Parliament of Tanzania

Kamati ya Viwanda yapokea taarifa ya Wizara

Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira imekutana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mjini Dodoma na kupokea taarifa ya Wizara juu ya maendeleo ya Sekta mbalimbali katika Wizara hiyo.

Akiwasilisha taarifa hiyo Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru alisema Serikali ya awamu ya tano imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda ambapo miradi 114 ya uwekezaji wa viwanda vipya imesajiliwa na Kituo Uwekezaji nchini (TIC)

Alisisitiza kuwa miradi hiyo pamoja na Viwanda vipya ipo katika hatua za mwisho za ujenzi na kwamba mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu Viwanda hivyo vitakuwa tayari kuanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la ndani na la nje

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Mheshimiwa Charles Mwijage (Mb) alisema maendeleo ya Viwanda yanategemea sekta nyingi na kwa kujua hilo Wizara yake inashirikiana kwa karibu na Wizara nyingine kuhakikisha wanatekelza adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya Uchumi wa Viwanda.

Akitoa ushauri wa Kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Dalali Peter Kafumu (Mb) aliishauri Wizara na taasisi zake zijipange ili kuondoa changamoto zilizoikwamisha Tanzania kupiga hatua kubwa katika sekta ya VIwanda hususan kwa Serikali za awamu zilizopita.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's