Parliament of Tanzania

Mhe Spika aahidi kudumisha uhusiano na Baraza la Wawakilishi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza Viongozi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa ataendeleza na kudumisha uhusiano baina ya Vyombo hivyo viwili.

Akizungumza na Viongozi wa Baraza hilo mara ya kuwasili Visiwani humo kwa kutumia Boti, Mhe Ndugai alimueleza Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lipo tayari kuanzisha programu maalum kwa ajili ya kubadilishana uzoefu baina ya Wajumbe wa Baraza hilo na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kuna haja kuanzisha utaratibu maalum wa kudumisha ushirikiano huu kwa kuweka utaratibu utakaowezesha kubadilishana uzoefu si tu baina ya Wajumbe na Wabunge lakini pia baina ya Watumishi wa toka pande zote,” alisema Mhe Ndugai.

Kwa upande wake Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid alimueleza Mhe Ndugai kuwa amefurahishwa na ziara yake ya kutembelea Baraza la Wawakilishi.

Aliongeza kuwa Baraza la Wawakilishi litaendelea kujifunza na kuomba ushauri toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ili hilo lifanikiwe kuna haja ya kuboresha zaidi mahusiano ya mihimili hiyo miwili ya kutunga sheria.

Pia Mhe. Maulid aliunga mkono hoja ya kuanzisha utaratibu wa kubadilishana uzoefu baina ya Wabunge na Watumishi wa Vyombo hivyo huku akisema kuwa utaratibu huo ni mzuri na utazidi kudumisha ushirikiano.

Aidha baada ya kuzungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Ndugai alipata fursa ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Wawakilishi na baadaye kutembelea Idara mbalimbali za Ofisi za Baraza la Wawakilishi na kujionea jinsi Watendaji wake wanavyofanya kazi.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's