi, TEHAMA na English;

(d) Iliendesha mafunzo kazini kwa wakufunzi 300 kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kufundisha na kujifunza;

(e) Iliwapatia mafunzo kabilishi (orientation) wakufunzi 528 waliopata ajira mpya vyuoni baada ya kuhitimu vyuo vikuu;

(f) Iliwapatia mafunzo ya Elimu kwa Michezo Wakufunzi 30 kutoka vyuo vya Ualimu 12 katika Chuo cha Ualimu Butimba kwa ushirikiano na Shirika lisilo la Kiserikali la Liike kutoka Finland;

(g) Ilitayarisha Vigezo vya Ubora wa Elimu ya Ualimu (Teacher Competency Framework) na kutoa mafunzo kazini kwa walimu 154 wa Shule za Msingi kwa ushirikiano na UNESCO na UNICEF;

(h) Ilitoa Mafunzo ya walimu kazini kuhusu Mbinu za ufundishaji Bainifu na Elimu ya Kinga dhidi ya VVU/UKIMWI kwa wakufunzi 154, walimu 50 wa shule za Msingi, walimu 240 wa shule za sekondari na wakaguzi wa shule wa Mkoa wa Kigoma chini ya mpango unaogharimiwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa (One UN-Joint Programme);

(i) Iligharimia mafunzo ya Walimu wa leseni 637 wanaosomea ualimu chuo Kikuu Huria cha Tanzania na watumishi wengine 385 wanaosoma vyuo vikuu ndani na nje ya nchi; na


(j) Iliratibu ukarabati na utoaji wa vifaa kwa ajili ya Maabara tatu za lugha katika Vyuo vya Ualimu vya Butimba, Morogoro na Mtwara Ufundi kwa ushirikiano na Shirika la USAID.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi. Moja ya majukumu ya Idara hii ni kuleta msukumo mpya katika juhudi za Serikali za kukabiliana na ongezeko la watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu. Jukumu la idara hii ni kutoa fursa ya kujiendeleza kielimu nje ya mfumo rasmi wa shule miongoni mwa vijana na watu wazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi:-

(a) Iliandaa muswada (script) wenye masomo 65 ya redio na televisheni, kitabu cha mwanakisomo, miongozo ya wawezeshaji na wasimamizi kwa ajili ya kufundishia Elimu ya Watu Wazima kupitia programu ya Ndiyo Ninaweza katika Halmashauri za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ilemela, Dodoma Mjini, na Songea Manispaa. Mpango mkubwa wa kupanua mafunzo ya kisomo wa Ndiyo Ninaweza nchi nzima umekamilika na utekelezaji utaanza mwezi Septemba 2010;

(b) Ilifanya ufuatiliaji na kuratibu vituo vya Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) vyenye jumla ya washiriki 987,289 na vituo vya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) vyenye washiriki 82,989 katika Halmashauri zote nchini;

(c) Ilifanya tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi na kutoa taarifa itakayowezesha kuandaliwa kwa Mpango Mkakati kwa kipindi cha 2010/2011 – 2014/2015; na

(d) Ilifanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mpango wa Mambo Elimu unaotoa elimu ya msingi kwa watoto wa jamii za wafugaji (Halmashauri za Ngorongoro, Kiteto na Loliondo) na jamii za wavuvi (Halmashauri za Lindi Mjini, Vijijini, Mtwara Mjini na Vijijini).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi: Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ina majukumu ya kubuni, kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo. Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, Serikali iliongeza nafasi na ubora wa mafunzo, ambapo Vyuo vya Ufundi Stadi viliongezeka kutoka 819 mwaka 2005 hadi kufikia 889 mwaka 2010. Katika kipindi hicho, idadi ya wanafunzi waliokuwa wakisomea mafunzo ya ufundi stadi iliongezeka kutoka 89,031 (wasichana 31,625) mwaka 2005 hadi 129,468 (wasichana 52,684) mwaka 2010. Katika kuimarisha ubora wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara iliratibu uanzishwaji wa mafunzo yanayozingatia umahiri (Competence-Based) katika vyuo vya ufundi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya mwaka 2005/2006 na 2009/2010, Vyuo vya Ufundi Stadi vya Songea, Arusha na Singida vilijengwa. Vyuo 19 vya Oljoro VTC, Mikumi; VTC; Kagera, VTC; Musoma, VTC; Dakawa, VTC; Ulyankulu, VTC; Tabora, RVTSC; Shinyanga, VTC; Mpanda, VTC; Moshi, RVTSC; Dodoma, RVTSC; Tanga, RVTSC; Iringa, RVTSC; Mbeya, RVTSC; Kihonda, RVTSC; Dar es Salaam, RVTSC; Mwanza, RVTSC; Kigoma, RVTSC na Morogoro VTTC vilikarabatiwa na kupewa vifaa, wakati Vyuo vitano (5) vya Ufundi vinaendelea kujengwa katika Mikoa ya Lindi, Manyara, Pwani, Dar es Salaam na Makete. Mfumo wa Tuzo wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Technical and Vocational Education and Training Framework) ulianzishwa na Serikali ambapo utekelezaji wake unasimamiwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Mfumo huu unaozingatia umahiri unatekelezwa katika ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni kwa wanafunzi wanaosomea cheti ngazi ya ufundi Stadi (National Vocational Awards Level 1- 3) na ngazi ya pili ni wanafunzi wanaosomea Cheti, Stashahada, Shahada, na Shahada ya Uzamili (National Technical Awards Level 4-10). Hadi sasa, utekelezaji wa mfumo huu umefikia wahitimu wanaomaliza ngazi ya Shahada (NTA 8). Mfumo huu wa mafunzo ni muhimu kwa sababu unawawezesha wahitimu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi kuendelea na mafunzo katika ngazi za juu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuchangia katika kutoa wataalamu ngazi ya kati, Vituo vinne (4) vya Mafunzo ya Ufundi na Huduma vya Mkoa (Regional Vocational Training and Services Centres) vya Dar es Salaam, Tanga, Moshi na Mtwara vimetambuliwa na Bodi ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili vianze kutoa mafunzo ngazi ya cheti hadi stashahada (NTA Level IV – VI). Katika mwaka wa fedha 2010/2011, vyuo hivi vinatakiwa kukamilisha mipango ya msingi ambayo itakidhi matakwa ya changamoto zilizopo kabla ya kuanza mafunzo rasmi katika mwaka wa fedha 2011/2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi:-
(a) Iliongeza udahili katika elimu ya ufundi na iliratibu upanuzi wa Elimu ya Ufundi ngazi ya Cheti na Stashahada kwa kuanzisha programu ya mafunzo ya Stashahada ya Sayansi ya Teknolojia ya Maabara katika Chuo cha Ufundi Arusha na kudhamini wanafunzi 505 wa mafunzo ya Stashahada;

(b) Iliwezesha kila Wilaya kuwa na kituo cha ufundi stadi kwa kufanya uchambuzi wa mahitaji ya stadi katika Wilaya 15 ambazo ni Tandahimba, Nanyumbu, Ruangwa, Liwale, Sumbawanga, Nkasi, Manyoni, Babati, Hanang, Mkuranga, Kyela, Magu, Serengeti, Rorya na Kongwa. Aidha, iliendeleza mashauriano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto juu ya kuviongezea uwezo wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 35;

(c) Ilipanua wigo wa fani za ufundi stadi idara kwa kuratibu uanzishwaji wa Mradi wa ‘Education for Employment – (EFE) chini ya udhamini wa CIDA – Canada, ukiendeshwa na Association of Canadian Community Colleges (ACCC) kwa kuhusisha vyuo vya ufundi na ufundi stadi 13 vinavyotoa mafunzo katika fani za Utalii, Kilimo na Madini; na

(d) Iliinua ubora wa mafunzo ya ufundi na ufundi stadi kwa kuhamasisha wanafunzi wa kike kujiunga na elimu na mafunzo ya ufundi. Aidha, iliratibu ushirikiano wa Italian-Tanzanian Technical Education and Labour Market Support Programme katika Chuo cha Ufundi Arusha ambapo chuo kimenufaika kwa kupatiwa Euro 200,000 za kununulia vifaa vya kufundishia, na Euro 40,000 za kusaidia kuinua ubora wa mafunzo yatolewayo pamoja na kusomesha wanafunzi wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Juu ina majukumu ya kutunga, kusimamia na kutathmini Sera, Sheria, Taratibu na Miongozo ya utoaji wa Elimu ya Juu. Elimu hii hutolewa katika Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki 11 vya Umma na 21 visivyo vya Serikali. Kazi za msingi zinazofanywa na Vyuo Vikuu ni kufundisha, kufanya utafiti unaolenga katika kuinua maisha ya wananchi na kutoa ushauri wa kitaalam kwa Serikali na umma kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti unaofanywa vyuoni una manufaa sana kwa kuvipandisha hadhi vyuo vikuu vyetu kitaaluma, kusaidia wananchi kuondokana na umaskini, pamoja na kuongeza uzalishaji viwandani na mashambani. Baadhi ya maeneo muhimu yaliyofanyiwa utafiti ni pamoja na chanjo ya UKIMWI, kubaini vijidudu vya malaria kwa haraka, kubaini usugu wa dawa za malaria kwa lengo la kudhibiti malaria nchini, uhifadhi wa ardhi na mazingira kwa ujumla, uzalishaji wa mbegu bora za mazao na kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea na wanyama na ufugaji bora wa kuku wa kienyeji na mbuzi wa maziwa.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005 Wizara yangu imefanikisha ongezeko la udahili katika Elimu ya Juu, ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 40,993 mwaka 2005/2006 hadi 118,951 mwaka 2009/2010. Jumla ya wanafunzi 10,884 walidahiliwa mwaka wa kwanza katika Taasisi za elimu ya juu zisizo kuwa Vyuo Vikuu zinazotoa shahada (8,824 Shahada ya Kwanza, 249 Uzamili na 1,811 Shahada za Uzamivu) na wanafunzi 9,947 walidahiliwa katika taasisi zinazotoa Stashahada ya Juu (Angalia Kiambatisho. Aidha, wanafunzi 130,060 wa Elimu ya Juu walipewa mikopo.


Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na Sheria ya vyuo vikuu ya mwaka 2005, kila chuo kinatakiwa kuwa na Hati Idhini. Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa mpaka sasa vyuo vikuu 17 vimeshapata Hati Idhini na vinaongozwa kwa kutumia Kanuni na Miongozo ya Hati Idhini zao. Vyuo vingine viko katika hatua mbalimbali za kukamilisha zoezi hilo.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imechukua juhudi za makusudi za kulitafutia ufumbuzi wa kudumu, tatizo la uhaba wa walimu katika shule za sekondari kwa kuongeza udahili katika Shahada za Ualimu katika Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Umma na Vyuo Vikuu binafsi. Aidha, kuanzia mwaka 2007/2008 Serikali imekuwa ikitoa mkopo kwa wanachuo wote wanaochukua Shahada za Ualimu, ili kuongeza idadi ya wanachuo wanaojiunga na mafunzo ya ualimu. Nia ya Serikali ni kuondoa kabisa tatizo la uhaba wa walimu shuleni. Ili kuvutia zaidi walimu wa sayansi, kuanzia mwaka 2009/2010 Serikali imekuwa ikiwapatia mikopo ya asilimia 100 wanafunzi wa programu za ualimu na wanaosomea masomo ya sayansi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha programu za shahada za ualimu katika vyuo vikuu ambapo, vyuo vikuu 10 visivyo vya Serikali (University College of Education Zanzibar, Tumaini University – Makumira College, Muslim University of Morogoro, Mwenge University College, St. Augustine University of Tanzania, St. John’s University, Sebastian Kolowa University College, Tumaini University – Iringa College, Teofilo Kisanji University na University of Arusha) vinaendesha programu za ualimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa vyuo vya Serikali vinavyotoa programu za ualimu, ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Chuo Kikuu Huria, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Chuo Kikuu Mzumbe. (Angalia Kiambatisho Na. 18). Kutokana na ongezeko la Idadi ya Vyuo vinavyotoa mafunzo ya ualimu, Idadi ya wahitimu wa Shahada za Ualimu imeongezeka kutoka walimu 2,760 mwaka 2005 kufikia walimu 5,331 wa mwaka 2009. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia walimu 12,120 watakaohitimu kwenye vyuo Vikuu mwaka wa 2010. Aidha, walimu wa shahada watakaohitimu mwaka kesho ni 11,849, na wale wanaotarajiwa kuhitimu mwaka 2012 watakuwa 13,411.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010 Idara ya Elimu ya Juu:-

(a) Iligharimia Wanafunzi 90 (85 raia wa Uganda na watano wa China) katika mpango wa kubadilishana wanafunzi;

(b) Iliendelea kuelimisha umma juu ya dhana ya uchangiaji wa gharama za Elimu ya Juu na fursa za Elimu ya Juu kwa kuwatembelea wadau mbalimbali wa elimu katika mikoa mitano ya Mara, Kigoma, Manyara, Arusha na Singida. Jumla ya shule 50 zilitembelewa na kuwafikia wanafunzi 7,481;

(c) Ili kupunguza tatizo la wahadhiri, iligharimia mafunzo ya Wanataaluma 80 kutoka vyuo vikuu 10 vya umma katika masomo ya shahada za uzamili na uzamivu na kugharimia mafunzo ya wahadhiri 18 wa shahada ya Uzamivu kwa kushirikiana na shirika la DAAD la Ujerumani. Aidha, idara iliratibu skolashipu 193 zinazotolewa na nchi mbalimbali;

(d) Ilikamilisha na kuzindua Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJU);

(e) Iliwezesha wafanyakazi 131 katika vyuo 8 kujiunga na mafunzo ya Shahada za Uzamili na Uzamivu kupitia Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (Science Technology and Higher Education Project) unaoendeshwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia kwa lengo la kuimarisha ufundishaji wa sayansi na teknolojia katika Elimu ya Juu ambapo jumla ya programu tano zimepitiwa na kufanyiwa marekebisho; na

(f) Iiliandaa rasimu ya namna ya kushirikisha Taasisi za fedha katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kama njia mbadala ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Ukaguzi wa Shule ina majukumu ya kuhakikisha kuwa Sera, Sheria, Kanuni na Viwango vya utoaji elimu vilivyowekwa vinatekelezwa kwa ufanisi katika shule za awali, msingi, sekondari, vitengo vya elimu maalum, vituo vya ufundi stadi, Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi na vyuo vya ualimu. Mwaka 2005 – 2010, idara iliimarisha Ukaguzi wa shule kwa kuongeza wakaguzi wa shule 365, kukarabati ofisi za Ukaguzi wa shule katika Wilaya 55 na kununua samani za ofisi katika wiliya 53. Aidha, zilinunuliwa kompyuta 120 na magari 91 kwa ajili ya ofisi za kanda na Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Idara ya Ukaguzi wa Shule:-

(a) Ilikagua jumla ya asasi 9,960 ambayo ni asilimia 49.56 ya asasi 20,094 zilizokuwa zimelengwa. Aidha, ilifanya ukaguzi maalum kwa ajili ya uanzishwaji wa shule mpya za sekondari 147 na msingi 51 na kuchunguza tuhuma na matukio maalum katika shule za sekondari 27 na shule za msingi 627. (Jedwali Na. 1 kinaonesha utekelezaji wa malengo ya ukaguzi wa shule hadi Juni 2010);

(b) Ilikarabati ofisi za ukaguzi wa shule katika Wilaya 20 na kununua samani za ofisi kwa ajili ya Wilaya 20 na magari 27 kwa ajili ya ofisi za Kanda na Wilaya;

(c) Ilifanya ufuatiliaji ili kubaini asasi za kielimu zinazoendeshwa kinyume na taratibu katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo asasi 830 zilipatikana na makosa. Kati ya hizo, 203 zilikutwa na dosari ndogondogo na 627 zilikutwa na dosari kubwa na kuagizwa kusitisha mara moja utoaji elimu;

(d) Iliendesha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili mwaka 2009 ambapo matokeo ya mtihani yalikuwa kama ifuatavyo: kati ya watahiniwa 394,508 waliojiandikisha kufanya mtihani, 364,957 (92%) walifanya mtihani huo. Watahiniwa 238,267 (65.3%) walifaulu, ambapo wavulana walikuwa 142,691 na wasichana 95,576. Aidha, watahiniwa 126,690 (34.7%) walifeli mtihani huo; na

(e) Ilianzisha utaratibu mpya wa kufanya ukaguzi wa shule ambapo shule zilizobainika kuwa chini ya wastani wa ubora wa shule uliowekwa zitakaguliwa zaidi ya mara moja kwa mwaka ili kufuatilia utekelezaji wa ushauri na kutoa msaada wa kitaalam na kitaaluma mpaka kufikia kiwango cha juu cha ubora wa shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Sera na Mipango inahusika na utoaji wa utaalam na huduma katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010 Idara ya Sera na Mipango:-

(a) Ilikusanya na kuchambua maoni ya wadau kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo na kuandaa rasimu ya kwanza ya pendekezo la Sera Mpya. Rasimu hii iliwasilishwa kwenye Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii mwezi Februari 2010 kwa ajili ya kupata maoni;

(b) Iliendelea kuimarisha mfumo wa takwimu za elimu (Educational Data Base System) katika Halmashauri 105 zilizobaki kwa kushirikiana na UNESCO kupitia programu ya ESMIS. Mfumo wa takwimu za elimu katika Halmashauri za Wilaya 28 zilizo kwenye majaribio (Pilot) ziliendelea kuimarishwa;

(c) Iliratibu uanzishwaji wa mradi wa Tanzania beyond Tomorrow ambao unahusu ufundishaji na ujifunzaji kwa kutumia TEHAMA kwenye shule za sekondari;

(d) Ilikarabati baadhi ya miundombinu kwenye vyuo vya ualimu vya Vikindu, Mhonda na Ilonga;

(e) Ilikarabati maabara tatu (3) za Lugha katika vyuo vya ualimu vya Butimba, Morogoro na Mtwara Ufundi na kuzipatia vifaa husika kwa ushirikiano na Shirika la USAID;

(f) Ilianza ujenzi wa shule mpya ya Miono inayojengwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Cushman and Wakefield ya Brussels - Ubelgiji; na
(g) Ilijenga shule mbili za Msingi kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China huko Msoga – Pwani, na Kiteto - Manyara.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu inasimamia masuala ya utawala, ajira, maslahi na maendeleo ya watumishi pamoja na sheria, kanuni, taratibu za utumishi na kuratibu masuala ya Programu ya Kuboresha Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2009/2010, Wizara yangu ilikabiliwa na madeni makubwa ya ndani yaliyojumuisha madai ya walimu na watumishi wasio walimu, wazabuni na posho za nyumba kwa wahadhiri wa Vyuo Vikuu.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2009/2010 Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu:-


(a) Ilishughulikia madai ya watumishi 25,440 yenye thamani ya shilingi 22,779,602,062 yaliyohusu malimbikizo ya mishahara, gharama za matibabu, likizo, safari za kikazi na gharama za masomo. Ilihakiki madeni hayo na kulipa kiasi cha shilingi 5,321,096,409.22 ikiwa ni madai yaliyokubaliwa wakati wa uhakiki kwa kushirikiana na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Aidha, Wizara bado inaendelea kushughulikia madai yaliyochelewa kuwasilishwa. Mpaka kufikia tarehe 07/06/2010, Wizara yangu imepokea jumla ya madai yenye thamani ya shilingi 6,203,679,120.60;

(b) Iliunda Kikosi Kazi (Task Force) kwa ajili ya kushughulikia rufaa za madeni zilizowasilishwa baada ya kukataliwa. Kamati hiyo inahusisha Maafisa toka Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Utumishi wa Walimu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Chama cha Walimu Tanzania na Maafisa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Hadi kufikia mwezi Mei 2010, jumla ya shilingi 17,703,392,146 zilikuwa zimelipwa kwa wazabuni;

(c) Ilishughulikia malipo ya madai ya wazabuni waliotoa huduma ya chakula na vifaa vya maabara ambapo, hadi kufikia mwezi Mei 2010, jumla ya shilingi bilioni 17.70 zilikuwa zimelipwa; na
(d) Ilishughulikia malipo ya madai ya wazabuni waliotoa huduma ya chakula na vifaa vya maabara ambapo, hadi kufikia mwezi Mei 2010, jumla ya shilingi bilioni 17.70 zilikuwa zimelipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano kina majukumu ya kuratibu utoaji na upokeaji wa habari za kielimu na kushirikiana na vyombo vya habari na wadau wengine wa sekta ya elimu katika kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano:-

(a) Kiliandaa na kuratibu urushaji wa vipindi 30 vya redio na televisheni ili kuifahamisha na kuihamasisha jamii kuhusu mikakati, mafanikio na changamoto za sekta ya elimu katika kutekeleza mipango ya elimu;

(b) Kiliandaa na kuchapisha nakala 25,000 za Jarida la EdSDP na kuzisambaza katika Kanda za elimu, taasisi na Wizara mbalimbali ili kuhamasisha jamii kushiriki katika kutekeleza mipango ya elimu;

(c) Kiliratibu maandalizi ya majibu ya maswali 30 yaliyopokelewa kutoka Tovuti ya Wananchi; na

(d) Kiliandaa Mkakati wa Mawasiliano kuhusu Ugatuaji wa Uendeshaji wa Shule za Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala, Taasisi na Mabaraza yaliyo chini ya Wizara yangu yanawajibika katika kuchangia usimamizi na hatimaye kufanikisha utoaji wa elimu bora nchini. Mwaka huu, kila Wakala, Taasisi na Baraza lilitekeleza kazi zilizopangwa kwa kuzingatia malengo na mipango ya elimu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ina jukumu la kutoa mafunzo ya elimu ya Watu Wazima na elimu ya kujiendeleza katika mfumo usio rasmi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima:-
(a) Iliongeza idadi ya wanachuo wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana kutoka 30,036 hadi 49,533 ambayo ni asilimia 99.1 ya idadi iliyokuwa imelengwa ya 50,000;

(b) Ilitoa mafunzo ya cheti kwa walengwa 40, stashahada 371, stashahada ya Juu 128 na Shahada ya Elimu yaWatu Wazima (NTA Level 7-8) 82;

(c) Iliwajengea uwezo wakufunzi na wahadhiri 56 wa Taasisi ya Elimu yaWatu Wazima katika kufundisha kwa kutumia mtaala unaozingatia soko la jira na masharti ya NACTE yanayolenga katika kuwapa umahiri (Competence-Based Education and Training);

(d) Ilianzisha programu ya Integrated Post-Primary Education (IPPE) ambayo inajumuisha Elimu ya Sekondari, ufundi stadi na masuala mtambuka, katika wilaya za Temeke, Bagamoyo, Siha, Mtwara Vijijini, Hai, Magu na Makete;

(e) Iligharimia mafunzo ya watumishi wawili wa shahada ya Uzamivu; tisa shahada ya Uzamili, mmoja wa Stashahada ya Juu, wawili wa cheti, 15 mafunzo ya muda mfupi na watano wa Elimu ya Sekondari;

(f) Ilinunua vifaa vya studio itakayotumika katika kutoa elimu ya masuala mtambuka, haki za binadamu, utunzaji wa mazingira, afya bora, umaskini na elimu ya kujikinga na UKIMWI kwa umma nchini;

(g) Iliunda Kamati ya Kudhibiti Ubora (Quality Assurance Committee) ili itengeneze mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya programu za TEWW; na

(h) Ilifuatilia na kutathmini utekelezaji wa mpango wa Elimu Masafa (Open Distance Learning - ODL) katika vituo vya mikoa 21.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Elimu Tanzania ina majukumu ya kubuni na kuandaa mitaala na mihtasari ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu na elimu maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Taasisi ya Elimu Tanzania:-
(a) Iliendesha mikutano 15 ya paneli za masomo ya mitaala ya shule na Vyuo vya Ualimu ili kupata maoni yatakayochangia katika kufanya mapitio ya mihtasari na hivyo kuinua ubora wa elimu;

(b) Iliandika moduli za masomo 26 kwa ajili ya mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti ambayo inasubiri kuhaririwa, na miongozo ya kufundishia masomo ya Kidato cha 1 – 4 ambayo inasubiri kuhakikiwa na kuchapishwa;

(c) Iliandika miongozo ya walimu ya kufundishia masomo 25 ya mtaala wa masomo ya Kidato cha tano na sita ambayo iko katika hatua ya uhakiki na uhariri;

(d) Ilichapa na kusambaza vitabu 24 vya mwaka wa pili wa MEMKWA vya kundi-rika 1 na 2;

(e) Ilikamilisha maandalizi ya vipindi 6 vya redio na televisheni kwa ajili ya masomo ya Hisabati na Kiingereza kwa darasa la III na IV;

(f) Iliandaa chati za somo la sayansi kwa ajili ya darasa la I-VII ambazo zinasubiri kufanyiwa majaribio kabla ya kuchapishwa; na

(g) Ilifanya majaribio ya miongozo ya kufundishia UKIMWI katika shule za awali na msingi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ina jukumu la kutoa na kusambaza huduma za maktaba kwa watu wote nchini; kuanzisha, kuendesha, kuongoza, kuimarisha, kutunza na kuendeleza Maktaba za Umma kuanzia ngazi za Mikoa,Wilaya hadi Vijiji na kutoa mafunzo na kuendesha mitihani ya Taaluma ya Ukutubi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania:-


(a) Ilikamilisha mpango mkuu wa kiwanja (Master Plan) kwa ajili ya Chuo cha Ukutubi na uhifadhi Nyaraka, Bagamoyo. Aidha, ilinunua viwanja viwili kwa ajili ya kujenga hosteli;
(b) Iliimarisha na kuboresha huduma za Maktaba kwa watu wazima na watoto katika mikoa 19 ikiwa ni pamoja na kuongeza machapisho 63,519 ya vitabu, magazeti na majarida 35,257, kurakai vitabu 135 na kujaridi mabunda 65 ya magazeti;

(c) Ilitoa mafunzo ya Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka kwa walengwa 113 wa Stashahada, 192 wa Cheti na 151 wa mafunzo ya muda mfupi;

(d) lihamasisha wananchi katika mikoa 21 nchini ili wajenge utamaduni wa kusoma, kwa kuendesha matamasha mawili ya vitabu katika mkoa wa Dar es Salaam na kuongeza idadi ya wasomaji kufikia 886,103; na

(e) Ilitoa ushauri wa kitaalam juu ya uanzishaji, upangaji na uendeshaji wa Maktaba za vyuo na taasisi. Ushauri ulitolewa kwa maktaba 89 za shule, moja ya chuo na moja ya taasisi moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Agency for the Development of Educational Management - ADEM) una majukumu makuu manne: kuandaa na kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu; kutoa ushauri wa kitaalamu katika mambo yanayohusu Uongozi na Uendeshaji wa Elimu; kufanya utafiti katika masuala yanayohusu Uongozi na Uendeshaji wa Elimu na kuandaa na kusambaza makala na vitabu mbalimbali vya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu. Katika kipindi cha 2005 – 2010, Wakala umeweza kutoa wahitimu 671 wa Stashahada ya Usimamizi wa Elimu (Diploma in Education Management).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ulitekeleza yafuatayo:-

(a) Ulitoa mafunzo ya stashahada ya Uongozi wa Elimu kwa wanachuo 289 kati ya 300 waliokuwa wametarajiwa;

(b) Ulitoa mafunzo ya Cheti cha Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa Walimu Wakuu 100 wa Shule za Msingi kati ya 500 waliokuwa wamelengwa katika Vyuo vya Ualimu vya Tabora na Butimba;

(c) Ulitoa mafunzo ya Uongozi na Uendesahji wa Elimu kwa Waratibu Elimu kata 435 kutoka katika wilaya za Manyoni, Newala, Tandahimba, Bariadi, Meatu, Mpanda, Nkasi, Manispaa ya Morogoro, Kilosa, Ulanga, Ilala, Handeni, Kilindi, Mwanga, Rombo, Siha, Biharamulo, Chato, Muleba na Ngara. Mafunzo haya yanakamilisha lengo la kutoa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata nchi nzima;

(d) Ulitoa mafunzo juu ya utayarishaji wa Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule (Whole School Development Planning) kwa Maafisa 185 kati ya 194 waliolengwa;

(e) Ulitoa mafunzo ya mwezi mmoja ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa washiriki 92 yaliyoshirikisha Maafisa Elimu Taaluma wa Mikoa. Maafisa Elimu Taaluma na Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya 80 kutoka Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Singida, Pwani, Shinyanga, Morogoro, Rukwa, Mbeya na Kigoma; na

(f) Ulikamilisha ripoti ya utafiti wa kielimu kuhusu kuinua Ubora wa Uongozi, kwa kuzingatia athari za tabia za Wakuu wa Shule katika kumotisha utendaji wa walimu. Mradi huu uliendeshwa chini ya mtandao wa LEAD-link (Leadership in Education for African Development) unaohusisha nchi za Tanzania, Malawi, Uganda, Zambia, Sudan, Swaziland, Msumbiji na Afrika Kusini. Mtandao huu unafadhiliwa na Uholanzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Taifa ya UNESCO ina majukumu ya kulishirikisha Taifa katika utekelezaji wa programu za UNESCO nchini kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nyanja za Elimu, Sayansi Asilia, Sayansi Jamii, Utamaduni, Mawasiliano na Habari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010, Tume ya Taifa ya UNESCO:-

(a) Iliratibu ushiriki wa ujumbe wa Serikali na wataalamu mbalimbali katika masuala ya UNESCO kwenye Kikao cha 35 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO ambapo mjumbe mmoja aliwakilisha vijana;

(b) Iliendelea kusimamia, kuratibu, pamoja na kutathmini utekelezaji wa miradi chini ya Participation Programme kwa kipindi cha 2008/2009.

(c) Iliendelea kuratibu utekelezaji wa Programu ya Kuhifadhi Historia ya Ukombozi Barani Afrika;
(d) Iliendelea kuratibu Programu ya Uhuishaji wa Mfumo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa kushirikiana na UNESCO;

(e) Ilisimamia utekelezaji wa miradi chini ya sekta tano za UNESCO pamoja na programu ya Mwaka wa Kimataifa wa Astronomia;

(f) Iliendelea kuratibu utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Mwaka wa Kimataifa wa Sayari Dunia (Intenational Year of Planet Earth- IYPE);

(g) Ilichapisha na kusambaza toleo Na. 6 la Jarida la Tanzania na UNESCO;

(h) Iliendelea kutoa elimu kuhusu masuala mtambuka ya jinsia, mazingira na Haki za Binadamu chini ya Mtandao wa Shule (Associated School Project Network); na

(i) kuimarisha Mtandao wa UNESCO wa shule zilizoshirikishwa (Associated Schools Project Network) kwa kushirikiana na asasi za Serikali na zisizo za kiserikali Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la Mitihani la Tanzania lina majukumu ya kuweka sera ya mitihani kwa kuzingatia Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. Aidha, Baraza lina majukumu ya kuendesha Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi na Sekondari, Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada, mtihani wa Maarifa na kusimamia uendeshaji wa mitihani itolewayo na bodi za nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Baraza la Mitihani la Tanzania:-

(a) Liliendesha Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2009 kwa watahiniwa 1,024,448;

(b) Liliendesha Mitihani ya Kidato cha Nne kwa watahiniwa 351,152 na Mtihani wa Maarifa (QT) kwa watahiniwa 25,040;

(c) Liliendesha Mtihani wa Kidato cha Sita 2010 kwa watahiniwa 65,629 na Mitihani ya Ualimu Mei 2010 ambapo jumla ya watahiniwa 22,212 walisajiliwa;
(d) Lilisimamia Mitihani ya Bodi za Nje kwa watahiniwa 832;

(e) Lilinunua printa ya kisasa ya kuchapia vyeti vyenye icha za watahiniwa ili kudhibiti udanganyifu;

(f) likamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Kituo ha Usahihishaji Mitihani cha Mbezi kilichoanza utumika rasmi Mei 2010; na

(g) Lilifanya uhakiki wa vyeti 54,357 vilivyowasilishwa na asasi mbalimbali ambapo vyeti 1,756 sawa na silimia 3.2 vilibainika kuwa ni vya kughushi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Maendeleo Dakawa chenye eneo la Ekari 7,500 kina jumla ya nyumba 82 na majengo mengine muhimu yanayowezesha uendeshaji wa: Chuo cha Ualimu chenye jumla ya Wanachuo 580 na Wafanyakazi 50; Shule ya Sekondari ya Wasichana yenye kidato cha tano na sita ambayo ina jumla ya wanafunzi 450 na wafanyakazi 20, Chuo cha Ufundi Stadi- VETA chenye jumla ya Wanachuo 160 na wafanyakazi 20, Shule ya Msingi ambayo ina wanafunzi 400 wa Elimu ya Msingi na 50 wa Elimu ya Awali pamoja na walimu 15. Aidha, kituo kina Zahanati inayotoa huduma kwa wanajamii 4,500 walio ndani ya kituo na maeneo ya jirani. Zahanati hii ina Maafisa Tabibu wawili na Wauguzi watatu. 63.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo kina majukumu ya kutunza na kuhifadhi majengo, vifaa na miundombinu iliyokabidhiwa na ANC kwa ajili ya kulinda historia ya ukombozi Kusini mwa Afrika. Baada ya Serikali ya Tanzania kukabidhiwa Kituo cha Maendeleo Dakawa kutoka kwa wapigania Uhuru wa ANC, Wizara yangu imekusudia kukiendeleza na kukitumia katika kutoa Elimu ya Sayansi na Ufundi kupitia Taasisi zilizopo na zitakazoanzishwa hapo Dakawa.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Kituo cha Maendeleo Dakawa:-


(a) Kilisimamia na kukarabati matanki ya kuhifadhia maji safi na njia kuu ya majisafi kwa umbali wa kilomita 17 kutoka chanzo cha maji (Wami) hadi kituoni;
(b) Kilitoa huduma ya kuondosha majitaka katika makazi ya watu ambayo jumla yao ni zaidi ya 2,000 na kufanya matengenezo ya mifumo ya majisafi na majitaka;

(c) Kiliratibu na kusimamia utunzaji wa mazingira ya kituo yenye eneo la kilometa za mraba 28 kama kilivyokabidhiwa na ANC; na

(d) Kiliratibu shughuli za kampuni ya ulinzi iliyopewa zabuni ya kulinda eneo zima la kituo na kudhibiti usalama wa vifaa na miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Elimu Tanzania ina majukumu ya kutafuta na kubaini vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya kugharimia maendeleo ya sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wadau wa elimu kuchangia kwa hiari katika miradi ya elimu. Katika kipindi cha 2005 – 2010, mamlaka iliweza kukusanya Shilingi bilioni 4.7 na kutumia shilingi bilioni 34.3 kugharimia maendeleo katika sekta ya elimu. Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi 25, Vyuo vya ualimu 16 na shule za awali na za msingi 61 na za sekondari 724 zimenufaika. Aidha, mamlaka ilitoa ufadhili wa Shilingi 91.8 milioni kwa ajili ya Pre-entry Programme kwa wasichana katika vyuo vikuu viwili na na vyuo vya ufundi viwili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Mamlaka ya Elimu Tanzania:-

(a) Iliendelea kutafuta rasilimali mbadala kwa ajili ya mfuko wa elimu kwa kuandaa harambee, kuwekeza katika amana za muda mfupi na kutafuta wahisani wa kufadhili au kusaidia baadhi ya miradi. Kufuatia jitihada hizi Shilingi milioni 836 zilipatikana. Kadhalika wahisani wafuatao wameonyesha nia ya kufadhili miradi ya elimu: Abbott Fund (Mradi wa maabara za sekondari), Sightsavers International (Mradi wa kuwawezesha wanafunzi wenye ulemavu wa kuona kujifunza kwa kutumia TEHAMA), Songas, (mradi wa madawati na vitabu);

(b) Iliendelea kupokea maombi na kufadhili miradi mbalimbali ya elimu yenye kulenga katika kuongeza ubora wa elimu na udahili, na kuleta usawa wa kijinsia. Taasisi 177 zilipata ufadhili wenye thamani ya shilingi 1.9 bilioni kwa ajili ya miradi ya kuinua ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Aidha, Mamlaka iliendelea kufadhili kozi za awali (Pre-entry Programmes) kwa wanafunzi wa kike wanaojiunga na Vyuo Vikuu;
(c) Iliendeleza ushirikiano na Halmashauri katika kuhimiza uanzishwaji wa mifuko ya elimu pamoja na kuhamasisha wadau kuchangia elimu kwenye maeneo yao, kwa kuandaa harambee kwa pamoja. Mamlaka ilishiriki kwenye harambee za Halmashauri 12 kwa lengo la kuzisaidia kuchangisha;

(d) Iliandaa rasimu ya marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Elimu No. 8 ya mwaka 2001 ambapo zoezi la kuandaa Waraka wa Baraza la Mawaziri umeanza;

(e) Iliendelea kutoa elimu kwa umma na kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari, vipeperushi na majarida. Aidha, Mamlaka ilishiriki katika vipindi vya radio na televisheni. Tovuti ya TEA www.tea.or.tz iliimarishwa kwa kubadili muonekano wake na kurahisisha utafutaji taarifa. Aidha, mamlaka iliandaa jarida la televisheni juu ya mfuko na kampeni ya kuchangia wanafunzi wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu);

(f) Ilifanya tathmini ya miradi 90 kwa lengo la kupima matokeo ya ufadhili; na

(g) Ilikamilisha makubaliano ya kununua majengo yanayomilikiwa na Shirika la Bima yaliyopo Mikocheni B kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ina jukumu la kutoa ithibati, kuratibu uanzishwaji wa Vyuo Vikuu, kuhakiki ubora wa elimu na kuidhinisha programu zifundishwazo ili zikidhi mahitaji ya Taifa na soko la ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania:-


(a) Ilitathmini ubora wa programu 25 za masomo ya Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vishiriki nchini kwa lengo la kuziidhinisha;

(b) Ilikamilisha rasimu ya andiko la Mfumo wa Tuzo zinazotambuliwa Kitaifa (National Qualifications Framework) na kuanza maandalizi ya andiko la kanuni za mfumo wa tuzo;

(c) Ilitathmini vyeti 250 vilivyowasilishwa na wahitimu wa vyuo vikuu toka nje ya nchi kwa lengo la kutambua uhalali wake;
(d) Iliratibu na kutathmini mradi wa majaribio ya kudhibiti ubora wa programu za vyuo vikuu 5 (St. John’s University, University of Dodoma, State University of Zanzibar, Dar es Salaam University College of Education na Muslim University of Morogoro) vinavyotekeleza mradi huo chini ya IUCEA;

(e) Ilikagua na kutathmini mipango ya kuanzisha au kuhuisha vyuo vikuu saba kwa lengo la kutoa hati husika. Vyuo hivyo ni: Chuo Kikuu cha Dodoma, St. John’s University, Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, Chuo Kikuu kitarajiwa cha Eckenford (proposed Eckenford University), St. Augustine University of Tanzania – Mtwara Centre, Kampala International University – DSM Centre na Chuo Kikuu kitarajiwa cha Mara (proposed Mara University); na

(f) Ilianzisha mfumo mpya wa udahili wa pamoja wa wanafunzi ujulikanao kama Centralized Admission System (CAS) ambao unahusisha vyuo vya elimu ya juu 43 (hivi ni pamoja na Vyuo vya Elimu ya Juu visivyokuwa Vyuo Vikuu) ili kuondoa uwezekano wa mwanafunzi mmoja kudahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja na hivyo kuwanyima nafasi Watanzania wengine wenye sifa za kujiunga na Taasisi nyingine za elimu ya juu, kudhibiti uhalali wa vyeti vya waombaji nafasi katika Elimu ya Juu, kuwapunguzia wazazi na wanafunzi gharama za kuomba udahili katika vyuo vikuu na kuongeza nafasi za uteuzi kwa waombaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi linasimamia na kuratibu mitaala, ubora wa mafunzo, mitihani, tuzo, usajili na ithibati za vyuo vya elimu ya ufundi vya umma na binafsi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009/2010, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi:-

(a) Lilikagua vyuo 28 vya elimu na mafunzo ya ufundi na kuvipa ithibati;

(b) Lilikagua vyuo 24 vyenye uwezo wa kutoa elimu na mafunzo ya ufundi na kuvisajili na kuhakiki utekelezaji wa masharti ya ithibati katika vyuo 18 vyenye ithibati kamili;

(c) Liliratibu uandaaji wa mtaala wa elimu ya ufundi na kuidhinisha programu 46 zenye kuzingatia umahiri na mahitaji ya soko la ajira;
(d) Lilikagua na kutathimini sifa za wakufunzi 200 na kuwasajili;

(e) Lilisimamia na kuviwezesha vyuo 18 vya elimu ya ufundi kuweka mfumo wa kudhibiti na kuhakiki ubora wa mafunzo yatolewayo;

(f) Liliratibu mitihani ya elimu ya ufundi katika vyuo 28 vinavyotumia mtaala mpya unaozingatia umahiri wa mwanafunzi na mahitaji ya soko la ajira;

(g) Liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo 17 vya elimu ya ufundi vinavyotoa mafunzo ya elimu ya ufundi ngazi ya Shahada na Stashahada ya Juu; na

(h) Liliratibu mafunzo ya ufundishaji katika mfumo wa Competence Based Education and Training (CBET) kwa walimu kutoka vyuo 20 vya elimu ya ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ina majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi raia wa Tanzania wanaosoma katika Taasisi za Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi na kukusanya marejesho ya mikopo hiyo. Katika kipindi cha 2005 – 2010, Bodi ilitoa mikopo yenye thamani Shilingi 576.03 bilioni kwa wanafunzi130,060. Aidha, ilikusanya marejesho ya mikopo yenye thamani ya Shilingi 3.68 bilioni kati ya Shilingi15.48 bilioni zilizotakiwa kurejeshwa.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu:-

(a) Iliwakopesha wanafunzi 74,498 jumla ya Shilingi 197.3 bilioni kwa ajili ya kulipia gharama za chakula na malazi, vitabu na viandikia, ada za mafunzo, utafiti, mafunzo kwa vitendo na mahitaji maalum ya vitivo;

(b) Ilitoa mikopo ya asilimia 100 kwa wanafunzi 7,238 wanaochukua masomo ya sayansi katika vyuo vya elimu ya juu;

(c) Iliongeza madaraja ya mikopo kutoka sita hadi 11 na hivyo kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kama ifuatavyo: daraja ya A (100%), B (90%), C (80%), D (70%), E (60%), F (50%), G (40%), H (30%), I (20%), J (10%), na K (0%); na
(d) Iliendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali zikiwemo vipeperushi, magazeti, redio na televisheni, mikutano, warsha na maonesho yaliyowezesha Bodi kukutana na kuwasiliana ana kwa ana na wadau kuhusu wajibu wa kuchangia elimu ya juu, taratibu za utoaji mikopo na urejeshwaji wake. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ina majukumu ya kuratibu, kudhibiti, kugharimia, kutoa na kukuza elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi:-

(a) Ilifanya maandalizi ya ukarabati wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya za Karagwe na Korogwe baada ya Halmashauri za Wilaya hizo kuridhia taratibu za utekelezaji;

(b) Iliendelea na ujenzi wa chuo cha ufundi stadi cha Wilaya ya Makete;

(c) Ilifanya upanuzi, ukarabati na ufungaji wa vifaa vya kisasa katika vyuo vya ufundi vya: Mpanda, Shinyanga, Tabora, Ulyankulu, Singida na Njiro – Arusha;

(d) Iliendelea na ujenzi wa vyuo vya Lindi, Pwani, Manyara na Dar es Salaam;

(e) Ilitoa mafunzo kwa walimu 287 wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi wa ngazi ya Cheti. Aidha, iliwapatia washiriki 542 mafunzo ya muda mfupi katika maeneo mbalimbali (walimu wa ufundi 25 kutoka vyuo binafsi, wakuu wa vyuo 70 wa vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali) na watumishi 81 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wa Wizara ya Elimu Mafunzo ya kompyuta;

(f) Ilitoa mafunzo kwa walimu 37 katika ngazi ya Stashahada katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro. Aidha, walimu wengine 40 wanaendelea kuhudhuria mafunzo ya Stashahada katika chuo cha VETA Morogoro;

(g) Iliwawezesha wanachuo 700 kushiriki katika mafunzo kwa vitendo (Field Work) katika hoteli ya Movenpick na viwanda vya Tanga Cement na Chemi – Cotex. Aidha, ilikamilisha maandalizi ya mafunzo kwa vitendo katika viwanda vya A to Z Arusha, TPC - Moshi, Tumbaku - Morogoro, TANESCO – Dar es Salaam, Coca Cola – Dar es Salaam, na Aluminium Africa (ALAF);

(h) Iliimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Chamber of Minerals ambapo vifaa vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 1.3 milioni vilitolewa kwa ajili ya Chuo cha Ufundi Stadi, Moshi na Dola 500,000 za Kimarekani zilizotolewa na Canada kwa ajili ya Chuo cha Ufundi Stadi Mkoa wa Mwanza. Viwanda vya madini vimeanza kufaidika na stadi zinazofundishwa; na

(i) Ilianza kufanya majaribio ya mkakati wa kutoa mafunzo katika sekta ya kilimo katika Kanda ya Mashariki na mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na wa kisasa katika Kanda ya Kati, kwa kushirikiana na shirika la Swiss Contact. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mheshimwa Spika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina jukumu la kutoa mafunzo, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam.


Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009/2010, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam:-

(a) Kilidahili wanafunzi 6,345 wa mwaka wa kwanza, ambapo 3,686 walikuwa wa shahada ya kwanza (wanawake 1,290) na 2,659 na wa shahada za uzamili na uzamivu (wanawake 764);

(b) Kiliendeleza ushirikiano na wafadhili mbalimbali katika kugharimia, taaluma, utafiti na kusambaza matokeo yake na ujenzi wa miundombinu;

(c) Kilitoa machapisho 17 ya vitabu na 275 ya majarida na kusambaza matokeo ya utafiti katika nyanja za demokrasia na utawala bora, biashara na uongozi, lugha, mazingira, sayansi asilia sheria, TEHAMA, uhandisi wa fani mbalimbali na ujasiriamali;

(d) Kiliajiri wanataaluma 380 ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi na pia kujaza nafasi za kazi zilizoachwa wazi na walioondoka;

(e) Kiligharimia mafunzo ya wafanyakazi wanataaluma 56 na waendeshaji 22;
(f) Kiliendeleza awamu ya tatu ya ujenzi wa jengo la Shule Kuu ya Biashara;

(g) Kiliendeleza upanuzi wa jengo la Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii kwa ajili ya semina;

(h) Kiliendeleza ujenzi wa kumbi mbili za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 kila moja;

(i) Kilifuatilia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa Mlimani City;

(j) Kilifanya mazungumzo ya kuendeleza ujenzi wa Makao Makuu mapya ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (Institute of Marine Sciences - IMS) eneo la Buyu – Zanzibar;

(k) Kiliendeleza mchakato wa ujenzi wa kumbi za mihadhara na semina, maabara, ofisi za taaluma na jengo la makumbusho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kupitia mradi wa Serikali wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia unaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.

(l) Kilikarabati hosteli sita za wanafunzi, kumbi za semina na mihadhara na nyumba 13 za wafanyakazi;

(m) Kilikamilisha makubaliano na Msajili wa Hazina na Mamlaka ya Bima (TIRA) kuhusu kuhamisha majengo ya Chuo cha Bima Mikocheni kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati taratibu za kisheria zikichukua mkondo wake;

(n) Kilikamilisha makubaliano na Manispaa ya Kinondoni kuhusu kuhamisha Shule ya Msingi Mlimani kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati taratibu za kisheria zikichukua mkondo wake; na


(o) Kilianzisha mchakato wa uchangiaji kutoka kwa wafanyakazi na wadau wa Chuo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Centre).


Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kina majukumu ya kufundisha, kutafiti, kutoa ushauri na huduma za kitaalamu katika maeneo ya Elimu na Ualimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kilitekeleza yafuatayo:-

(a) Kilidahili wanafunzi wapya 946 ambapo 120 ni wa masomo ya sayansi na 826 ni wa masomo ya Sanaa na Sayansi ya Jamii., na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wote chuoni hapo kuwa 2,966 ambapo 763 ni wa mwaka wa pili na 1,257 ni wa mwaka wa tatu;

(b) Kilikamilisha ujenzi wa kumbi tatu za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,000 kwa wakati mmoja. Kumbi hizo zinatarajiwa kuanza kutumika rasmi katika mwaka wa masomo 2010/2011;

(c) Kiliendelea kugharimia mafunzo ya watumishi 77, ambapo wahadhiri 55 wako kwenye mafunzo ya shahada za uzamili na 22 kwenye shahada za uzamivu ndani na nje ya nchi;

(d) Kiliendelea kuimarisha miundo mbinu na matumizi ya TEHAMA; na

(e) Kiliendelea kushirikiana na vyuo na taasisi za ndani na nje ya nchi katika utafiti na mafunzo, hususan kwa shahada za uzamili na uzamivu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa kina majukumu ya kufundisha, kutafiti, kutoa ushauri na huduma za kitaalam katika maeneo ya Ualimu na Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa:-

(a) Kilidahili wanafunzi wapya 750 wa shahada ya kwanza kati ya 800 waliokuwa wamelengwa;

(b) Kiliendelea na mchakato wa upanuzi wa maktaba awamu ya pili kwa kumteua mkandarasi mshauri wa mradi;

(c) Kiliendelea na mchakato wa kuanza ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja na kuanza maandalizi ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi;

(d) Kilikamilisha andiko la mradi wa ujenzi wa jengo la utawala;
(e) Kilikamilisha ujenzi wa uzio wa Chuo wa awamu ya pili kwa kupanda miti eneo lote la mipaka ya Chuo; na

(f) Kilikamilisha ukarabati wa barabara za ndani ya Chuo awamu ya kwanza na ya pili.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ilianzishwa mwaka 2003, kufuatia kufutwa kwa Sheria ya mwaka 1981 iliyoanzisha Chuo kilichoitwa Tanzania School of Journalism (School of JournalismAct No. 8) na kukifanya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Chuo hicho kilihamishwa kutoka Wizara ya Habari na kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupewa hadhi ya kuwa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (School of Journalism and Mass Communication). Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ina majukumu ya kutoa elimu na mafunzo ya Shahada, Stashahada ya Juu na Cheti katika nyanja mbalimbali, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaaluma na kitaalam katika masuala ya habari, mawasiliano, mahusiano ya umma, matangazo ya biashara, pamoja na utangazaji.


Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu iwe sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu hii imekua na kupanua shughuli zake kwa kutoa Shahada za Kwanza ya Uandishi wa Habari (BA in Journalism), Shahada ya Kwanza ya Mawasiliano ya Umma (BA in Mass Communication), Shahada ya Kwanza ya Uhusiano wa Umma na Matangazo (BA in Public Relations and Advertising) na Stashahada ya Juu ya Mawasiliano ya Umma (Post-Graduate Diploma in Mass Communication). Ili kuinua ubora wa ufundishaji na kutoa Elimu kwa vitendo, Shule Kuu imeanzisha vituo vya utangazaji vijulikanavyo kama Radio Mlimani na Mlimani Television pamoja na gazeti la kila wiki la The Hill Observer.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma:-


(a) Iliongeza idadi ya wanachuo kutoka 40 waliokuwepo kabla ya mwaka 2003 hadi wanafunzi 300 mwaka 2009/10;
(b) Iliajiri wanataaluma sita;

(c) Iliandaa mtaala wa Shahada za Uzamili; na

(d) Ilikarabati vyumba 8 vya mihadhara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kinatekeleza majukumu yake ya kutoa mafunzo ya Shahada za Kwanza, Shahada za Uzamili na Uzamivu, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja za Kilimo, Misitu, Mifugo, Mazingira, wanyama pori, ufugaji wa samaki na fani nyingine za Sayansi na Teknolojia. Katika kipindi cha mwaka 2005 – 2010, chuo kilitoa wahitimu 4,473. Kati ya hao, 3,969 walikuwa wa shahada za kwanza 811 wa shahada za Uzamili na 65 wa shahada za Uzamivu.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo:-


(a) Kiliendeleza utafiti sehemu mbalimbali nchini unaolenga katika kuinua ubora wa kilimo, hifadhi za misitu, mifugo na maliasili nyingine, ikiwa ni pamoja na matumizi ya wanyamakazi katika Kilimo (Kisilo Wilaya ya Njombe); Mradi wa mbinu bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji (Wilaya ya Handeni); uzalishaji wa matunda na mboga (Wilaya za Morogoro na Mvomero) ambapo wakulima zaidi ya 1,500 hufaidika na mazao kutoka kwenye bustani hiyo kila mwaka;

(b) Kiliendeleza hifadhi na ukarabati wa Chanzo cha Maji cha Mto Mzinga kwa kushirikiana na jamii;

(c) Kiliendelea, chini ya mradi wa PANTIL, kutoa elimu kwa wanavijiji juu ya umuhimu wa upandaji miti, ufugaji nyuki na kuongeza matumizi ya pembejeo na ukuzaji wa soko kwa aina za miti isiyojulikana na isiyotumika sana nchini Tanzania. Mikoa ya Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Arusha wamehamasishwa kupanda na kutumia miti hiyo. Mradi huu umetoa machapisho 11 kwenye majarida ya kisayansi;

(d) Kilitoa ushauri wa kitaalam katika: kilimo, mifugo, misitu, wanyamapori, umwagiliaji na tiba ya wanyama ambayo yalikiingizia chuo Sh. 38,009,052.50;
(e) Kiliendelea na mradi wa ‘Uboreshaji wa Zao la Maharage’ ambao umewezesha kutoa aina za maharage za PESA na MSHINDI ambazo hupevuka mapema na kuiva haraka wakati wa kupika; na

(f) Kiliandaa shahada za kwanza sita ambazo ni:- Bachelor of Science in Human Nutrition, Bachelor of Science in Family and Consumer Sciences, Bachelor of Irrigation and Water Resources, Bachelor of Bioprocess and Post-harvest Engineering, Bachelor in Applied Agricultural Extension na Bachelor of Agricultural Education zitakazodahili jumla ya wanafunzi 470 katika mwaka wa masomo 2010/2011. Aidha, chuo kiliandaa stashahada 2 ambazo ni: Diploma in Tropical Animal Health na Diploma in Laboratory Technology Science.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Elimu ya Biashara cha Moshi ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Majukumu yake ni kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri katika nyanja za ushirika, maendeleo ya jamii, biashara, oganaizesheni, ujasiriamali na masuala mtambuka.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10 Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Elimu ya Biashara Moshi:-


(a) Kiliongeza udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka wanafunzi 2,186 (wa kike 734) mwaka wa masomo 2008/09 hadi 2,713 (wa kike 980) mwaka 2009/10. Hili ni ongezeko la wanafunzi 527 ambayo ni sawa na asilimia 24 (asilimia 33.5 kwa wasichana). Aidha, chuo kilianzisha programu mpya mbili za Cheti katika Kampasi ya Kizumbi - Shinyanga zenye jumla ya wanafunzi 84 ;

(b) Kiligharimia mafunzo ya wanataaluma 24 wanaoendelea na masomo katika ngazi mbalimbali (Shahada za Uzamivu 13 (wanawake wawili, na wanaume 11), Shahada za Uzamili 11 (mwanamke mmoja)) na wafanyakazi waendeshaji wanne (Stashahada ya Uzamivu wanne (wanawake watatu);

(c) Kiliendelea kuimarisha shughuli za utafiti na uchapishaji kupitia mpango wa utafiti mdogo unaogharimiwa na chuo, kwa njia ya ushindani na uendeshaji wa warsha za kuwajengea uwezo wanataaluma katika utafiti na ushauri;
(d) Kiliendelea kuimarisha vituo vya mikoani kwa kuviongezea wafanyakazi, kuainisha mahitaji, kuyaingiza kwenye bajeti ya Chuo. Aidha, kiligharimia ukarabati wa vituo vya Mwanza na Shinyanga;

(e) Kiliendelea kuimarisha ushirikiano na vyuo ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Makerere , Chuo Kikuu cha Malawi, Chuo Kikuu cha Zambia, Chuo cha Ushirika cha Uingereza na Chuo cha Biashara na Teknolojia cha Humber kilichoko Canada;

(f) Kiliimarisha utoaji wa elimu ya ushirika kwa ujumla na ile ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) kwa kutoa mafunzo katika ujasiriamali na uongozi, utunzaji wa vitabu vya hesabu na uendeshaji wa aina mbalimbali za vyama vya ushirika, ambapo jumla ya wanaushirika na wajasiriamali 18,207 [wanawake 7,112 (39%)] walipata mafunzo haya katika vituo vya mikoani;

(g) Kiliendesha semina na warsha kwa wanafunzi, wafanyakazi na jamii kwa ujumla ili kuimarisha masuala mtambuka na kuyaingiza kwenye mitaala ya chuo katika ngazi mbalimbali;

(h) Kiliendelea kutekeleza masharti yaliyotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu ili kujitayarisha kuwa Chuo Kikuu kamili (Fully Fledged University) kwa: kugharimia mafunzo ya wanataaluma katika ngazi mbalimbali, kukarabati majengo ya mihadhara na ofisi za wanataaluma na kuimarisha miundombinu ya maktaba kwa kuifanya iendeshwe kwa kutumia kompyuta (computarization of library services), kufunga mtambo wa ulinzi; na

(i) ilikamilisha Mpango Mkakati wa Chuo kwa mwaka 2010/2011 - 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina majukumu ya kufundisha kwa njia ya masafa na ana kwa ana, kutafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu na kueneza maarifa kupitia vituo vyaChuo vilivyopo mikoani. Katika kipindi cha 2005 – 2010, chuo kilitoa wahitimu 1,341 (wanawake 521) wa Vyeti, Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania:-

(a) Kilidahili jumla wanafunzi 7,882 wa mwaka wa kwanza (wanawake 2,756) wakiwemo wanafunzi 4,229 wa shahada za kwanza, 1,782 wa shahada za juu na 1,871 wa Cheti na Stashahada na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi wote waliopo chuoni kufikia 30,066 (wanawake 7,922). Aidha, kati yao waliodahiliwa katika programu za ualimu walikuwa 1,810 (880 wa Shahada ya Kwanza, 433 wa Stashahada za Uzamili na 497 wa Diploma ya Ualimu);

(b) Kilikamilisha ukarabati wa majengo ya vituo vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania vya Kilimanjaro, Njombe, Tanga, Dodoma na Mbeya;

(c) Kilifanikiwa kupata umiliki wa majengo ya iliyokuwa Rukwa Regional Transport Co-operation Limited;

(d) Kilikamilisha ujenzi wa Jengo la Miliki, ghala, vyoo vya nje, jukwaa la muda (podium), na uzio kuzunguka eneo lililojengwa, viwanja vya michezo, mfumo wa kuvuna maji, makaravati ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi na katika barabara ya eneo lililojengwa katika makao makuu ya chuo; na

(e) Kilianzisha majadiliano kuhusu uanzishaji wa vituo vya Chuo Kikuu Huria nchini Rwanda na Uganda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Ardhi kina jukumu la kufundisha, kutafiti na kutoa ushauri na huduma za kitaalamu katika nyanja mbalimbali zikiwemo za maeneo ya ardhi, mazingira na ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Chuo Kikuu Ardhi:-

(a) Kilidahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza 807 wa Shahada za Kwanza, wanafunzi 10 wa Stashahada na 68 wa Shahada za Uzamili na Uzamivu. Jumla ya wanafunzi wote walioko chuoni ni 2,143 ikilinganishwa na wanafunzi 1,701 waliokuwepo chuoni mwaka wa masomo 2008/09. Hili ni ongezeko la asilimia 26. Idadi ya wanafunzi wa kike ni asilimia 24 ya wanafunzi wote;

(b) Kilikamilisha utayarishaji wa maandiko sita (6) ya miongozo na taratibu za uendeshaji wa Chuo. Maandiko mengine 23 yako katika hatua mbalimbali za uandaaji;

(c) Kiliajiri wafanyakazi wapya 108. Kati ya hao, 51 ni wahadhiri na 57 ni waendeshaji;
(d) Kiligharimia mafunzo ya wafanyakazi wanataaluma 62 na waendeshaji 45 katika ngazi mbalimbali;

(e) Kiliendelea kufanya utafiti katika maeneo 63, kukamilisha utafiti katika maeneo 11 na kutoa machapisho 19;

(f) Kilianzisha programu mpya tano, ambapo mbili ni za Shahada ya Kwanza, mbili ni za Uzamivu na moja ni ya Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma);

(g) Kilikamilisha awamu ya pili ya kuweka huduma ya Intaneti katika majengo yasiyo na huduma hii ili kukuza matumizi ya TEHAMA Chuoni;

(h) Kiliendelea na ukarabati wa hosteli za wanafunzi, kumbi za mihadhara, ukumbi wa mikutano, nyumba za wafanyakazi, ofisi za wafanyakazi na ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua;

(i) Kilinunua vifaa vya TEHAMA pamoja na kupokea machapisho 512 kupitia miradi ya Benki ya Dunia na Carnegie Corporation; na

(j) Kilikamilisha awamu ya tatu ya ujenzi wa jengo jipya la mihadhara na ofisi (Lands Building) kwa kutumia fedha kutoka Serikalini na mkopo kutoka Mamalaka ya Elimu Tanzania (TEA).


Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kina majukumu ya kufundisha, kutafiti, kutibu na kutoa ushauri na huduma za kitaalam katika maeneo ya tiba na afya. Katika kipindi cha 2005 hadi 2010, chuo kilitoa wahitimu 1,377 wa Shahada ya Kwanza na 238 wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu. Kati ya hawa, Madaktari wa Shahada ya Kwanza walikuwa 807, wafamasia 232 na Madaktari wa meno 121.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2009/10 Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili:-


(a) Kilidahili wanafunzi wapya 342 wa shahada ya kwanza katika fani mbalimbali. Hii ni sawa na asilimia 97.7% ya lengo lililowekwa la wanafunzi 350. Pamoja na udahili huu, idadi ya wanafunzi wa shahada ya kwanza Chuoni ilikuwa 1,370;
(b) Kilitoa wahitimu wa shahada ya kwanza 282 katika fani za tiba (177), meno (28), famasia (34), uuguzi (25) na afya ya jamii na mazingira (18) na wahitimu wa uzamili na uzamifu 73;

(c) Kilikamilisha uwekaji wa samani na umeme kwa majengo mapya ya ofisi, maktaba na kumbi za mihadhara;

(d) Kilikamilisha tathmini na kuwalipa fidia jumla ya wakazi 1,919 wa eneo linalotarajiwa kutumika kwa upanuzi wa Chuo la Mloganzila, Kwembe na Kisokwa wanaostahili kulipwa fidia ya mali zao kwa gharama ya Sh. 8,067,904,700;

(e) Kiliajiri watumishi 37 kati ya 67 waliokuwa wamelengwa ambao wanajumuisha idadi ya watumishi Chuoni kufikia 587;

(f) Kiliongeza programu tano za uzamili na uzamivu kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa watu wenye sifa zinazohitajika, pamoja na waalimu wa kufundisha Chuoni na katika vyuo vikuu vya Afya na Sayansi Shirikishi nchini. Ongezeko hili linafanya jumla ya programu za uzamili na uzamivu Chuoni kuwa 46;

(g) Kimekamilisha ujenzi wa kantini katika eneo la hosteli za Chole ambapo mkandarasi anamalizia kazi ya kufunga majiko ya gesi; baada ya kukamilisha uwekaji wa samani, kantini itakuwa tayari kwa kuanza kuhudumia wanafunzi mia sita (600);

(h) Kilikamilisha ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo la hosteli za Chole pamoja na kibanda cha walinzi;

(i) Kilikamilisha utafiti kuhusu upatikanaji wa kipimo cha kugundua vijidudu vya malaria kwa haraka (Rapid Malaria Diagnostic Test) na matokeo yake kutumiwa na Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria katika kutengeneza sera za kutibu malaria nchini;

(j) Kilianza utafiti wa kuchunguza vinasaba vya vijidudu vya malaria kwa lengo la kubaini viashiria vya usugu kwa dawa mbalimbali za malaria;


(k) Kilijenga uwezo wa ufuatiliaji wa wagonjwa wanaopata dawa bora dhidi ya malaria;
(l) Kiliendelea kutengeneza mfumo wa takwimu (Data base) kwa ajili ya akinamama wajawazito uliosaidia kuimarisha utoaji wa huduma na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito. Aidha, utafiti huu uliainisha mikakati ya kupambana na ubakaji wa akina mama na watoto;

(m) Kilitoa mafunzo ya stadi za maisha kuhusu kutambua viashiria hatari kwa maisha ya mama na watoto na kuhusu hatua zinazostahili, umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya; kufuata utaratibu wa rufaa na kutafuta huduma endapo athari zinatokea;


(n) Kilikamilisha uchunguzi wa chanjo ya kifua kikuu (Mycobacteria vaccae vaccine) kwa watu wenye virusi vya UKIMWI (VVU) ili kubaini kama inaweza kupunguza uwezekano wa kupata TB kama ugonjwa nyemelezi. Matokeo yalionesha kuwa chanjo hiyo inatoa kinga dhidi ya kifua kikuu kwa asilimia 40 ya wagonjwa wenye VVU. Matokeo haya yameleta hamasa kubwa sana kwa watafiti duniani kuendeleza utafiti huo zaidi kwa madhumuni ya kupata chanjo dhidi ya TB kwa watu wenye VVU;

(o) Kiliendeleza utafiti wa chanjo ya UKIMWI kwa awamu ya kwanza na ya pili (Clinical Trial of HIV Vaccine Phase I & II), ambapo jumla ya watu sitini kutoka Jeshi la Polisi walijitolea kuchanjwa, na matokeo kuonyesha kuwa chanjo hii ni salama na yenye uwezo mkubwa wa kuchochea utengenezaji wa viashiria vya kinga ya mwili dhidi ya Virusi vya UKIMWI. Aidha, Chuo kilipata ufadhili wa kuendeleza utafiti wa chanjo hiyo kwa kina zaidi kwa ushirikiano kati ya Tanzania, Msumbiji, Ujerumani, Sweden, Uingereza na Amerika, ukiongozwa na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili; na

(p) Kilifanikisha machapisho 150 katika majarida ya Kimataifa na ndani ya nchi kutokana na utafiti uliofanywa na chuo katika maeneo mbalimbali.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu Mzumbe kina majukumu ya kupata, kukuza, kuhifadhi na kueneza maarifa na stadi za menejimenti kwa njia ya mafunzo, utafiti na huduma za kiufundi na kitaalamu. Chuo kimeongeza udahili kutoka wanafunzi 3,210 (wanawake 1,1210) mwaka 2005, hadi 5,172 (wanawake 2,239) mwaka 2010.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/10, Chuo Kikuu Mzumbe:-

(a) Kilidahili wanachuo wapya 3,206 (1,362 wanawake), kwa mwaka wa masomo 2009/10, ambapo, 1,577 walikuwa wa shahada ya kwanza, diploma na cheti, na 1,629 walikuwa wa shahada za uzamili, na hivyo kuvuka lengo la 2,310 kwa asilimia 39. Aidha, idadi ya wanachuo wote iliongezeka kutoka 3,537 mwaka 2007/08 hadi 5,210 mwaka 2009/10 Idadi hii ni sawa na asilimia 109 ya lengo la wanafunzi 4,773 waliokuwa wamepangwa kufikiwa mwaka huu wa masomo;

(b) Kilikamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa kike inayotarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 400 kwa wakati moja, katika Kampasi Kuu Mzumbe, ambapo wanachuo 200 tayari wanaishi humo;

(c) Kilikamilisha asilimia 85 ya ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la ofisi, litakalotosheleza wahadhiri 271 na wafanyakazi waendeshaji 127 ambapo tayari limeezekwa na upigaji lipu na uwekaji wa miundombinu ya umeme na mawasiliano unaendelea;

(d) Kilikamilisha michoro ya maktaba na kuendelea na taratibu za kumpata mkandarasi;

(e) Kililipia Sh. Milioni 750 (50%) kati ya Sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya vitalu vitatu vilivyopo Upanga Dar es Salaam kwa ajili ya upanuzi wa Shule Kuu ya Biashara Kampasi ya Dar es Salaam;

(f) Kiligharimia mafunzo kwa watumishi 25 ambapo wahadhiri walikuwa 20 (sita Uzamivu na 14 Uzamili) na wafanyakazi waendeshaji 10 (watano shahada za Uzamili, wawili shahada ya kwanza, wawili stashahada, na mmoja cheti);

(g) Kilikamilisha tafiti 20 kati ya 30 na kutoa ushauri katika maeneo 35 ya menejimenti, uongozi na Sayansi ya Jamii kwa ujumla;

(h) Kilichapisha vitabu viwil na makala 26 za kufundishia ambapo makala nane zilichapishwa katika majarida ya kimataifa; na

(i) Kiliajiri wahadhiri 23 kati ya 37 waliolengwa na waendeshaji 10 na kufikisha idadi ya wahadhiri 284 na waendeshaji 315 chuoni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo Kikuu cha Dodoma kinatekeleza majukumu yake ya kutoa mafunzo ya Shahada za Kwanza na za Juu, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika nyanja za Ualimu, Hisabati, Sanaa na Lugha, Sayansi za Jamii, Sayansi za Kompyuta, Tiba na Uuguzi, na Sayansi Asili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Chuo Kikuu Dodoma:-

(a) Kilidahili wanafunzi wapya 7,946 na kufanya idadi ya wanafunzi wote chuoni kuwa 15,121;

(b) Kiliongeza nafasi za udahili kwa kuanzisha Shule Kikuu ya Sayansi za Kompyuta na Habari, Sanaa na Sayansi za Jamii, Sayansi ya Tiba na Uuguzi, Sayansi za Ardhi, Hisabati na Sayansi Asili;

(c) Kiliajiri wafanyakazi wapya 676 na kufanya jumla ya wafanyakazi kuwa 978; na

(d) Kilikamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza ya Chuo cha Elimu chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 10,000; awamu ya kwanza ya Chuo cha Sayansi za Kompyuta, Habari na mawasiliano kwa asilimia 50%; jengo la utawala kwa asilimia 90, barabara zinazozunguka na kuunganisha kwa ndani kwa kiwango cha changarawe na lami kwa asilimia 85; awamu ya kwanza ya Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii kwa wanafunzi 5,000, na awamu ya kwanza ya Chuo cha Sayansi za Afya na Tiba kwa wanafunzi 500. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kina majukumu ya kuendesha mafunzo katika fani za Sayansi za Jamii kwa kiwango cha Cheti, Stashahada na Shahada; kutoa Mafunzo ya Uongozi na kufanya Utafiti na kutoa Ushauri wa Kitaalamu kwa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere:-

(a) Kilidahili wanafunzi wapya 238 wa ngazi ya cheti, 332 wa Stashahada na 313 wa Shahada ya Kwanza;

(b) Kiliajiri wanataaluma wanne na wafanyakazi waendeshaji watatu;
(c) Kiligharimia mafunzo ya wanataaluma 15 (10 uzamili na watano Uzamivu) na wafanyakazi waendeshaji watano;

(d) Kilikarabati Mabweni ya Mwongozo na Azimio;

(e) Kilijenga uzio kuzunguka eneo lote la Chuo - Kivukoni; na

(f) Kilianza awamu ya kwanza ya ujenzi wa kumbi tatu za mihadhara, ofisi za wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji eneo la Bububu, Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Ufundi Arusha kina jukumu la kutoa elimu na mafunzo ya ufundi katika fani za Magari, Ujenzi, Mitambo, Umeme, Barabara, Sayansi na Teknolojia ya Maabara, Eletroniki na Mawasiliano ya Anga kwa kiwango cha Cheti na Stashahada. Aidha, Chuo hufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika maeneo yake ya taaluma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2009/2010, Chuo cha Ufundi Arusha:-

(a) Kilidahili wanafunzi wapya 217 (23 wa kike) na kuvuka lengo la udahili la 205 kwa asilimia sita. Aidha, mwezi Januari 2010 chuo kilidahili wanafunzi 150 wa programu za mafunzo ya ufundi mchundo/stadi (Vocational Education and Training);

(b) Kilianzisha programu mpya ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara iliyokuwa na wanafunzi 23 (5 wa kike);

(c) Kilinunua vifaa vya maabara na kuunda Kamati ya Wanataaluma ya kuhakiki ubora pamoja na uwezekano wa kukarabati vifaa na zana za kufundishia na kuandaa mpango mkakati wa kuinua ubora wa mafunzo kwa vitendo na teknolojia chuoni;

(d) Kilikarabati nyumba mbili za wafanyakazi na kumteua mshauri mwelekezi wa kukarabati bweni na nyumba nyingine za wafanyakazi;

(e) Kilianza mpango wa kukuza elimu ya kujiendeleza kwa kutoa mafunzo ya stashahada kwa njia ya masomo ya jioni, ambapo jumla ya wanafunzi 21 walidahiliwa (Uhandisi Umeme sita, Uhandisi Elektroniki na Mawasiliano ya Anga 15);
(f) Kilikamilisha ujenzi wa maabara za Kemia, Fizikia na Biolojia;

(g) Kiliandaa kozi ya awali kwa ajili ya kuwawezesha wanachuo wa kike kujiunga na Chuo;

(h) Kiligharimia mafunzo ya wanataaluma na waendeshaji 17 katika Vyuo na Taasisi mbalimbali katika ngazi ya Uzamivu (5), Uzamili (4), Shahada ya Kwanza (6) na Diploma (2). Aidha, chuo kilipeleka wanataaluma watano katika mafunzo ya muda mfupi ya Automation and Variable Speed Drives kwa kushirikiana na Kilimanjaro Institute of Telecommuniation and Electronics and Computers (KIITEC);

(i) Kiliandaa mitaala mitatu NTAs 4 -6 ya Programu ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara ambayo tayari imeanza kutumika;

(j) Kiliandaa mitaala miwili ya Shahada ya Kwanza ya Uhandisi Ujenzi na Umwagiliaji na kuiwasilisha kwa wadau pamoja na Bodi ya Chuo; na

(k) Kiliimarisha ushirikiano na nchi wahisani, Mashirika ya Kimataifa, Vyuo vya Elimu ya Juu na vya Ufundi vilivyo nchini na vya Kimataifa kama ifuatavyo:-


- Mpango wa Elimu ya Ajira (Education for Employment – EFE) unaofadhiliwa na serikali ya Kanada, Chuo kinashirikiana na Chuo cha Camosun (Camosun Community College) cha Canada chini ya uratibu wa The Association of Canadian Community Colleges (ACCC) katika kuandaa mitaala ya kozi za Mining and Mineral Processing, Heavy Duty Equipment Technology na Lapidary and Jewellery Technology ngazi ya cheti na Stashahada ambayo itakamilika katika mwaka wa masomo wa 2010/2011;

- Ushirikiano na Vyuo vya Ufundi barani Afrika chini ya utaratibu wa Commonwealth Association of Polytechnics in Africa (CAPA);

- utafiti wa Mahitaji ya Soko (Labour Market Survey) la wahandisi wa Ujenzi na Umwagiliaji, ambao ulikiwezesha Chuo kuandaa mitaala kwa ajili ya kuanzisha Programu ya Shahada ya Kwanza ya Ujenzi na Umwagiliaji;
- Uimarishaji na usajili wa kitengo cha Uzalishaji na Utoaji Ushauri wa Kitaalamu (ATC – Production and Consultancy Bureau) kwenyeBodi ya Usajili wa Wahandisi;

- Kilitoa msaada wa Sh. 1,000,000 kwa watoto yatima na watu wenye UKIMWI kupitia Kikundi cha Upendo cha Chuo cha Ufundi Arusha; na

- Ununuzi wa vitabu vyenye thamani ya Sh. 16,000,000 kwa ajili ya programu za Sayansi na Teknolojia ya Maabara, na Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, na msaada wa vitabu 610 kutoka Tanzania National Parks (TANAPA).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Changamoto:-

(a) Kiwango cha chini cha ufaulu katika masomo ya Hisabati Sayansi na Kiingereza katika ngazi zote za elimu hususan Elimu ya Msingi na Sekondari;

(b) Kushuka kwa Net Enrolment Ratio (NER) katika elimu ya msingi kutoka 97.2 mwaka 2008 hadi 95.9 mwaka 2009;

(c) Pamoja na kusomesha walimu wengi, bado kuna uhaba wa walimu hususan katika maeneo ya pembezoni kutokana na mazingira magumu ya kufanyia kazi;

(d) Kiwango kidogo cha uandikishaji wa watoto katika elimu ya awali;

(e) Kushuka kwa uandikishaji wa watoto wenye mahitaji maalumu ya kielimu katika ngazi ya Elimu ya Msingi kutoka 7,241 mwaka 2008 hadi 5,532 mwaka 2009;

(f) Uhaba wa maabara za masomo ya sayansi katika Elimu ya Sekondari na vyuo vya ualimu;

(g) Upungufu wa vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia katika Elimu ya Sekondari na Elimu ya Juu;

(h) Upungufu na uchakavu wa miundombinu katika Elimu ya Juu, Shule Kongwe za sekondari na vyuo vya ualimu;

(i) Mahitaji makubwa ya rasilimali katika kuviwezesha vyuo vya ualimu kutumia TEHAMA;
(j) Idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sayansi katika ngazi zote za elimu na mafunzo;

(k) Kuongezeka idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaohitaji mikopo kutoendana na uwezo wa Serikali wa kutoa mikopo hiyo;

(l) Uhaba wa walimu, wakufunzi na wahadhiri; na

(m) Kuongeza udahili wa wanafunzi katika elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kutoa mafundi wa ngazi za kati watakaoinua uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu malengo na bajeti ya mwaka 2010/1. Katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa malengo ya mwaka 2009/2010, Wizara itatekeleza yafuatayo katika mwaka 2010/2011.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Kamishna wa Elimu. Katika mwaka 2010/2011, Ofisi ya Kamishna:-

(a) Kuimarisha utoaji elimu kwa usawa kwa kuandaa mwongozo wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Elimu Jumuishi;

(b) Kutoa elimu kwa umma inayohusu uzuiaji wa mimba za utotoni kwa wanafunzi;

(c) Kufanya uchaguzi wa wanafunzi wenye ulemavu kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2011 na kununua na kusambaza vifaa maalum vya kufundishia na kujifunzia na visaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum;

(d) Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa utoaji wa Elimu Maalum/Jumuishi katika Halmashauri 16 za Mikoa ya Manyara, Arusha, Lindi na Mtwara;

(e) Kutayarisha na kutangaza vipindi 580 vya masomo kwa njia ya redio (Sayansi, Kiingereza na Kiswahili Darasa la V – VII; Historia, Jiografia na Uraia kwa Darasa la III – VII), na 52 vya Boresha Elimu na Ufundishaji kwa Kutumia Njia Shirikishi;

(f) Kufuatilia utekelezaji wa masharti ya usajili wa shule katika mikoa 10 (Arusha, Dodoma, Tabora, Tanga, Mbeya, Mwanza, Iringa, Morogoro, Pwani na Mtwara);
(g) Kukamilisha uandishi wa taarifa ya matokeo ya Utafiti wa Kimataifa kuhusu Ubora wa Elimu ya Msingi katika Nchi 15 za Kusini na Mashariki ya Afrika (SACMEQ Research Project III) na kuisambaza kwa wadau; na

(h) Kuandaa rasimu ya uanzishwaji wa Bodi ya Weledi ya Walimu (Teachers Professional Board).


Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Msingi. Mwaka 2010/11, kazi kubwa za Idara ya Elimu ya Msingi zitakuwa:-

(a) Kutathmini utekelezaji wa MMEM Awamu ya II kwa ajili ya kuandaa MMEM Awamu ya III;

(b) Kufuatilia na kutathmini matumizi ya fedha za MMEM II na utekelezaji wa malengo yake ikiwa ni sehemu ya mapitio ya Sekta ya elimu;

(c) Kufanya utafiti na kuainisha njia mbalimbali za kuongeza uandikishaji na mahudhurio katika shule za awali;

(d) Kuandikisha watoto 2,043,984 wa Elimu ya Awali na 1,383,752 wa Elimu ya Msingi;

(e) Kuandaa miongozo ya ufuatiliaji na tathmini ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na upimaji wa utoaji wa elimu ya awali pamoja na kuwajengea uwezo wadau 142 wa malezi/makuzi na maendeleo ya mtoto katika Halmashauri 5;

(f) Kufuatilia uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na wa darasa la kwanza mwaka 2011;

(g) Kuinua ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia na utoaji wa elimu kwa usawa kwa kuendelea kugharimia ujenzi wa Shule ya Msingi Monduli Jeshini (Sokoine Cantonment) na kukarabati Shule ya Msingi Arusha;


(h) Kuratibu na kufuatilia Mpango wa Lishe Shuleni katika Halmashauri 16 zinazofadhiliwa na WFP, kukamilisha uandaaji wa Mpango wa Kitaifa wa Lishe shuleni na mradi wa ufundishaji kwa kutumia TEHAMA wa Bridge IT;
(i) Kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwaandikisha watoto katika shule za awali ili wawe tayari kuanza Darasa la Kwanza na kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu;

(j) Kuwajengea uwezo walimu kupitia walimu mahiri 3,000 watakaobainishwa ili kuinua kiwango cha ufundishaji wa masomo ya Hisabati, Sayansi na Lugha; Aidha, katika mwaka 2010/11 majaribio yataanza kutumia vitabu vya New Oxford English Course for Schools ili kuimarisha lugha ya Kiingereza shuleni;

(k) Kugharimia mafunzo kwa wasimamizi wa elimu ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa;

(l) Kuimarisha mtaala ili uzingatie umahiri wa mwanafunzi na mahitaji ya soko la ajira (Competence Based Curriculum)

(m) Kuwajengea uwezo wasimamizi wa elimu 200 wa ngazi mbalimbali, wakiwemo Maafisa Elimu wapya katika usimamizi na, uendeshaji wa Elimu ya Msingi;

(n) Kuratibu uandaaji na uendeshaji wa mitihani ya Taifa ya Darasa la IV na VII; na

(o) kutafuta wadhamini wa michezo na kuanza kuhamasisha michezo katika Elimu ya Msingi;

Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Sekondari katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES), mwaka 2010/2011, Wizara itatekeleza awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES II) kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI. Mradi wa MMES II unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2010/2011 – 2014/2015 kwa mkopo wa dola za Marekani 470 milioni. Chini ya mpango huu, shule zitapatiwa ruzuku ya kununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kujenga maabara na nyumba za walimu, kuwajengea uwezo walimu wa sayansi, hisabati na lugha ya kiingereza. Katika mwaka huu wa fedha mradi huo umetengewa kiasi cha shilingi 150 bilioni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa awamu ya pili ya MMES unategemea kuinua ufaulu katika elimu ya sekondari hususan katika masomo ya Sayansi, Hisabati na lugha za Kiingereza na Kiswahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na utekelezaji wa malengo yaliyotajwa awali, Wizara itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kupunguza uhaba wa walimu kwa kuanza mradi wa Tanzania Beyond Tomorrow kwa majaribio (TestPhase). Mradi huo unahusu kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa kutumia TEHAMA katika shule 500 za awamu ya kwanza; na

(b) Kufuatilia utekelezaji wa ugatuaji wa uendeshaji wa shule za Sekondari katika Halmashauri za Wilaya, ikiwa ni pamoja na kutoa na kuratibu utekelezaji wa miongozo mbalimbali kwa kushirikiana na OWM-TAMISEMI.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya Elimu ya Ualimu. Katika mwaka 2010/2011, Idara ya Elimu ya Ualimu itatekeleza yafuatayo:-


(a) Kuwapangia vituo vya kazi walimu 14,501 wa Shule za Msingi wanaohitimu sasa katika vyuo vya ualimu vya umma na vile vya binafsi. Aidha, Idara itawapangia kazi walimu 17,204 (7,084 wa Diploma na 12,120 wa Shahada ya Kwanza) katika shule za serikali. Mafanikio haya makubwa yataiwezesha Serikali kupeleka angalau walimu watano katika kila Shule ya Sekondari nchini;

(b) Kudahili walimu wanafunzi 4,550 wa ngazi ya Cheti Daraja A, 5,055 wa Stashahada na 320 wa fani maalumu za Michezo, Muziki, Sanaa za Maonesho/Ufundi, Elimu Maalumu ya Sayansi Kimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali;

(c) Kuendeleza juhudi za matumizi ya TEHAMA katika kufundisha na kujifunza, ikiwa ni pamoja na kuendesha mafunzo ya ndani vyuoni (in –house training) na kufanya mazunguzo na wahisani wenye nia ya kusaidia juhudi za matumizi ya TEHAMA;

(d) Kuratibu utoaji wa elimu ya michezo kwa kuanza na vyuo vya ualimu 12 kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali liitwalo Liike la Finland;

(e) Kutayarisha mwongozo wa vigezo vya ubora wa walimu (Teacher Competency Framework) pamoja na kuendesha mafunzo ya walimu kazini kwa walimu 700 wa shule za msingi katika Halmashauri saba za majaribio (Mtwara (V), Makete, Bagamoyo, Temeke, Hai, Siha na Magu) kwa kushirikiana na UNICEF;
(f) Kuwajengea uwezo wa wakufunzi 240 kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi, Elimu ya UKIMWI, na Stadi za Maisha kwa kushirikiana na UNESCO ili kuinua kiwango chao cha kukabiliana na athari zitokanazo na magonjwa hatarishi kama vile UKIMWI, mimba zisizotakiwa, na mahusiano yasiyofaa;

(g) Kuimarisha mafunzo ya ualimu ili kuhakikisha wahitimu wa ualimu katika ngazi ya cheti na Diploma wanafikia viwango stahili katika hisabati na lugha ya Kiingerza ili kuimarisha taaluma;

(h) Kuendesha mafunzo ya mbinu za Ufundishaji Bainifu na Elimu ya UKIMWI kwa Wakufunzi 36, walimu wa Shule za Msingi 190 na walimu wa Shule za Sekondari 40 wa Mkoa wa Kigoma chini ya mpango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (OneUN-Joint Programme North Western Tanzania: Transition from Humanitarian to SustainableDevelopment); na

(i) Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kifaransa kupitia mradi wa mafunzo kazini, kwa walimu wa Kifaransa 160 wa Shule za Sekondari na 240 wa Shule za Msingi, kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ufaransa.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi itaanza utekelezaji wa Mpango kabambe wa Kisomo kwa wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Mpango huu ulioanza kwa majaribio katika Wilaya tisa sasa utasambazwa nchi nzima chini ya kauli mbiu ya “Ndiyo Ninaweza”. Pamoja na hayo, Idara itafanya yafuatayo:-


(a) Kuwezesha uandaaji, ununuzi na usambazaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya wanakisomo kwa ajili ya programu ya Ndiyo Ninaweza;

(b) Kuratibu mafunzo ya wasimamizi 45 na wawezeshaji 360 wanaofundisha kisomo kwenye Halmashauri tisa za majaribio ya Mpango wa Ndiyo Ninaweza;


(c) Kufanya ufuatiliaji na tathmini katika Halmashauri tisa (9) zinazotekeleza programu ya Ndiyo Ninaweza ili kubainisha mafanikio na changamoto zilizojitokeza;
(d) Kuandaa, kuchapisha na kusambaza vitabu 450 vya wanakisomo (nukta nundu na maandishi makubwa), vitabu 60 vya wawezeshaji na miongozo ya wasimamizi kwa ajili ya programu ya Ndiyo Ninaweza;

(e) Kuandaa Mwongozo wa Uanzishaji na Usimamizi wa Mafunzo ya Elimu Masafa na Ana kwa Ana;

(f) Kuratibu utafiti wa kisomo ili kubaini hali halisi ya kiwango cha kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kushirikiana na UNESCO;

(g) Kuandaa Mpango Mkakati wa Elimu juu ya Haki za Binadamu; na

(h) Kuratibu uaandaaji na Uchapishaji wa Magazeti Vijijini na makala nyingine katika vituo vya Kanda.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Idara ya katika mwaka 2010/11, Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi SEADI itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kukamilisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (MMEU);

(b) Kuendelea kutangaza na kuhamasisha vijana kujiunga na elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kupitia maonesho na vyombo mbalimbali vya habari, na kutembelea Shule za Sekondari;

(c) Kuendeleza mpango wa ujenzi wa Vyuo 28 vya VETA vya Wilaya na kukamilisha ujenzi wa Vyuo vya VETA vya Mikoa ya Pwani, Manyara, Lindi na Dar es Salaam;

(d) Kuendelea kuratibu uandaaji wa Bridging Course ya kuwapa sifa wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi kujiunga na mafunzo ya ufundi sanifu;

(e) Kugharimia mafunzo ya vitendo viwandani kwa wanafunzi 700 wa Chuo cha Ufundi Arusha; na

(f) Kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa katika masuala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011 Idara ya Elimu ya Juu itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kukamilisha uandaaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJU) na kuanza utekelezaji wake;

(b) Kugharimia mafunzo ya wanafunzi 1,750 wa Shahada ya Kwanza ya Udaktari, Udaktari wa Meno na Tiba ya Mifugo katika vyuo vikuu vya ndani;

(c) Kugharimia mafunzo kwa wanafunzi 70 raia wa Uganda na watano wa China katika utaratibu wa kubadilishana wanafunzi wa shahada ya kwanza;

(d) Kuendelea kuelimisha umma kuhusu dhana ya uchangiaji wa gharama za Elimu ya Juu na fursa za Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari, maonesho ya taasisi za Elimu ya Juu na kwa kutembelea wadau wa elimu;


(e) Kugharimia mafunzo ya Shahada za Uzamili na Uzamivu kwa wanataaluma 80 wa Vyuo Vikuu vya Umma;

(f) Kuratibu uteuzi wa wanafunzi 270 kwa nafasi zinazotolewa na nchi rafiki ambazo ni Algeria, China, Cuba, Urusi, Uingereza, Korea Kusini, Uturuki, Misri na India na 50 wa wanaokwenda kusoma Msumbiji kwa makubaliano ya kubadilishana wanafunzi;


(g) Kuanza kujenga hospitali ya kufundishia (University Teaching Hospital) katika eneo la Mloganzila kwa ajili ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili;

(h) Kuendelea kuratibu utekelezaji wa mradi wa Science, Technology and Higher Education unaodhaminiwa na Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia, unaolenga kusomesha na kuimarisha ufundishaji wa Sayansi na Teknolojia katika Elimu ya Juu; na


(i) Kushirikiana na Taasisi zingine katika kugharimia ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wenye ulemavu katika vyuo vikuu nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Idara ya Ukaguzi wa Shule itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kusimamia ubora wa elimu itolewayo kwa kutumia utaratibu mpya wa ukaguzi wa shule kwa kukagua jumla ya asasi 20,045;

(b) Kuimarisha ukaguzi wa shule kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa kuwapatia usafiri, ukarabati wa ofisi, kuwajengea uwezo wakaguzi na kuwapatia stahili zao;

(c) Kuongeza ufanisi katika usimamizi wa elimu kwa kuteua na kutoa mafunzo ya awali kwa wakaguzi wa shule wapya 150;

(d) Kusimamia na kuendesha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili mwaka 2010; na

(e) Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa utaratibu mpya wa ukaguzi wa shule.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Idara ya Sera na Mipango itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kukamilisha na kuchapa nakala 500,000 za Sera ya Elimu na Mafunzo 2011 na kusambaza kwa wadau mbalimbali wa elimu na kuandaa mkakati wa utekelezaji;

(b) Kugharimia utafiti wa kutafuta gharama halisi ya kumsomesha mwanafunzi wa Elimu ya Juu (Unit Cost Study);

(c) Kuimarisha Mfumo wa Takwimu (Database) ya elimu katika Halmashauri 105 kwa kushirikiana na UNESCO kupitia programu ya ESMIS;


(d) Kuratibu shughuli za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu;

(e) Kuratibu maandalizi ya mpango mkakati wa utekelezaji wa TEHAMA kwa Wizara; na

(f) Kukarabati miundombinu ya vyuo vya ualimu 10.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuajiri watumishi wapya 290, kuidhinisha vibali vya ajira za wataalam wa kigeni 1,000, kuthibitisha kazini watumishi 55 na kupandisha vyeo watumishi 906;

(b) Kutekeleza Muundo mpya wa Wizara kwa lengo la kuimarisha utendaji; na

(c) Kuendelea kuratibu ulipaji madeni ya walimu na watumishi wasio walimu na kuweka mikakati ya kuepusha malimbikizo ya madeni hayo ili kuondoa usumbufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuratibu utoaji wa habari katika vyombo vya habari kuhusu matukio mbalimbali ya kielimu ili kufahamisha wadau wa Elimu kuhusu maendeleo ya sekta ya Elimu na kuweka kumbukumbu za Wizara;


(b) Kuandaa, kutengeneza, kuchapa na kusambaza nakala 300,000 za Jarida la EdSDP kwa Kanda nane za elimu ili kuihamasisha jamii kushiriki katika kutekeleza mipango ya Elimu;

(c) Kuandaa machapisho mbalimbali yakiwemo mabango, vipeperushi, vijarida na kalenda kwa ajili ya kuelezea sera na mipango mbalimbali ya maendeleo ya elimu kwa wadau;


(d) Kuratibu upatikanaji wa majibu ya maswali yanayoulizwa na wadau wa elimu kupitia Tovuti ya Wananchi (www.wananchi.go.tz); na

(e) Kutayarisha mkakati wa mawasiliano na habari unaohusu shughuli za Wizara.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala, Taasisi na Mabaraza yaliyo chini ya Wizara yangu yanafanikisha utoaji wa elimu bora. Wakala, Taasisi na Mabaraza yatatekeleza kazi zilizopangwa kwa kuzingatia malengo na mipango ya elimu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Katika mwaka 2010/2011, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi 420 ambapo, 150 ni wa ngazi ya Cheti, 140 wa Stashahada na 130 wa Shahada;

(b) kuandikisha jumla ya walengwa 75,000 kupitia mpango wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana;

(c) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika usimamizi wa taarifa za Elimu yaWatuWazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi;

(d) Kuratibu utekelezaji wa Programu ya majaribio ya Integrated Post-primary Education (IPPE) katika wilaya za Siha, Temeke, Magu, Makete, Mtwara Vijijini, Hai na Bagamoyo na kuandika masomo ya Ufundi na Masuala mtambuka ya programu hii katika mfumo wa moduli;

(e) Kuendelea kuwajengea uwezo wa kufundisha mtaala unaozingatia soko na matakwa ya NACTE wakufunzi na wahadhiri wa TEWW na Vyuo vilivyo chini ya NACTE;

(f) Kufanya tathmini ya kina ya programu zinazoendeshwa na TEWW pamoja na mpango wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana tangu ulipoanza mwaka 2004 hadi 2009;

(g) Kuandaa mitaala na kuandika moduli za masomo ya kidato cha tano na sita kwa masomo ya Economics, General Studies, Accounts na Applied Basic Mathematics kwa mfumo wa Elimu Masafa;

(h) Kuandaa moduli za mafunzo ya Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Endelevu kwa njia ya Elimu Masafa; na

(i) Kuendesha mafunzo ya elimu masafa na ana kwa ana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Taasisi ya Elimu Tanzania itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kutoa mafunzo elekezi juu ya mitaala iliyorekebishwa kwa walimu 1,650 wa sekondari;
(b) Kubuni na kuandaa mtaala wa mafunzo ya ualimu unaotumia TEHAMA;

(c) kugharimia mafunzo ya wakuza mitaala 55 juu ya kubuni, kutengeneza na kueneza maandishi ya kielimu yanayotumia TEHAMA;

(d) Kuchapisha moduli za masomo 17 kwa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na 26 kwa mafunzo ya Ualimu Cheti; na

(e) kuhariri muhtasari wa masomo ya mitaala ya elimu ya awali, msingi na sekondari ili kuingiza maoni ya wadau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuimarisha na kuinua ubora wa huduma za maktaba kwa watu wazima na watoto katika mikoa 19 ikiwa ni pamoja na kuongeza machapisho 60,000;

(b) Kutoa ushauri wa kitaaluma juu ya uanzishaji, upangaji na uendeshaji wa Maktaba za Shule, Vyuo, Taasisi na Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya nchini;

(c) Kutoa mafunzo ya Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka kwa walengwa 200 wa cheti; 220 wa stashahada na 180 wa mafunzo ya muda mfupi kwa wafanyakazi wa maktaba za shule, vyuo na taasisi mbalimbali nchini; na

(d) Kuendeleza ujenzi na kuimarisha Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka Bagamoyo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa hosteli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11. Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu utatekeleza yafuatayo:-

(a) Kutoa mafunzo ya Stashahada ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa viongozi 300 wa idara mbalimbali za elimu na Mashirika Yasiyo ya Serikali;

(b) Kutoa mafunzo ya mwezi mmoja ya Cheti cha Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi 500;
(c) Kutoa mafunzo ya mbinu za kuandaa Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule kwa Maafisa 2,000 katika ngazi ya Wilaya;

(d) Kutoa mafunzo ya mwezi mmoja ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa Wakuu wa Shule za Sekondari 240;

(e) Kutoa mafunzo ya awali ya Uongozi na Uendeshaji wa elimu kwa Wakuu Wapya wa Shule za Sekondari 1,000 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara;

(f) Kutoa mafunzo ya mwezi mmoja ya Uongozi na Uendeshaji wa elimu kwa Wakaguzi wa Shule 120;

(g) Kutoa mafunzo ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa Maafisa Elimu wapya 106 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara;

(h) Kugharimia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa wafanyakazi 16 wa Wakala ndani na nje ya nchi juu ya mbinu bora za ufundishaji, utafiti na ufuatiliaji wa mafunzo ya Uongozi na Uendeshaji wa Elimu;

(i) Kufanya utafiti wa kielimu kuhusu Uongozi na Uendeshaji wa Elimu katika Afrika Mashariki na Kusini mwa Africa chini ya mtandao wa Lead-link; na

(j) Kukamilisha Mpango Kabambe wa Maendeleo wa Wakala (Master Plan) na kuanza awamu ya kwanza ya utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Taifa ya UNESCO. Katika mwaka 2010/11, Tume ya Taifa ya UNESCO itatekeleza yafuatayo:-

(a) Itafanya tathmini ya miradi ya UNESCO inayoendelea chini ya programu inazowashirikisha watekelezaji yaani Participation Programme na mingine itakayoidhinishwa na UNESCO;

(b) Kuendelea kuratibu utekelezaji wa mpango kazi wa progamu ya Mwaka wa Kimataifa wa Sayari Dunia (International Year of the Planet Earth - IYPE);

(c) Kuendeleza ushirikiano na Tume za UNESCO za Afrika ya Mashariki chini ya Mpango wa pamoja wa ushirikiano kwa kuandaa na kutekeleza mipango ya kujenga uwezo wa wafanyakazi (capacity building), kufanya ziara za kielimu (Study Tours) na programu ya kubadilishana watumishi (Staff Exchange Programme); na

(d) Kuendelea kuratibu mtandao wa Shule za UNESCO (Associated School Project Network - ASPNET) na kuendelea kuelimisha wanafunzi katika shule hizo juu ya masuala mtambuka ya jinsia, haki za binadamu, stadi za maisha na mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Baraza la Mitihani la Tanzania litatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuendesha mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Sita, Maarifa (QT) na Ualimu; na

(b) Kuongeza ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa mitihani kwa kununua server yenye uwezo mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011 Kituo cha Maendeleo Dakawa kitatekeleza kazi zifuatazo:-

(a) Kuendelea na mchakato wa kukibadilisha kituo kuwa Centre of Excellence; katika kutoa elimu na utaalam wa Sayansi na Ufundi kwa vijana; na

(b) Kuratibu shughuli za maendeleo ya Taasisi zilizopo kwenye kituo.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Mamlaka ya Elimu Tanzania itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kutafuta rasilimalifedha kwa ajili ya Mfuko kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wa ndani na nje ya nchi na kutafuta ufadhili wa miradi;

(b) Kutoa ufadhili wa miradi 250 ya elimu kwa Taasisi za elimu 250 zinazolenga kusaidia kuongeza udahili, ubora na upatikanaji wa elimu kwa usawa;

(c) kukamilisha uandaaji wa rasimu ya marekebisho ya Sheria Na. 8 ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001; na
(b) Kuendelea kuhamasisha Halmashauri za Serikali za Mitaa kuanzisha Mifuko ya elimu na kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) na kuhamasisha uchangiaji wa mfuko wa elimu kupitia vipindi vya televisheni na redio, vipeperushi, majarida na vyombo vingine vya habari.


Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Katika mwaka 2010/2011, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kukamilisha zoezi la kuandaa kanuni za utekelezaji wa mfumo wa tuzo zinazotambuliwa Kitaifa (National Qualifications Framework);

(b) Kuendelea kuratibu na kutathmini mradi wa majaribio ya udhibiti wa ubora wa programu za vyuo vikuu vitano unaotekelezwa na Inter-University Council for East Africa (IUCEA); na

(c) Kuendelea kusimamia udahili wa wanafunzi wapatao 60,000 kwa kupitia mfumo wa udahili wa pamoja (Centralized Admission System) ili kuondoa tatizo la mwanafunzi mmoja kudahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja na hivyo kubana nafasi kwa wenye sifa kudahiliwa katika Taasisi za elimu ya juu nchini.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi litatekeleza yafuatayo:-


(a) Kukagua vyuo 25 kwa ajili ya kutoa ithibati, kusajili vyuo 20 vya ufundi na kubaini sifa za wakufunzi ili kuwasajili;

(b) Kuratibu na kuandaa mitaala 30 inayozingatia umahiri na mahitaji ya soko la ajira pamoja na kuratibu mitihani katika vyuo vinavyotumia mitaala hiyo;

(c) Kuratibu mitihani katika vyuo 30 vinavyotumia mitaala inayolenga katika kujenga umahiri wa mwanafunzi na mahitaji ya soko la ajira;

(d) Kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo 17 vinavyotoa mafunzo ya elimu ya juu ya ufundi; na
(e) Kuratibu mafunzo kwa wakufunzi katika vyuo 20 juu ya ufundishaji katika mfumo wa elimu unaozingatia kumwezesha mwanafunzi kuwa mahiri (Competence Based Education and Training –CBET).


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuongeza udahili kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi 89,617 wanaosoma ndani na nje ya nchi katika ngazi mbalimbali za elimu ya juu;

(b) Kuwahamasisha wanafunzi wengi zaidi kuchukua masomo ya sayansi kwa kuendelea kutoa mikopo kwa asilimia 100;

(c) Kuimarisha ukusanyaji wa marejesho ya mikopo kwa kuelimisha na kuhamasisha wadaiwa, waajiri na umma kwa ujumla juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo itolewayo na Bodi. Aidha, Bodi inatarajia kukusanya Sh. bilioni tano kama marejesho ya mikopo iliyotolewa;

(d) Kuendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali zikiwemo vipeperushi, magazeti, redio, televisheni, warsha na maonesho kuhusu wajibu wao wa kuchangia elimu ya juu na taratibu za utoaji mikopo na urejeshwaji wake;

(e) Kushirikiana na Wizara kujenga mfumo mbadala na endelevu wa utoaji wa mikopo ya Elimu ya Juu kwa kutumia Asasi za fedha ili kupanua wigo wa wanaostahili kupewa mikopo; na

(f) Kuboresha mfumo wa Means Testing ili kupunguza malalamiko na rufaa za wanafunzi kwa Waziri. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kutegemeza awamu ya kwanza ya Programu ya Vituo vya Ufundi Stadi vya Wilaya (District Vocational Training Centres Programme) kwa kujenga vituo sita vya ufundi stadi;
(b) Kujenga uwezo wa wakufunzi 30 na watumishi wa kawaida 315;

(c) Kuendelea kufanya utafiti katiti (Tracer Study) wa nchi nzima ili kubaini soko la elimu ya ufundi stadi;

(d) Kukarabati karakana za vituo vitatu vya ufundi stadi vya Mwanza, DSM na Kihonda na kujenga Ofisi za Kanda ya Kusini-Mashariki; Mtwara; na

(e) Kuendeleza ujenzi wa vituo vitano vya Ufundi Stadi - Lindi, Mtwara, Manyara, Pwani na Dar es Salaam na kuimarisha Vituo vya Ufundi Stadi vya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2010/2011, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 6,785 ambapo 4,125 ni wa shahada ya kwanza na 2,660 Shahada ya Uzamili na Uzamivu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa kike na wenye mahitaji maalum;

(b) Kuendeleza ushirikiano na wafadhili mbalimbali katika kugharimia utafiti na mafunzo, hasa katika nyanja za mazingira, ujasiriamali, nishati, utalii, sekta isiyo rasmi, TEHAMA, mabadiliko ya tabianchi, miundo mbinu, lugha, demokrasia, na utawala bora;

(c) Kutoa machapisho 19 ya vitabu na 280 majarida katika nyanja mbalimbali za utafiti;

(d) Kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya chuo ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;

(e) Kuendeleza ujenzi wa Makao Makuu mapya ya Taasisi ya Sayansi za Bahari eneo la Buyu, Zanzibar;

(f) Kuanzisha shahada nne (4) za kwanza (B.A. in Kiswahili, B.Sc. in Textile Engineering, B.Sc. in Textile Design and Technology na B.Sc. in Actuarial Science), shahada mbili za Uzamili (Masters in Intergrated Sanitation Management na MSc.in Biodiversity and Conservation) na shahada moja ya Uzamivu (PhD. by Coursework and Dissertation in Political Science and Public Administration);
(g) Kufanya ukaguzi wa kitaaluma katika Shule Kuu na Idara za kitaaluma (Academic Audit); na

(h) Kuajiri na kusomesha wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji kwenye fani mbalimbali.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11 Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kitatekeleza yafuatayo:-


(a) Kudahili wanafunzi wapya 1,000 (150 wa fani ya sayansi);

(b) Kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu;


(c) Kujenga kituo cha afya ili Chuo kiwe na uwezo wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa jamii ya Chuo Kikuu Kishiriki;

(d) Kuipatia maktaba ya chuo vitabu 1,000, majarida 200 na kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili kuinua ubora wa elimu inayotolewa; na

(e) Kugharimia mafunzo ya wanataaluma 10 katika ngazi ya Uzamili, watano wapya katika ngazi ya Uzamivu na sita wanaoendelea na mafunzo ya Shahada ya Uzamivu.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 800 wa shahada ya kwanza na kufanya idadi ya wanachuo kufikia 2,200;


(b) Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia; kuanza mchakato wa ujenzi wa jengo la utawala ili kuongeza nafasi za ofisi; na

(c) Kugharimia mafunzo ya wahadhiri 20 (wanne Uzamivu na16 Uzamili).
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanachuo wapya 195 (Shahada ya Kwanza 150, Stashahada ya Uzamili 15, Shahada ya Uzamili 10 na Cheti 20);

(b) Kuanzisha gazeti la wiki la mafunzo kwa wanachuo;

(c)Kufanya utafiti katika fani za uandishi wa habari, mawasiliano na utangazaji;

(d) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia; na

(e) Kujenga na kukarabati miundombinu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanachuo 2,304 wa shahada ya kwanza na 300 wa Uzamili na Uzamivu;


(b) Kujenga na kukarabati miundombinu ya chuo ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;

(c) Kuanzisha shahada mpya sita za kwanza na sita za Uzamili;

(d) Kuanza mradi wa uvunaji maji ya mvua kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji;


(e) Kuanzisha Taasisi ya Kitaifa ya Bioteknolojia yaKilimo (National Agricultural Biotechnology Institute) ili kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa Kilimo Kwanza; na


(f) Kufanya utafiti unaolenga kumwondolea umaskini mkulima, kukuza uchumi na kuboresha mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Elimu za Biashara Moshi cha Chuo Kikuu cha Sokoine kitatekeleza kazi zifuatazo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 1,500 wa mwaka wa kwanza ili kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 2,713 mwaka 2009/10 hadi 3,330 kwa Mwaka 2010/11. Ongezeko la udahili wa wanafunzi litatokana na kuanzishwa kwa kozi za cheti katika kampasi ya Kizumbi (Shinyanga);

(b) Kuendelea kugharimia mafunzo ya Wahadhiri 30 katika kiwango cha Shahada za Uzamili na Uzamivu;

(c) Kuimarisha matawi manne ya kanda, Mtwara, Iringa, Mwanza na Tanga ili kuielimisha jamii katika masuala ya Vyama vya Ushirika vya Akiba na mikopo (SACCOS), maendeleo ya ushirika, utunzaji mazingira, na mikakati ya kupunguza umaskini;

(d) Kukamilisha utekelezaji wa masharti yaliyotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu ili kukiwezesha Chuo kupanda daraja na kuwa Chuo Kikuu kamili ifikapo mwaka 2014;

(e) Kuendelea na ukarabati wa miundombinu ya chuo kwa ajili ya kuinua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia; na

(f) Kufanya utafiti juu ya vyama vya ushirika, SACCOS na utunzaji wa mazingira.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2010/11, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimejizatiti kutekeleza shughuli zifuatazo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 7,306 (wanawake 2,262). Kati ya hao, 2,238 ni wa Vyeti na Stashahada, 2,827 wa Shahada ya Kwanza na 2,241 ni wa Stashahada ya Uzamili na Shahada za Uzamili na Uzamivu. Aidha, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatarajia kutoa wahitimu 1,697, ambapo 1,257 watakuwa wa Shahada ya Kwanza, 112 Vyeti na Stashahada nyingine, 328 Stashahada ya Uzamili na Shahada za Uzamili na Uzamivu;

(b) Kujenga ofisi za vituo vya Mikoa ya Mtwara na Manyara;
(c) Kukarabati majengo kwa ajili ya kuinua ubora wa elimu na kutengeneza mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia katika kituo cha Mkoa wa Rukwa, Kagera, Kilimanjaro, Mara na Ruvuma;

(d) Kununua ardhi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika vituo vya mikoa; na

(e) Kujenga vituo vya Elimu Masafa (Afrika/ SADC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2010/2011, Chuo Kikuu Ardhi kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 1,350 wa Shahada ya kwanza, 75 wa Shahada za Uzamili na Uzamivu na 20 wa cheti. Jumla ya wanafunzi wote inalengwa kuwa 2,606, ambayo ni ongezeko la asilimia 21 ukilinganisha na mwaka 2009/10. Wanawake wanatarajiwa kuwa asilimia 30 ya wanafunzi wote;

(b) Kuanzisha programu mpya tatu (3) za shahada ya kwanza katika uhandisi-ujenzi (Civil Engineering), Fedha na Uhasibu (Finance and Accountancy); na Masoko (Marketing);

(c) Kugharimia mafunzo ya wahadhiri 25 wapya na wafanyakazi waendeshaji 20 wapya;

(d) Kukamilisha utafiti katika maeneo 15 kati ya 63 yanayoendelea; kutoa machapisho 25 na kutoa huduma za kitaalamu (Consultancies and Public Service) katika miradi 100; na

(e) Kujenga na kukarabati miundombinu ya chuo ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2010/11 Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya wa shahada ya kwanza 350 na wa shahada za uzamili na uzamivu 170;

(b) Kuanza matayarisho ya ujenzi wa majengo ya utawala, kumbi za kufundishia na hosteli ya wanafunzi katika eneo la Mloganzila;
(c) Kujenga miundombinu ya barabara, maji na umeme na kukamilisha makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Korea Kusini na kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kufundishia ya Chuo Kikuu (University Teaching Hospital) katika eneo la Mloganzila;

(d) Kukarabati na kujenga miundombinu katika kampasi ya Muhimbili ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia; na

(e) Kuendeleza utafiti, katika maeneo mbalimbali kama vile malaria, magonjwa ya akina mama na watoto, chanjo ya UKIMWI na dawa asilia.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Chuo Kikuu Mzumbe kitatekeleza kazi zifuatazo:-

(a) udahili wanafunzi wapya 2,600, ambapo 1,400 ni wa cheti, stashahada na Shahada ya Kwanza na 1,200 ni wa Shahada za Uzamili;

(b) Kugharimia mafunzo ya watumishi 20 katika Shahada za Uzamivu na 42 katika Shahada za Uzamili;


(c) Kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400, kukamilisha ujenzi wa ofisi za wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji zenye uwezo wa kuhudumia wahadhiri 271 na wafanyakazi waendeshaji 127 katika Kampasi Kuu Mzumbe na kukamilisha ujenzi wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wasomaji 400 kwa wakati mmoja, kwenye Kampasi ya Mbeya;

(d) Kumalizia malipo ya vitalu vitatu vilivyopo Upanga, kwa ajili ya upanuzi wa Shule Kuu ya Biashara Kampasi ya Dar es Salaam;

(e) Kujenga na kukarabati miundombinu ya chuo ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;

(f) Kukamilisha tafiti 20, kuandaa machapisho na kutoa ushauri katika maeneo ya menejimenti, uongozi na Sayansi ya Jamii; na
(g) Kuchapisha vitabu sita, makala za kufundishia sita na makala nyingine 30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Chuo Kikuu Dodoma kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 5,000 katika shahada ya kwanza na 600 katika Shahada za Uzamili, ambapo asilimia 70 ya wanafunzi hawa wapya watadahiliwa katika shahada za elimu na mafunzo ya sayansi;

(b) Kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya Chuo cha Elimu kwa lengo la kuwa na walimu wanafunzi 10,000, Chuo cha Sayansi Asili na Hisabati wanafunzi 5,000 na Chuo cha Sayansi za Ardhi wanafunzi 3,000;

(c) Kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa Chuo cha Sayansi za Kompyuta, Habari na Mawasiliano ili kiwe na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,500 na kujenga awamu ya pili ya Chuo cha Sayansi za Afya na Tiba ili kiweze kuchukua wanafunzi 4,500;

(d) Kukamilisha ujenzi wa awamu ya pili ya Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii ili kiweze kuchukua wanafunzi 15,000. Ujenzi huu wa awamu ya pili ya Chuo Kikuu cha Dodoma utakiwezesha chuo kufikia lengo la kuwa na idadi ya wanafunzi wapatao 40,000 chuoni hapo;

(e) Kukamilisha ujenzi wa barabara za ndani na za waenda kwa miguu; miundombinu ya kusafirishia maji safi, maji taka na maji ya mvua, umeme na mawasiliano;

(f) Kukamilisha utafutaji wa maji na uwekaji wa miundombinu ya maji safi, kuinua ubora wa mazingira na upandaji wa miti; na

(g) Kuinua ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/2011, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kudahili wanafunzi wapya 230 wa programu ya Cheti, 300 Stashahada na 300 wa Shahada ya Kwanza;
(b) Kugharimia mafunzo ya wanataaluma 10 (watano Uzamili na watano Uzamivu) na wafanyakazi waendeshaji 10 ikiwa ni pamoja na wanaoendelea na masomo;

(c) Kutathmini mitaala ya Cheti, Stashahada na Shahada ili iweze kufanyiwa marekebisho;

(d) Kukamilisha uandaaji wa mitaala ya ualimu kwa programu za Stashahada na Shahada;

(e) Kuendelea na ujenzi wa awamu ya pili katika Tawi la Chuo eneo la Bububu – Zanzibar;

(f) Kufuatilia ufumbuzi wa tatizo la mmomonyoko wa ardhi Kivukoni katika ofisi ya makamu wa Rais – Mazingira; na

(g) Kuanza ujenzi wa hosteli mbili za wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010/11, Chuo cha Ufundi Arusha kitatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuanzisha programu mpya ya shahada ya kwanza katika fani ya Civil and Irrigation Engineering;

(b) Kuandaa mitaala ya programu 4 za Stashahada katika fani za Heavy Duty Equipment Technology, Lapidary & Jewelery Technology, Civil and Irrigation Engineering na Computer Engineering;

(c) Kutathmini mahitaji na kufanya mapitio ya kozi ya msingi ya ukutubi;

(d) Kuanzisha kitengo cha uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kama mashine za kuchomea na Huduma za Utaalam Elekezi;

(e) Kugharimia mafunzo ya mbinu za utaalam uelekezi kwa wanataaluma 15;

(f) Kufanya ukarabati wa jengo la utawala, karakana na nyumba za watumishi; na

(g) Kuandaa Mpango Mkakati wa chuo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani za pekee kwa wananchi, viongozi na Wahisani mbalimbali kwa kuchangia utekelezaji wa Mipango ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Baadhi ya Wahisani hao ni Serikali za: Algeria, Canada, China, Cuba, Finland, India, Ireland, Jamhuri ya Watu wa Korea, Japan, Marekani, Misri, Norway, Pakistan, Poland, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Sweden na Uturuki.

Aidha, mashirika yaliyochangia katika kufanikisha programu zetu za Elimu ni pamoja na Aga Khan Education Foundation, Barclays Bank, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), CIDA ( Canada), COL, CRDB, DAAD, DANIDA, DFID, EDC, GTZ, ILO, International Reading Association, Irish Aid, JICA, JOVC, KOICA, NBC, NMB, NORAD, OPEC, Oxfam, Peace Corps, Plan International, Sida (Sweden), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), UNAIDS, UNDP, UNESCO, UNFPA, UNICEF, USAID, VSO, WFP, Sight Savers International, UIL, Book Aid International, BP, Care International, CBP, Children International,Winrock International, World Vision na ZAIN.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwashukuru viongozi wa matawi ya, CWT, RAAWU, THTU na TUGHE kwa ushirikiano na ushauri wao katika kushughulikia masuala ya wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya, sasa naliomba Bunge lako Tukufu lipitishe makadirio ya matumizi yaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Jumla ya Shilingi 665,572,537,000 kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ili kutuwezesha kutekeleza mpango wa mwaka huu wa Wizara, katika maombi haya:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shilingi 72,005,369,000 zinaombwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Idara ambapo Shilingi 27,107,197,000 zinaombwa kwa ajili ya mishahara na Shilingi 44,898,172,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shilingi 453,935,161,000 zinaombwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Taasisi ambapo Shilingi 169,745,089,000 zinaombwa kwa ajili yamishahara, na Shilingi 284,190,072,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi mengineyo. Kati ya hizo, Shilingi 239,900,000,000 zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Shilingi 139,632,007,000 zinaombwa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kati ya hizo, Shilingi 56,212,445,000 ni fedha za ndani na Shilingi 83,419,562,000 ni fedha kutoka kwa washiriki wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru wewe pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.