Kamati ya PAC yaigiza SUA kutafuta fedha ya kuendeleza miradi yote waliorithi kutoka ANC
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imekiagiza Chuo Kikuu cha
Sokoine (SUA) kutafuta fedha kwa ajili ya kuiendeleza miradi yote
iliyorithiwa na Chuo hicho kutoka Chama cha Ukombozi wa Afrika ya Kusini
(ANC).
Kamati ilitoa agizo hilo jana wakati ilipotembelea Chuo
hicho na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na chuo ikiwemo hiyo
iliyoachwa na chama cha ANC iliyopo eneo la Mazimbu Mkoani Morogoro.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na shamba la nguruwe, shamba la kufugia ng'ombe, majengo,mashamba na vinu vya kuhifadhia nafaka.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Ujumbe wa Kamati hiyo, Shally Raymond
alisema uongozi wa SUA lazima uhakikishe miradi hiyo inafanya kazi ili
iweze kuingiza mapato ya Chuo na pia kuwasaidia Watanzia kwa ujumla.
"Miradi
hii ni hazina kubwa sana tuliyoachiwa na ni ya gharama kubwa,tujitahidi
tutafute fedha ili tuifufue iweze kufanya kazi kulingana na uwezo
wake," alisema.
Alisema kwa sasa miradi hiyo inazslisha chini ya
kiwango na kwamba Chuo hicho kinatakiwa kutafuta fedha ili kukarabati
baadhi ya miundombinu pamoja na kupata mitaji ya kuendeleza miradi.
Kwa
upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gerald Monela alisema
ni kweli suala la kutoendeleza miradi hiyo ipasavyo limekuwa likiwaumiza
kama viongozi na limekuwa likijadiliwa mara kwa mara katika vikao vya
Baraza la Chuo hicho.
"Tatizo kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili
ya mtaji na kukarabati baadhi ya mitambo ikiwemo mtambo mkubwa wa
kuzalisha chakula cha mifugo, tumekuwa tukifanya michakato mbalimbali ya
kuomba mikopo benki lakini tunakwama kutokana na kukosa dhamana kutoka
Serikalini," alisema.
Alisema kwa sasa chuo hicho kimeanzisha
Kampuni itakayosimamia miradi yote ya chuo ikiwemo miradi ya ANC na
kwamba kwa sasa kipo katika mchakato wa kumpata Meneja wa Kampuni hiyo.