Parliament of Tanzania

Wabunge wawachangia waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera

Wabunge wameazimia kwa kauli moja kutoa posho zao zaKikao cha Tano cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Moja, leo tarehe 13 Septemba, 2016 ili fedha hizo zikasawaidie Wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016.

Hoja hiyo ilitolewa na Mbunge wa Mlalo, Mheshimiwa Rashid Shangazi ambaye awali alitoa Hoja ya kuahirisha mjadala uliokuwa mezani ili kujadili suala hilo kwa muda wa nusu ambapo wakati akichangia alipendekeza Waheshimiwa Wabunge watoe posho zao za siku moja kuwasaidia wahanga hao ikiwa kama sehemu ya rambirambi na kuwashika mkono Wahanga wa tetemeko hilo.

Mara baada ya Waheshimiwa Wabunge kuikubali hojahiyoNaibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson aliwashukuru Wabunge wote kwa kukubali kutoa fedha hizo ambapo pia aliwataka Waheshimiwa Wabunge kusimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka Marehemu wote walipoteza maisha katika janga hilo.

Aidha, Naibu Spika aliaigiza Serikali kumaliza mapema kufanya tathimini ya athari zilizosababishwa na Tetemeko hilo ili kujua ni mahitaji kiasi gani yanatakiwa kuelekezwa huko ikiwemo mahitaji ya Chakula, Malazi pamoja na Matibabu.

Kuhusiana na kuundwa kwa Kamati Maalum ya Bunge ya kushughulikia suala hilo, Mheshimiwa Naibu Spika alisema kuwa suala hilo litashughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.

Awali akitoa kwa niaba ya Waziri Mkuu kauli ya Serikali kuhusiana na Tetemeko hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa George Simbachawene alisema hadi sasa idadi ya vifo vilivyoripotiwa kutokana na tetemeko hilo katika Mkoa wa Kagera ni 17 huku majeruhi wakiwa 252.

Mhe Simbachawene aliongeza kuwa Serikali imechukua na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwapatia makazi ya muda baadhi ya wananchi ambao wameathirika ikiwemo kuhakikisha majeruhi wote wanapata matibabu.

Kwa upande mwigine, Wabunge wameendelea kujadili miswada miwili ambayo ni Muswada Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016 (The Government Chemist Labaratory Authority Bill,2016) na Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa Mwaka 2016 (The Chemist Professionals Bill, 2016). Miswada hiyo iliwasilishwa Septemba 9, 2016 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's