Parliament of Tanzania

SPIKA achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maspika katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola-Afrika

Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika. Uchaguzi huo umefanyika katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliofanyika Mjini Abuja.

Kwa wadhifa huo, Mhe Ndugai ataongoza Maspika wenzake toka Mabunge na Mabaraza ya kutunga Sheria 63 yaliyoko katika nchi 18 za Jumuiya ya Madola kwenye Bara la Afrika. Wadhifa huo ni wa miaka miwili kuanzia sasa hadi mwaka 2019 kutakapofanyika uchaguzi mwingine.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mabunge Barani Afrika ni pamoja na Afrika ya Kusini, Bostwana, Cameroon ,Ghana, Kenya, Lesotho, Msumbiji, Mauritius, Malawi, Nigeria, Namibia, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia.

Akizungumzia uchaguzi huo, Mhe Ndugai amesema "Kwa hakika nawashukuru Maspika wenzangu kwa kunipa dhamana hii ya kuwa Mwenyekiti wao, ni heshima kwangu binafsi lakini zaidi Kwa Tanzania. Nimatumaini yangu kwamba Bunge letu litaendelea kung'ara kitaifa na kimataifa tukiwa Bunge moja lenye Upendo na mshikamano".

Huu ni wadhifa wa nne kwa Mhe. Ndugai katika masuala ya Bunge kwenye medani ya Kimataifa. Amewahi kuwa Mwakilishi wa Nchi za Afrika Mashariki katika Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani mwaka 2008-2011, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Umoja wa Mabunge ya Afrika, Pacific na Carribbean na Jumuiya ya Ulaya mwaka 2011-2014 na Rais wa Baraza la Mabunge ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC – PF).

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's