United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mkutano wa Kumi wa Bunge la
Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo Jumanne tarehe 30
Januari 2018 na unatarajiwa kumalizika tarehe 9 Februari 2018 Mjini Dodoma.
Mkutano huu umeanza kwa kushuhudia Wabunge wapya watatu waliochaguliwa hivi karibuni wakila Kiapo cha Uaminifu. Wabunge hao ni;
Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro – Songea Mjini.
Mhe. Monko Justine Joseph – Singida Kaskazini.
Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa –
Longido.
Katika Mkutano huu wa Kumi, wastani
wa maswali 125 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge. Aidha, wastani wa
Maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa
kwa siku ya Alhamisi tarehe 1 na 8 Februari,2018.
Kwa upande wa Miswada ya Serikali, Bunge
pia linatarajia kupitisha kwa hatua zake zote Miswada Miwili ya Sheria ambayo
ilisomwa Mara ya Kwanza katika Mkutano wa Tisa wa Bunge kwa mujibu wa
Kanuni ya 91. Miswada hiyo ni :-
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 5) wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 5) Bill, 2017].
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017 [The Public Service Social
Security Fund Bill, 2017].
Aidha, wakati wa Mkutano huu, Kamati 16 za Kudumu za Bunge zitawasilisha Taarifa zake Bungeni.
Hon. Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika
Newala Mjini (CCM)