Parliament of Tanzania

Bunge laongeza Siku ili kuchambua Miswada mitatu ya Sheria za Ulinzi wa Rasilimali za Taifa

Bunge limeongeza siku za Mkutano wa Saba hadi tarehe 05 Julai 2017, ili kupitia Miswada mitatu ya sheria inayohusu marekebisho ya Sheria za Madini na ulinzi wa rasilimali za Taifa.

Akitoa maelezo Bungeni, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alisema kuwa Kamati ya Uongozi ilikutana tarehe 28 Juni, 2017 Jioni, ili kufanya marekebisho ya Ratiba ya Mkutano wa saba Bunge ambao ulitarajiwa kuisha tarehe 30 Juni, 2017 na kukubaliana kuongeza siku tatu za kazi hadi tarehe 5 Julai, 2017 ili kuliwezesha Bunge kupitia Miswada hiyo.

Kufuatia uamuzi huo Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa ameunda Kamati ya pamoja itakayopitia Miswada miwili ambayo tayari imeshasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Miswada hiyo ni; Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017];(iii)Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permmanent Sovereignty)] Bill, 2017].

Mhe Spika alisema kuwa Kamati hiyo ya pamoja itakayochambua miswada hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe Dotto Biteko na itajumuisha Wajumbe wa Kamati nne za Bunge ambazo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Aidha kwa upande mwingine Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Uenyekiti wa Mhe Mohamed Omary Mchengerwa itauchambua Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's