United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
TAARIFA YA MHE. SPIKA
________________
[Imetolewa Chini ya Kanuni ya 33(1) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016]
_______________
Katika Mkutano wa Tisa wa Bunge, Bunge lilipitisha Miswada Minne ya Sheria ya Serikali ifuatayo:-
1. Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017 [The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017];
2. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendment) (No. 4) Bill, 2017];
3. Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania wa Mwaka 2017 [The National Shipping Agencies Bill, 2017]; na
4. Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wa Mwaka 2017 [The Drugs Control and Enforcement (Amendment) Bill, 2017].
Kwa taarifa hii, napenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba, tayari Miswada hiyo minne imepata Kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa Sheria za Nchi zinazoitwa:-
1. Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya Mwaka 2017 [The Tanzania Telecommunications Corporation Act No.12 of 2017];
2. Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) Na. 13 ya Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendment) (No. 4) Act No.13 of 2017];
3. Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania Na. 14 ya Mwaka 2017 [The National Shipping Agencies Act No. 14 of 2017]; na
4. Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 15 ya Mwaka 2017 [The Drugs Control and Enforcement (Amendment) Act No. 15 of 2017).
Job Y. Ndugai (Mb)
SPIKA
30 Januari, 2018