Parliament of Tanzania

Spika awaasa Mawaziri na Wabunge kuzingatia Mahudhurio wakati wa vikao vya Kamati za Bunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amewataka Wabunge na Mawaziri kuzingatia mahudhurio wakati wa shughuli za Kamati za Bunge.

Mheshimiwa Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni leo kabla ya Kuahirisha Mkutano wa Nne wa Bunge ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mahudhurio hafifu ya Mawaziri na Wabunge katika Vikao vya Kamati vilivyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 02, 2016, Mjini Dodoma.

Alisema katika vikao hivyo vya Kamati imetengenezwa orodha ya Wabunge na Mawaziri watoro ambayo ataitunza hadi vikao vingine vya Kamati vinavyotarajia kuanza Octoba 17, 2016 ili kuona kama wataendelea na tabia hiyo.

“Ningeomba tunakoenda tuzingatie sana mahudhurio kwa pande zote mbili, kwani katika vikao vilivyopita vya Kamati yamekuwa hayaridhishi kabisa,” alisema Spika.

Aidha, Mheshimiwa Spika aliwashukuru Wabunge kwa kuendesha Mkutano wa Nne kwa salama na amani bila migogoro yoyote.

“Watanzania hawapendi kuona vurugu na msambaratiko, msambaratiko ukianzia Bungeni utakwenda hadi kwa wananchi vilevile umoja ukianzia hapa unaenda kwa wananchi wetu, naomba tuendelee na utaratibu huu wa kudumisha amani ndani ya Bunge letu,” alisema.

Mheshimiwa Spika pia alizungumzia suala la Serikali kuhamia Dodoma ambapo alisema Ofisi ya Bunge tayari imeshahamia na kwamba shughuli zake zote inazifanyika Dodoma huku akiwatoa hofu ya maeneo kwa ajili ya viwanja vya makazi na ofisi kwa Wabunge na wafanyakazi wa Serikali.

“Kuna maeneo ya kutosha kwa ajili ya Wabunge, Ofisi za Serikali hivyo msiwe na wasiwasi, kwa yeyote anayehitaji Kiwanja nawahakikishia kuwa watapata,” alisema Mhe Spika.

Mkutano wa Nne wa Bunge umeahirishwa hadi Novemba Mosi, 2016, Jumanne saa tatu Asubui.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's