| E-mail this to a friend | Printable version |
| Date | Session | Sitting | |
|---|---|---|---|
| 31 January 2013 | 10 | 3 | |
Hon Freeman Mbowe[CHADEMA] |
|||
KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru sana kwa maelezo ambayo ninaamini ni ya msingi na ya muhimu sana kwa Taifa. Lakini nitaomba swali langu nilielekeze hapo hapo. Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni dhahiri kwamba yaliyotokea Lindi na Mtwara yamesababishwa kwa kiwango kikubwa na Political Mis-management, pamoja na mawasiliano hafifu kati ya Serikali na wananchi, na ni dhahiri kwamba kauli za Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi, vilichochea kwa kiwango fulani kujaza hasira ya wananchi. Na ni ushuhuda ulio wazi kwamba baada ya wewe kwenda na kuona umuhimu wa kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi wale umeweza kupata ufumbuzi angalau wa muda wa tatizo hili. Pamoja na mimi kuwapa pole sana wote walioathirika na maafa haya ni kwa nini sasa Serikali, isiwachukulie hatua za uwajibikaji Watumishi wote wa Serikali na wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao waliona viashiria vyote vya wananchi kutokuridhika na yaliyokuwa yanaendelea Mtwara na bado haikuchukuliwa hatua yoyote ya maana ya kufanya mawasiliano kama ulivyofanya wewe? Pili hapohapo Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni kwa sababu gani sasa Serikali, isiweke wazi Mikataba yote inayohusu Oil and Gas ambayo imeonesha hofu kubwa sana kwa wananchi wa Lindi na Mtwara na hata kwa Tanzania kwa ujumla, ili mambo haya yawe wazi na kila mtu aweze kuyaona, kuondoa hisia ambazo pengine zinajengeka kwa kutokuelewa? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru sana Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ndugu yangu Mbowe. Kuhusu swali la kwanza, kitu nilichojifunza pale ni kweli, inawezekana analolisema kwa kiasi fulani linaweza kuwa lina mshiko. Lakini tukubali vilevile kwamba, vyama vya siasa kwa ujumla wake vimechangia sana katika kupotosha jambo hili. Mheshimiwa Spika, na tatizo lililojitokeza ni kwamba, kila mmoja kwa namna yake alilichukua na kulitafsiri kutegemea na malengo ambayo anataka kuyafikia katika eneo lile. Kwa hiyo, uko vilevile ukweli, wala sio siri, ushindani wa chaguzi zinazokuja na kwa hiyo, jambo gani ukilichukua sasa linaweza likakupa Political mileage lakini bila kujua kwamba, unaweza hata wewe usifike huko katika mazingira ya vurugu kama hizi. Kwa hiyo, mimi ninadhani kikubwa sasa tumefika mahali pazuri, kubwa lisiwe kutafutana uchawi, hapana; tutafanya kazi ya kuchunguza jambo hili kwa kina kujaribu kuona wapi tulikosea, wapi nani alifanya nini, lakini kwa ujumla wake kubwa iwe ni kwamba, hapa tulipofika basi tusirudi tena pale wote kwa ujumla wetu. Litatusaidia sana huko tunakotaka kwenda. Mheshimiwa Spika, la pili. Aah, hili la kuwawajibisha na nini, liko ndani ya uwezo wa Waziri Mkuu, liko ndani ya uwezo wa Rais. Tutaangalia mazingira tutaona kama yanahitaji hatua za namna gani. Lakini mimi kama ninavyotazama pale tutalaumiana wengi tu kwa sababu, jambo lile lilikuwa ni la watu wote pale. Kubwa tu iwe ni ile kwamba, huko tunakokwenda kwa upande wa Serikali, tunapokuwa na mambo makubwa kama haya ushirikishwaji wa jamii kwa ukubwa sana, ndio liwe jambo la msingi. Mheshimiwa Spika, vema, umezungumza juu ya Mikataba na unaona kwamba, pengine ni moja ya kichocheo kikubwa sana katika jambo hili, ni namna tu tutakavyolieleza. Mimi sidhani kama Mikataba ile ina mambo ambayo ni ya ajabu ya siri kubwa sana ambayo, haiwezi kutolewa ufafanuzi watu wakajua ni nini kimo ndani, kimetengenezwaje, kinatakiwa kujibu hoja gani, kwa hiyo, kwa kweli, ni jambo tu ambalo tukikaa kwa utaratibu wa kawaida hata kupitia mfumo wa Kibunge tu, ni vitu vinavyoweza kupatikana mkavitazama, ilimradi tu tufuate utaratibu. |

KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru sana kwa majibu yako, lakini hapa mwisho kidogo umekuwa elusive. Hukutaka kutoa Kauli kwamba, Serikali, inakiri Mikataba hii itatolewa wazi, umesema tunaweza, tunaweza, tunaomba Mheshimiwa Waziri Mkuu uwe firm kwamba, Mikataba hii itawekwa wazi ili kuondoa utata na hofu ambayo wananchi wanaijenga. Mheshimiwa Spika, lakini wakati huohuo Mheshimiwa Waziri Mkuu, utakubali na utakiri kwamba, Serikali yenu inakuwa sikivu pale pressure ya wananchi inapokuwa kubwa? Kwa sababu, bila pressure ya wananchi, mambo yote mazuri ambayo yameelezwa yanayokusudiwa kufanywa Lindi na Mtwara, yalikuwa hayazungumzwi, hayana mawasiliano. Haya mambo yamekuja kuzungumzwa baada ya pressure ya wananchi; utakiri kwamba, sasa Serikali yako inakuwa sikivu baada ya pressure, ikiwemo maandamano? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbowe, anajenga hoja lakini haina mshiko hata kidogo. Mimi naamini suluhu na jibu la kweli, si maandamano hata kidogo. Suluhu ya kweli pale ambapo jambo halieleweki ni watu kukaa chini mkaomba kupewa zinazohitajika, zikatolewa, mkazitumia kwa shughuli za maendeleo. Maandamano ukishayaendekeza mara nyingi matokeo yake huwezi ukayadhibiti ndio shida ninayoiona mimi kwa hiyo, ni vizuri hata kama unaweza ukasema pengine hiyo ndio njia ya kuishiniza, kuifanya tu, Serikali imekuwa sikivu muda wote. Mambo mangapi hapa yanafanyika kwa njia hiyo, muda wote tumekuwa tukisikiliza. Kwa hiyo, ni kitu tu ambacho nadhani ni cha kujiepushanacho kwa sababu, si kitu kizuri sana.
Mheshimiwa Spika, lakini naona umerudia tena lile la Mkataba. Naomba niseme Mheshimiwa Mbowe, Serikali, ilikwishakubali kwamba, Bunge hili linayo fursa ya kupata Mkataba wowote, kubwa ni kufuata utaratibu kupitia Ofisi ya Spika. Spika, ataiarifu Serikali, Mkataba unaohitajika tutauleta utatazamwa kwa utaratibu tuliokubaliana. Sasa ukisema uanikwe maana yake unataka twende tukatoe kwenye magazeti na kwenye nini, mikataba nayo ina misingi yake kwa hiyo, ni lazima tuendelee kuiheshimu vilevile. Lakini hiyo, haina maana kwamba, watu wasipate kujua ni nini kimo kama wanaona iko sababu ya kufanya hivyo. |

Hon Namelok Sokoine[CCM] |
|||
Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wenyeji wa Wilaya ya Ngorongoro, wamekuwepo pale kabla ya ukoloni na kabla ya eneo lile kutangazwa kuwa Hifadhi. Kwa hivyo basi, wana sababu ya kutumia rasilimali zilizokuwepo katika eneo lile, lakini Serikali, ilipitisha Sheria bila kuwashirikisha wananchi wa eneo lile ya kupiga marufuku kufanya shughuli zozote za kiuchumi, ikiwemo kulima bustani katika eneo lile. Mheshimiwa Spika, hivi karibuni, Mheshimiwa Waziri Mkuu, tulipata taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba, wananchi wale wanateseka na njaa na hivyo kuwapelekea akinamama, watoto, kuteseka na njaa na hata baadhi ya watoto kulazwa katika Hospitali, wakiwa wamepata utapiamlo. Mheshimiwa Waziri Mkuu, je, Serikali, wakati inatunga Sheria hiyo, ilikuwa ina mpango gani wa kudumu kwa ajili, ya wenyeji wanaoishi katika eneo lile? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, sina hakika kama nimemwelewa vizuri kwa sababu, Morogoro Ngorongoro, ooh, sorry. Alikuwa anazungumzia Ngorongoro, nilisikia kama Morogoro. Samahani sana. Mheshimiwa Spika, suala la Ngorongoro ni jambo ambalo pengine, suluhu ya kweli, labda ni kukaa na kulitazama tena. Kwa sababu, si jambo limeanza leo, ni jambo la muda mrefu. Ni jambo ambalo limekuwa likitazamwa kwa misingi ya kisheria kwa muda mrefu. Lakini moja ambalo unaweza kabisa ukaliona ni kwamba, kadiri idadi ya watu inavyoongezeka, shinikizo la hali ya maisha katika eneo lile na yenyewe inazidi kuongezeka. Ndio maana unaona sasa hivi kunajitokeza mahitaji ambayo inabidi kama Serikali, tukae chini tuone tunafanyaje. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka nikubaliane na Mheshimiwa Namelok kwamba, pengine kitakachohitajika hapa ni kuchukua muda kidogo kujaribu kulifanyia kazi, tuone Sheria zile zinasema nini, sasa hivi wanaishije, tulikuwa tukifanya nini muda wote katika mazingira ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo. Halafu, tuone kama bado Sheria hizo ni relevant au bado ni za msingi au kama kunahitajika kuzirekebisha kidogo katika kujitahidi kukidhi mahitaji mapya. Ni lazima tukubali ni eneo nyeti kidogo na ni lazima tuone namna ya kushughulika nalo. |
|||
| 31 January 2013 | 10 | 3 | |
Hon Namelok Sokoine[CCM] |
|||
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru sana kwa majibu yako mazuri. Kwanza, niipongeze Serikali, kwa hatua iliyochukua ya kuamua kupeleka mahindi mara baada ya kutangazwa. Lakini pia, niipongeze Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili, pia walikwenda kuona hali halisi inayoendelea ndani ya Ngorongoro. Je, Mheshimiwa Waziri Mkuu, unafikiri ni muda gani tutachukua mpaka ufumbuzi huo utakapopatikana, wakati Watanzania wenzetu wanateseka na njaa? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, swali gumu. Ukisema itachukua muda gani, siyo rahisi sana kulijibu. Lakini mimi ninadhani kubwa hapa, kama nilivyosema, tukae chini tuliangalie suala zima kwa mtazamo ambao utajaribu kuwianisha maslahi yote ya wananchi, ya nchi, halafu tuone ni namna gani tutaweza kuondokana na hili tatizo. Mheshimiwa Spika, kwa sasa tunachofanya ni kujaribu tu kusaidia kujibu tatizo la sasa. Inapotokea kwamba, kuna njaa mahali tunajitahidi kusaidia, lakini ni dhahiri kwamba, hatuwezi kuendelea hivyo kwa muda wote. Kwa hiyo, ni lazima tufike mahali tuone suluhu ya kweli ni kitu gani. |
|||
| 31 January 2013 | 10 | 3 | |
Hon Mwigulu Nchemba[CCM] |
|||
Mheshimiwa Spika, asante. Mheshimiwa Waziri Mkuu, hali ilivyo sasa ni karibu kila Halmashauri, ina upungufu wa watumishi. Na Idara nyingi za Serikali, kama si zote, zina upungufu wa Watumishi wa Serikali, mpaka Tume ya Mipango ina upungufu wa Watumishi wa Serikali. Na wakati huo huo karibu kila mtaa kuna mwanafunzi aliyetoka chuo chenye heshima hapa Tanzania na wengine nje ya nchi, anatafuta kazi. Sehemu nyingine kuna mtu mmoja anashikilia nafasi zaidi ya moja, yaani nafasi yake na anakaimu nafasi ya mtu aliyekuwa anakaimu. Swali linakuja. Hawa vijana wanaotoka chuo wakienda kuomba kazi, wanaambiwa waje na uzoefu wa miaka mitatu (3) na zaidi. Swali la kwanza, ni kwa nini Serikali, inaruhusu upungufu wa Watumishi Serikalini, ilhali kuna wanafunzi inaowasomesha kwa gharama kubwa wako mtaani wanatafuta kazi? Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kama tatizo ni uzoefu, wanaambiwa waje na uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu (3) ama minne (4), ilhali hakuna chuo kinachofundisha uzoefu. Ni kwa nini usitoe tamko leo kufuta kigezo hicho, wanafunzi wanapotoka chuo wanapoomba nafasi za kazi za kuanzia? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, naomba nijaribu kumjibu ndugu yangu Mheshimiwa Mchemba, kama ifuatavyo; kubwa ni kweli tunakubali kwamba, uko upungufu wa watumishi kwa ujumla. Na upungufu mkubwa zaidi hasa uko kwenye eneo la Walimu, ambao ndio bado linatusumbua, ingawa tunaendeleza zile jitihada za kujaribu kutoa wanafunzi wengi zaidi kwenye sekta hii ya elimu, kama tulivyosema mwaka huu tunatarajia kuajiri Walimu 25,000. Lakini bado utakachokiona kwa upande wa Walimu ni kwamba, ongezeko la wanafunzi mwaka hadi mwaka na ongezeko la shule, litaendelea kuwa ni tatizo litakaloendelea kwa muda kidogo kabla hatujamaliza kabisa. Lakini juhudi za kuendelea kuongeza udahili wa wanafunzi vyuo vikuu nadhani unakwenda vizuri kwa sasa. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa watumishi wengine, Sekta ya Afya nayo, bado haijakaa vizuri. Wizara ya Afya, inajitahidi kuongeza udahili wa wanafunzi katika eneo hilo, lakini bado kama mnavyojua mradi ule ni mkubwa, Zahanati kila Kijiji, Kituo cha Afya kila Kata kwa hiyo, demand ni kubwa kidogo, lakini nayo inasimamiwa inakwenda vizuri. Mheshimiwa Spika, kwa Idara nyingine, ninachoweza kusema kwa uhakika ni kwamba, tuko katika hali nzuri zaidi kuliko katika Sekta hizo mbili. Inawezekana kwenye Halmashauri moja moja kwa sababu moja au nyingine pakawa na upungufu zaidi, lakini kwa ujumla wake Idara nyingi katika Halmashauri nyingi hazina matatizo makubwa, tumejitahidi sana. Na wala si kweli kwamba, tunapoajiri kigezo hicho ndio tunakizingatia muda wote, hata kidogo; tumechukua vijana wengi sana tumewaajiri moja kwa moja na wengine kwa kweli, uzoefu wanaupata wakiwa katika Halmashauri zenyewe. Mheshimiwa Spika, na tunatambua kwamba, mahitaji kwenye Halmashauri, huwezi ukasubiri eti mpaka apate uzoefu, uzoefu anaupata wapi kama yeye mwenyewe ni mtu wa mipango na mipango iko ndani ya Halmashauri. Kwa hiyo, tumeajiri wengi; tatizo tunaloweza kulikubali tu ni kwamba, inawezekana Sekta ya Umma, haitoshi kuwaajiri wote kama pengine inavyohitajika. Lakini hata hivyo, tutajitahidi kuangalia kwa karibu zaidi tuone wapi, labda kwenye Halmashauri yako kuna tatizo pengine maalum, tutajaribu kulikabili na kulimaliza. |
|||
| 31 January 2013 | 10 | 3 | |
Hon Mwigulu Nchemba[CCM] |
|||
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Waziri Mkuu, lakini pia bado natambua kwamba, kuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana na hili la uzoefu. Ni kwa nini, Serikali, isiandae mpango maalum wa kuwa inachukua vijana kwa ajili ya attachment, hata wakalipwa gharama za usafiri tu, ili wawe wanapata uzoefu na kuweza kutambua ujuzi wa mwanafunzi? Kwa sababu vyeti peke yake havitoshi kujua mwanafunzi ana uwezo gani wa kazi. |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, sawa. Nadhani ni ushauri mzuri tu, acha tutaungalia tuone namna ya kulitekeleza. Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, lakini naomba tu niseme. Nilisahau kidogo pale Mtwara Mjini, nyumba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Sinani na yenyewe ilichomwa moto; nilikuwa nimepitiwa kuitaja ile nyumba. Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ahsante sana |
|||
| 8 November 2012 | 9 | 8 | |
Hon Freeman Mbowe[CHADEMA] |
|||
KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kwanza ya kumuuliza swali Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunatambua kwamba Taifa letu sasa hivi linapita katika mchakato wa kutafuta maoni ya Watanzania kuhusu Katiba mpya iliyopendekezwa. Pamoja na Serikali kutoa ahadi yake kwamba, ingependa Katiba hii iwe tayari kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2015, bado ni jambo la kupenda, lakini linaweza lisiwe la uhalisia. Sasa swali langu, kwa kuwa mchakato wa Katiba hautoi mamlaka kwa Serikali kuvunja Katiba iliyopo na kwa sababu Katiba inatoa mamlaka kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 kupiga kura. Pia kwa sababu tangu Uchaguzi Mkuu uliopita tumeendelea kufanya Chaguzi mbalimbali bila kuthamini kwamba tuna watu ambao tunawanyima uhuru wa kupiga kura kwa sababu daftari la kudumu la kupiga kura bado limepitwa na wakati. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tarehe 19 Aprili, nilikuuliza swali hapa kuhusiana na mpango wa Serikali hasa Ofisi yako katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na ulitoa ahadi ya Serikali ya kulifanyia kazi jambo ambalo mpaka sasa hivi halijatekelezwa. Mheshimiwa Waziri Mkuu, una kauli gani ya kuwaambia Watanzania kuhusiana na hili? |
|||
| Answer From Prime Minister | |||
Mheshimiwa Spika, Tanzania tumeweka utaratibu wa upigaji kura na namna gani tunaweza tukawapata wale wote wenye kustahili kupiga kura waweze kupata fursa ya kupiga kura na utaratibu wa lile daftari la wapiga kura ilikuwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha kwamba hakuna Mtanzania tunayemwacha nje ya utaratibu huo. Ndiyo maana katika daftari lile tulipoanza tukaweka na utaratibu vile vile wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na utaratibu wa kuendelea kuliboresha daftari lile mara kwa mara ili tusije tukamwacha mtu au tusije tukaenda na watu ambao tayari pengine bado hawako hai. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, bado naamini utaratibu ule ni mzuri na kama nilivyoahidi ni kitu ambacho kiko ndani ya utaratibu wa Tume na sisi kazi yetu ni kuiwezesha Tume kutekeleza hilo jukumu wakati wanapohitaji Serikali kusaidia. Kwa hiyo, tutaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu na wala hatuna dhamira yoyote ya kutaka kumnyima fursa mtu yeyote kwa sababu hatuna sababu ya kutokufanya hivyo. Kwa hiyo, imani yangu ni kwamba bado tuko katika mstari sahihi. |