Parliament of Tanzania

Bunge lapitisha Bajeti ya Serikali

BUNGE limepitisha Bajeti ya Serikali ya Trilion 29.5 baada ya kuhitimisha mjadala mkali wa kujadili na kuchambua bajeti hiyo Bungeni uliodumu kwa siku tano.

Bajeti hiyo ambayo ni ya kwanza katika Serikali ya Awamu ya Tano iliwasilishwa Bungeni tarehe 8 Juni, 2016 na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango ambapo kabla ya kufanyiwa maamuzi na Bunge, wabunge walipata fursa ya kuijadili na kuichambua ikiwa ni matakwa ya kikanuni .

Akitangaza matokeo ya kura baada ya wabunge kuipigia kura Bajeti hiyo Bungeni, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah amesema Idadi ya wabunge wote waliokuwepo ukumbini ilikuwa 252 ambapo kati yao waliopiga kura za ndiyo walikuwa 251 huku kukiwa hakuna kura ya hapana.

Aidha, kura moja ambayo haikupigwa ilikuwa kura ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson ambayo kwa kawaida huwa ni kura ya maamuzi.

Dk. Kashilillah amesema idadi ya wabunge wote Kikatiba ni 393 lakini hadi sasa wabunge waliopo ni 389 huku wabunge 137 walikuwa hawapo ukumbini.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Naibu Spika amesema Bajeti hiyo imepitishwa kwa kishindo kwa kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, akidi ya kikao cha Bunge kuendelea ni nusu ya wabunge ambao ni 195 na ili Bajeti hiyo ipitishwe ilitakiwa kupigiwa kura ya ndiyo na nusu ya akidi ya wabunge 195 ambao ni wabunge 98.

Upitishwaji wa Bajeti hiyo ni umefanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 107 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge ambayo inaelekeza kwamba mjadala kuhusu Hotuba ya Bajeti utakapomalizika huku Kanuni ya 77 (1) ikieleza idadi ya wabunge wakati wa kufanya maamuzi kwamba itakuwa ni nusu ya wabunge wote.

Wakati huohuo Bunge limepitia Muswada wa Sheria ya kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa mwaka 2016.

Muswada huo umepitishwa leo katika hatua zake zote mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Serikali.

Akielezea namna ya upitishwaji wa Muswada huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema ni tofauti na miswada mingine kwa kuwa hautangazwi katika Gazeti la Serikali na wala haujadiliwi na wabunge.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's