United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mkutano wa Tisa wa
Bunge la Kumi na Moja umeahirishwa hadi Januari 30, 2018 ambapo pamoja na mambo
mengine, Bunge limetoa onyo kali pamoja na kuwaagiza Wahariri wa Magazeti ya
Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kuchapisha habari za kuomba radhi Bunge katika
kurasa za mbele za magazeti yao ndani ya siku tano kuanzia tarehe ya Leo (17
Novemba, 2017,) kutokana na kosa la kuchapisha na kusambaza mwenendo wa
shauri lililokuwa likifanyiwa kazi na Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge.
Adhabu
hiyo imetolewa Bungeni leo wakati Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akitoa taarifa
fupi kuhusu shauri la kuvunja Haki na Kinga
za Bunge linalowahusu Wahariri na Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe na kumuagiza Mwanasheria
Mkuu wa Serikali awafikishe Mahakamani Wahariri hao iwapo watashidwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku
tano.
Mnamo tarehe 22 Septemba, 2017, magazeti hayo yalichapisha habari za mwenendo wa shauri na ushahidi uliotolewa na Mhe. Zitto Kabwe (Mb) mbele ya Kamati, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Kamati
ya Maadili ilipendekeza na hatimaye Bunge kuridhia adhabu hiyo kwa wahusika
baada ya kuzingatia kuwa Wahariri na Waandishi hao; waliitikia wito na kutoa
ushirikiano kwa Kamati, walikiri na kujutia makosa yao na kwa kuwa ni wakosaji
wa mara ya kwanza.
Wahariri
na Waandishi wa Habari waliohojiwa na Kamati ya Maadili ni; Ndg. Denis Msacky,
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Ndg. Bakari Kimwanga, mwandishi wa
habari wa gazeti la Mtanzania, Ndg. Angetile Osiah, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Ndg. Elias Msuya, mwandishi wa habari wa gazeti la
Mwananchi, Ndg. Edmond Msangi, Mhariri
Mtendaji wa gazeti la Nipashe na Ndg.
Gwamaka Alipipi, mwandishi wa habari
wa gazeti la Nipashe.
Kuhusu
Mheshimiwa Zitto, Spika wa Bunge aliliambia Bunge kuwa alitakiwa kufika mbele
ya Kamati hiyo kwa mara nyingine kwa ajili ya mahojiano kutokana na vitendo
vyake ya kuendelea kudharau Bunge, lakini bado hajaitikia wito na hivyo kwa
wakati muafaka Kamati hiyo itamhoji na hatimaye kupeleka taarifa yake Bungeni
kwa hatua zaidi.
Kwa
upande mwingine Spika wa Bunge Mheshimiwa Ndugai kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge, (Toleo la Januari, 2016,)
ameunda Kamati maalum mbili za Ushauri kuhusu namna ya kuliwezesha Taifa
kunufaika na sekta ndogo ya gesi na
Kamati maalum ya Ushauri kuhusu namna kuliwezesha
Taifa kunufaika na Sekta ya Uvuvi.
Kamati hizo
mbili zimeelekezwa kufanya kazi kwa muda wa siku thelathini kuanzia
tarehe watakayojulishwa na Katibu wa Bunge na baada ya kukamilisha kazi yake
itawasilisha taarifa kwa Spika ili taratibu zingine muhimu zifuate.
Wajumbe
walioteuliwa na Spika wa Bunge kuunda Kamati ya Ushauri kuhusu namna ya kuliwezesha Taifa kunufaika na sekta ndogo ya
gesi ni pamoja na; Mhe. Innocent
Lugha Bashungwa, Mb Mhe. Dustan Luka Kitandula, Mb, Mhe. Dkt. Suleiman Ally
Yussuf, Mb, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mb, Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa, Mb, Mhe.
Ruth Hiyob Mollel, Mb; Mhe. Richard Philip Mbogo, Mb; Mhe. Omar Mohamed Kigua,
Mb; Mhe. Abdallah Ally Mtolea, Mb; Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mb na Mhe. Doto M. Biteko, Mb - ambaye atakuwa
Mwenyekiti.
Kwa upande wa kamati
ya Ushauri kuhusu namna ya kuliwezesha
Taifa kunufaika na sekta ya Uvuvi, Mheshimiwa Spika amewatea wajumbe wafuatao;
Mhe. Mussa Azzan Zungu, (Mb). Mhe. Salum Mwinyi Rehani, (Mb), Mhe. Masoud
Abdallah Salim, (Mb); Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo, (Mb), Mhe. Mbaraka Kitwana
Dau, (Mb), Mhe. Dkt. Immaculate Sware Semesi, (Mb), Mhe. Dkt. Christine Gabriel
Ishengoma, (Mb), Mhe. Stanslaus Shing’oma Mabula, Mb, Mhe. Mussa Bakari
Mbarouk, (Mb), Mhe. Cosato David Chumi, (Mb) na Mhe. Anastazia Wambura, (Mb)- ambaye atakuwa Mwenyekiti.