United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma leo.
Akizungumza wakati akipokea Ripoti hiyo Naibu Spika amesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu kwa Bunge na ni kiashiria cha ushirikiano mzuri kati ya Bunge na Tume hiyo.
“Ushirikiano uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mzuri na kwa upande wangu natumaini tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Dkt.Tulia.
Akizungumzia majukumu ya Bunge Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge la kumi na moja linatimiza majukumu yake vyema hali itakayochochea maendeleo hapa nchini katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tume hiyo na Bunge kama mdau muhimu na kuahidi kuuendeleza kwa maslahi ya pande zote.
Ziara ya Tume hiyo pamoja na kukabidhi ripoti hiyo kwa Naibu Spika ililenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Tume hiyo kuhusu majukumu ya Bunge ambapo wajumbe hao walitembelea maeneo mbalimbali ya Bunge.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.