Parliament of Tanzania

Mhe. Spika atoa wito wa Kampuni kutoka Misri kuja kuwekeza hapa nchini

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ametoa wito kwa Kampuni kutoka Misri kuja kuwekeza hapa nchini.

Mhe Spika alitoa wito huo wakati akizungumza na wabunge kwenye mkutano uliokutanisha na viongozi wa mabunge ya nchi tatu katika Ukumbi wa Pius Msekwa.

Viongozi hao ni Spika wa Bunge la Misri Dkt. Abdel Alal, Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo na na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Kimataifa (CPA), Emilia Lifaka

“ “Tunaimani na kampuni kutoka Misri zitaendelea kuja kuwekeza hapa nchini,” alisema.

Aidha, aliwashukuru viongozi hao kwa kuja kutembelea Bunge ambapo watapata furasa ya kukutana na viongozi mbalimbali ikiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Kwa upande wake Spika Bunge la Misri Dk Abdel Alal mbali na kushukuru kwa mapokezi mazuri alisema nchi yake itaendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya kimkakati chini ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Alitolea mfano mradi unaeendelea wa Mradi ya kuzalisha umeme megawati 2,115 kwa njia ya maji wa Stiegler’s Gorge, Dk Ahamed alisema kampuni zaidi kutoka nchini kwake ziko tayari kuja na kuwekeza Tanzania.

Dkt. Ahamed alipongeza utekelezaji wa mradi wa Stiegler’s Gorge ambalo alisema ni miongoni mwa masuala yaliyoimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, alisema wamekubaliana na Spika Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuunda Jumuiya ya bonde la Mto Nile kwa sababu ya manufaa ya mto huo.

Kwa upande wake , Rais wa Seneti ya Burundi, Ndikuriyo alisema Mkataba wa Amani wa Arusha umesaidia kurejesha amani katika nchi ya Burundi, na kutumia fursa hiyo kumpongeza Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete iliyesaidia kufanikisha makubaliano hayo alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Ndikuriyo alisema uhusiano mzuri kati ya Burundi na Tanzania ulianza tangu dunia ilipoumbwa na kwamba uhusiana huo ni wa kihistioria.

Awali, Mwenyekiti wa CPA na Naibu Spika wa Cameroon, Lifaka aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge wanawake ambayo ni asilimia 36. 7 ya wabunge wote.

“Hili ni jambo la kujivunia, kwa utashi huu wa kisisasa wa kutowasahau wanawake wanaojitokeza kugombea nasafi mbalimbalimbali,” alisema.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's