Parliament of Tanzania

Overview

Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.

Bunge la Tanzania linaendeshwa kwa misingi ya Bunge la Jumuiya ya Madola na linafuata mtindo wa Bunge la Jumuiya ya Madola kwa kiwango kikubwa.

Uhai wa Bunge:

Ibara ya 65 ya Katiba inaeleza kuwa maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano. Hivyo, Uhai wa Bunge ni muda unaoanzia tarehe ambayo Bunge Jipya limeitishwa na Rais kukutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaida kufanyika.

Muhula wa Bunge:

Muhula wa Bunge ni vikao mbalimbali vya Bunge vinayoanzia mkutano wa kwanza wa Bunge baada ya kuvunjwa na vinavyoishia Bunge linapovunjwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwingine.

Bunge linaongozwa na Spika ambaye huchaguliwa na Wabunge miongoni mwao au anaweza asiwe Mbunge, lakini ni lazima awe mwanachama wa chama kimojawapo ambaye atapitishwa na chama chake na mwisho kupigiwa kura na Wabunge.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 22 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2016, Rais ndiye huliitisha Bunge jipya. Kwa kawaida, Bunge la kwanza huanza mnamo mwezi Oktoba baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mkutano wa Bunge:

Bunge limeundwa na vipindi viitwavyo Mikutano. Mkutano wa Bunge ni mfululizo wa vikao vya Bunge, kuanzia kikao cha kwanza hadi cha mwisho. Kuna Mikutano 20 katika Bunge moja.

Kuna mikutano minne katika Bunge.

  1. Mkutano wa kwanza, kati ya Oktoba hadi Novemba;
  2. Mkutano wa pili, kati ya Januari hadi Februari;
  3. Mkutano wa tatu, kati ya Aprili hadi Juni;
  4. Mkutano wa nne, kati ya Augosti hadi Septemba.


Kikao cha Bunge:

Kikao cha Bunge ni kipindi cha siku moja kinachoanza kwa kusomwa Dua na kumalizika kwa kuahirisha Bunge hadi siku itakayotajwa au kwa kumalizika kwa mkutano au Bunge.

Kanuni ya 29(2), Waziri Mkuu ambaye ndiye Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni hutoa hoja ya kuliahilisha Bunge kwa kutaja siku, mahali na saa ambapo mkutano unaofuata utaanza.



Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's