United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana
Jumatatu tarehe 23 Oktoba 2017 Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa Tisa wa Bunge tarehe 7 Novemba 2017. Mhe. Spika Job Ndugai ameziita Kamati hizo
kuanza shughuli zake tarehe hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (3) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge.
Aidha,
Mhe. Spika aliziita mapema Kamati ya Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama na Kamati ya HesabuzaSerikali (PAC) kuanza vikao vyake toka Oktoba
16, 2017.
Katika kipindi chote hiki,
shughuli zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kupokea, kuchambua na kujadili taarifa
kutoka Serikalini, taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), uchambuzi wa Sheria Ndogo na uchambuzi wa miswada mitatu ya sheria.
Mkutano wa Tisa wa Bunge hili la kumi na Moja unatarajiwa kufanyika Bungeni Mjini Dodoma kuanzia tarehe 9 Novemba, 2017 mara baada ya Vikao vya Kamati za kudumu za Bunge.
Unaweza kusoma ratiba ya vikao vya kwa kila
Kamati kupiti Tovuti hii ambayo ni www.parliament.go.tz