Parliament of Tanzania

Bunge laahirishwa hadi Januari 31

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameliahirisha Bunge hadi tarehe 31 Januri 2017.

Waziri Mkuu aliahirishwa Bunge kwa kuwasilisha hotuba yake Mezani ya tarehe 11 /11 2016 wakati wa kikao maalum cha Bunge kuomboleza kifo cha Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta.

Hotuba hiyo ambayo haikusomwa kutokana na msiba wa Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa Dimani, Zanzibar, iliwasilishwa Bungeni na kila mbunge kupata nakala.

Awali akiwasilisha hotuba hiyo mezani Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alisema “kwa mujibu wa kanuni za Bunge leo hii nilipaswa kutoa hotuba ya kuahirisha Mkutano wa tano wa Bunge kwa kuosoma hapa mbele yenu, Katika mazingira haya sitaweza kusoma hotuba yangu, naomba sana itoshe na iridhiwe nanyi kuwa hotuba hii iingie katika Hansard na katika tovuti ya Bunge na tovuti nyingine za serikali,”.

Katika hotuba yake hiyo, sehemu kubwa ilieleza shughuli mbali mbali zilizofanyika katika mkutano wa tano wa Bunge ikiwemo kupitisha kwa miswada miwili ambayo ni Muswada Sheria ya huduma za Habari 2016 na ule wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali 2016.

Shughuli nyingine zilizoelezwa katika hotuba hiyo ni pamoja na wabunge kupokea na kushauri kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2017/18, pamoja na wabunge kupokea na kujadili taarifa za kamati.

Mkutano wa Sita wa Bunge la Kumi na Moja ambao unatarajia kufanyika kwa wiki mbili kuanzia Tarehe 31 januari 2017 utatanguliwa na vikao vya Kamati za Bunge vitakavyoanza tarehe 16 Januari 2017 ikiwa ni kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, kuwa kabla ya kila mkutano wa Bunge kutakuwa na vikao vya Kamati .

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's