You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Daftari, Dr. Maua Abeid[CCM]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
3 4 11 April 2011 Muswada wa Sheria ya Famasi wa Mwaka 2010 (The Pharmacy Bill, 2010)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hiyo ya Muswada wa Famasia.

Mheshimiwa Naibu Spika, si jambo la kupuuza kabisa kuacha kuwasimamia watoa huduma za dawa na vifaa viendavyo navyo. Hivi sasa baadhi yao wanajifanya madaktari ambao wanao uwezo wa kumpa mtu dawa au kujinunulia bila ya kupimwa na kujulikana maradhi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, fani ya Pharmacy ni muhimu sana, kwani bila ya kuisomea na kuijua vyema, watendaji wanaweza kuua mara moja. Zipo dawa zinazouwa over the counter kwa mfano, asprin lakini akipewa mwenye ugonjwa fulani anaweza kufariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya dawa huwezi kuzichanganya na kuliwa kwa pamoja, hivyo iwapo daktari kaandika kwa makosa na pharmacist yupo basi anaweza kuepusha balaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo haja ya kusimamia vyema dawa ya mifugo hivyo bodi inayohusika na uagizaji, usambazaji wa dawa hizo lazima wawe karibu na baraza hili la famasia na kusaidiana mawazo na coordination.

Mheshimiwa Naibu Spika, udhibiti wa dawa za kienyeji zinazotengenezwa locally na zile zinazoagizwa nchini zenye lengo la kuboresha urembo hayana budi sasa kufanyiwa utafiti na kujua ubora wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo haja ya kuweka bayana kazi za TFDA na hizi za Baraza la Famasia ili kuondoa mwingiliano wa majukumu. Baraza hili ni vyema wakaongezewa madaktari katika wajumbe wake kwani wao ndio wanao-prescribe hizo dawa.

Mheshimiwa Naibu spika, composition of the council, kupita kwa baraza hili isiwe ndio chanzo cha kupokea rushwa kwa wauza dawa za reja reja na ukiukwaji wa ethics za profession hii. Naamini regulation nzuri zitatungwa kwa haraka ili kusimamia utekelezaji mzuri wa shughuli za dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo haja na kuwa na baraza la kumlinda mlaji ili watumiaji wapate forum ya kupeleka malalamiko yao na mawazo pia. Naelewa upungufu mkubwa uliopo wa mafamasia na kada hizo ziendazo nazo, hivyo Wizara ianze sasa kuweka mikakati na kutekeleza kwa haraka ya kuongeza intake ya wanafunzi wa fani hiyo katika shule husika. Umuhimu wa kutoa elimu kwa umma ya kuwaeleza majukumu ya Pharmacy Council, TFDA na TBS ili wananchi waelewe wapi pa kupeleka kero zao.