Parliament of Tanzania

Bunge laahirishwa hadi Septemba 5

Mkutano wa Saba wa Bunge umeahirishwa hadi Septemba 5 mwaka huu huku Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwapongeza Wabunge na Mawaziri kwa ushirikianio wao katika kipindi chote cha miezi mitatu.


Akitoa shukrani hizo mara baada ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Spika aliwashukuru pia wasaidizi wake ambao ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na wenyeviti wa tatu wa Bunge.


“Vilevile kwa niaba ya wabunge wote, tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutuwezesha kuhakikisha Bunge hili linaendelea, Miswada tunayoipitisha hapa anaipitisha kwa haraka bila kusita, tunaenedelea kufanya kazi na Serikali yake ambayo iko hapa,” alisema


“Shukrani kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye yupo hapa Bungeni, ametupa kila aina ya ushirikiano, shukrani pia kwa mawaziri wote, Kambi Rasmi ya Upinzani kwa changamoto mnazotupatia ambazo zimetusaidia kuendesha shughuli, shukrani kwa Kamati ya Uongozi na Kamati nyingine zote” alisema.


Awali akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Majaliwa alisema Katika Mkutano huu wa Bunge, Bunge lilijadili na kupitisha Bajeti za Wizara zote 19 pamoja na Bajeti Kuu ya Serikali.


Aidha, alisema Bunge limepitisha miswada mbalimbali pamoja na Maazimio matano ya kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kwamba pia lilipitisha Azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa hatua anazochukua za kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini.


“Katika Mkutano huu jumla ya maswali 499 ya msingi na mengine 1,834 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali kupitia kwa Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu,” alisema.


Alisema pia Bunge liliendesha semina mbalimbalimbai kwa waheshimiwa Wabunge kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi na kuwapa uelewa mpana wa masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Nchi.


“Bunge pia lilipata fursa ya kuchagua wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Wabunge tisa walichaguliwa


Aidha, aliwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani nchini ili wananchi waweze kushiriki shughuli za maendeleo bila hofu


Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ulinzi na usalama, afya, ardhi pamoja na masuala mbalimbali kuhusiana na Serikali za Mitaa


Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's